HUKMU YA KUTUMIA MAJI YALIO TUMIWA
Swali: Je yafaa mtu kutumia maji yalio tumiwa kujitwayarisha kukamilishia Udhu wake. Mfano; mtu akayakusanya maji ya kutawadhia kwenye chombo kisha maji
yale akayatumia katika kuoshea miguu je yafaa kufanya hivyo?
Jawabu: Kutumia maji yaliotumika katika twahara ni katika Mas’ala wanchuoni walio ikhtilalifiana sawa au si sawa katika kuyatumia maji yale kukamilisha Udhu au kutawadhia upya.
Madh’habu ya Imamu Malik anaona yafaa kutumia kwa sababu maji yale ni twahara na waweza kutwahirishia ikiwa maji yale hayakubadilika lakini ni Makruhu kutumia.
Na msimamo huu ndio msimamo wa Sheikhul islam Ibn Taimiyah. Asema kwa sababu maji yalio tumika katika kuondoshea hadathi yamebaki katika utwahara wake,na imesihi
kutoka kwa Mtume ﷺ Akisema:
[إن الماء طهور لا يُنجِّسُه شيء] رواه أبو داود ، والترمذي
[Hakika ya Maji ni Twahara hayanajisiki kwa kitu chochote] [Imepokewa na Abuu
Dawud na Attirmidhiy]
Maji hayawezi kuwa na janaba,wala hayawezi kuchukuwa hukmu ya janaba.
Lakini msimamo wa wengi katika wanachuoni wanaona maji yalio tumiwa hayafai kuyatumia katika kuondoshea hadathi. sawa iwe ni hadathi ndogo kama kutawadhia, au Hadathi kubwa, kama kuoga janaba na msimamo huu ndio msimamo wa wengi na ni katika kujiondoa kwenye shaka na khilafu.
Kwa hivyo itakuwa ni bora kutumia maji ambao hajatumiwa katika kuondoshea hadathi sawa kukamilishia Udhu au kutawadhia.
Na allah ndie Mjuzi zaidi.