0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ITIKADI YA AL-BADAA

ITIKADI YA AL-BADAA

Al-Badaa maana yake ni kudhihiri baada ya kutoweka, au kwa maana ya kuanzishwa kwa rai mpya. Na neno hili (Al-Badaa kwa maana zote mbili linamaanisha kuwepo hali ya kutojua jambo kisha kujua kunakuja baadae, na mambo yote haya mawili kwa Allaah ni muhali. Raafidhwah wanainasibisha sifa hii ya ( Al-Badaa) kwa Allaah.

 عن الريان بن الصلت قال: سمعت الرضا (ع) يقول:” ما بعث الله نبيّاً قط إلا بتحريم الخمر وأن يقرّ لله بالبدا” [الكليني في الكافي 1/148].

Imepokewa kutoka kwa Rayyaani bin As-Swalt kwamba amesema:  “Nilimsikia Ar-Ridhwaa akisema: [Hajapata Allaah kumtuma Nabii yoyote ispokuwa kwa kuharamisha pombe na kukiri (Al-Badaa) kuwa ni katika sifa za Allaah.].

Na kutoka kwa Abdullaah amesema:

[“ما عبد الله بشيء مثل البداء”  [أصولالكافي، كتاب التوحيد، باب البداء: 1/146

[Hakuna alioko katika Mbingu na Ardhi ajuae Ghaybu (yasioonekana au yasiyojulikana) ila Allaah” [An-Naml : 65].

Badala yake wanaitakidi kuwa Maimamu wao wanajua elimu zote, wala halifichikani kwao jambo lolote. Je, hii inaweza kuwa itikadi ya Uislamu aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu  ́alayhi wa sallam)?

Na itikadi hii ya Al-badaa ndio itikadi ya Mayahudi kama yalivyo kuja kwenye katika cha Bibilia Mwanzo, Sura ya Sita, ya ya 5

“Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.

6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.”

CHANZO CHA ITIKADI YA  AL-BADAA

Wanachuoni wakishia walikuwa wakiwaelezea wafuasi wao kuwa ungozi na utawala utarudi kwao na kuwa Dola itakuwa yao, na wakaweka mda wa miaka sabiini na kuna riwaya walio inasibisha kwa Imam Al-Jaffar Al-Swadiq juu ya hilo,ulipo pita mda huwa na kuwa yale walio kuwa wakiahidi wafuasi wao hayakutimia na wafuasi wakawa ni wenye kuliza kwa nini miaka 70 imepita na hali na Ungozi hawajarudi kwao, ndio hapo wakatafuta njia na mbinu za kutaka kuwakinaisha wafuasi wao wakanzisha itakadi hii ya Al-Badaa, Kuwa Allah subhanahu wataala ameonelea kubadilisha wakati na tarehe ya uongozi huo.

tazama haya katika kitabu cha Tafsiri Al-Ayyaashiy 2/218 na kitabu cha Al-Ghayba ukurasa 263 na kitabu cha Biharul-Anwaar 4/214

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.