0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ITIKADI YA MASHIA JUU YA QUR’ANI TUKUFU

ITIKADI YA MASHIA JUU YA QUR’ANI TUKUFU

Waislamu wote duniani wanaitakidi kwamba Qur’ani ni kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu aliyetukuka kilichokamilika,Hakina shaka ndani yake na ni uongofu kwa waumini. Kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

الم  ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ}  البقرة:1-2}

[Alif Lam Mim.Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu.]   [Al-Baqara:1-2]

hakiingiliwi na batili mbele yake wala nyuma yake, Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema:

لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ}   فصلت:42}

[Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.]    [Fuss’ilat:42]

Qur-ani ni kitabu kilichopangiliwa vyema, tena kwa ufanisi na ustadi wa hali juu! Mwenyezi Mungu aliyetukuka ndiye aliyekiteremsha kitabu hiki na yeye ndiye aliyeahidi kukihifadhi.Mwenyzi Mungu anasema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ}    الحجر:9}

[Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.]      [Al-Hijr:9]

Hii ndio itikadi ya kila muislamu anavyo itakidi juu ya Qur’ani tukufu,na sasa tutizame namna wanavyo itakidi mashia juu Qur’ani tukufu, na hili ni kwa mujibu wa vitabu vyao vakutegemewa.

ITIKADI YA MASHIA JUU YA QUR’ANI TUKUFU

MASHIA wanasema kuwa hii Qur’ani tuliyonayo si Qur’an ile Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu aliyetukuka kwa Mtume Muhammad ﷺ, bali imebadilishwa, ikazidishwa na kupunguzwa.

Wanachuoni wengi wa Shia wanaitakidi kwamba Qur’ani hii tuliyonayo ina upungufu; kwa madai ya kwamba kuna Aya zimepunguzwa hasa zile zinazotaja fadhila za Ali Ibn Abi Twalib radhi za Allah ziwe juu yake na kizazi chake, na Aya zinazompa haki ya Ukhalifa baada ya kufariki Mtume ﷺ.

Na haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mwanachuoni wao wakutegemewa Muhammad bin Ya’aquub Al-Kulayniy, katika kitabu chake “Usuulul-Kaafiy” katika mlango aliouita, ‘Hawakuikusanya Qur-aan yote isipokuwa Maimamu’ (anakusudia Maimamu wao wa ki-Shia), kisha akaleta riwaya ifuatayo:

 رواى الكليني في (الكافي) والصفار في (البصائر) عن جابر، قال: سمعت أبا جعفر (عليه السلام) يقول: “ما ادعى أحدٌ من الناس أنّه جمع القرآن كلّه كما أُنزل إلاّكذّاب، وما جمعه وحفظه كما أنزله الله تعالى إلاّ علي بن أبي طالب (عليه السلام) والاَئمّة من بعده (عليهم السلام).

Kutoka kwa Jaabir, amesema: Nilimsikia Abu Ja’afar akisema: “Hajapata kudai mtu yeyote kuwa kaikusanya Qur-aan yote kama Alivyoiteremsha Allaah ispokuwa atakuwa ni muongo. Hakuna aliyeikusanya na kuihifadhi kama alivyoiteremsha Allaah isipokuwa ´Aliy bin Abi Twaalib na Maimamu baada yake.”   [Usuulul-Kaafi:1/228 na Al-Baswaair: 2/213.

 عن جابر، عن أبي جعفر (عليه السلام)، أنّه قال: “ما يستطيع أحد أن يدّعي أنّ عنده جميع القرآن كلّه ظاهره وباطنه غير الاَوصياء. الكافي 1: 228 | 2، بصائر الدرجات: 213 | 1

Na imepokewa toka kwa Jaabir toka kwa Ja’afar kwamba amesema: “Hawezi kudai mtu yeyote kwamba anayo Qur-aan kamili isipokuwa walioachiwa wasia.”

عن هشام بن سالم عن ابي عبد الله عليه السلام قال : إن القرآن الذي جاء به جبرائيل عليه السلام إلى محمد صلى الله عليه وسلم سبعة عشر ألف آية.

Na imepokewa kutoka kwa Hishaam bin Saalim, toka kwa Abii Abdillaah (Ja’afar) amesema: “Hakika Qur-aan aliyokuja nayo Jibriyl kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni aayah 17,000.”

Maana ya maneno hayo ni kuamanisha ya kuwa Qur’ani tuliyonayo imepungua aya nyingi sana,kwa sababu Qur’ani hii tuliyonayo iko na aya 6000 na kitu na hii ni kumanisha kuwa nusu ya mswahafu umepunguwa. Qur’ani hii ambao Mwenyezi Mungu ameahidi kuifadhi.

Anamesema mwanachuoni wa kishia katika utangulizi wa tafsiri yake naye Abul-Hasan Ibn Muhammad Twahir Al-Aamiliy,

اعلم أن الحق الذي لا محيص عنه بحسب الأخبار المتواترة الآتية وغيرها أن هذا القرآن الذي في أيدينا قد وقع فيه بعد رسول الله صلى الله عليه وسلم شيء من التغييرات ، وأسقط الذين جمعوه بعده كثيرا من الكلمات والآيات.

“Jua ya kwamba, jambo la haki lisilokwepeka kutokana na habari Mutawaatiri zifuatazo na nyinginezo ni kwamba: Qur-ani hii ambayo imo mikononi mwetu imeingiliwa na mabadiliko baada ya (kufa) Mtume ﷺ Wale walioikusanya (Maswahaba) wameondosha baada ya (kufa) Mtume ﷺ

maneno mengi na Aya nyingi….”

Na mpaka kupelekea kwa Mwanachuoni wao kuandika kitabu cha kuthibtisha kuwa Qurani tulionayo imepunguwa na kubadilishwa.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.