HUKMU YA KUKAUKA KWA NGUO ILIO NAJISIKA
Swali: Ni nini hukumu yanajisi iliokauka na kupotea athari yake. Kama vile rangi au harufu na kadhalika.
Jawabu: Nguo ilioingia najisi kisha ikikauka na kupotea athari ya najisi kama vile rangi au harufu au tamu kwa kupigwa na jua au kwa jambo lolote lile kwa msimamo wa jamhuri ya wanchuoni ni kuwa nguo haitwahiriki kwa kukauka ni lazima itwahrishwe kwa Maji.
Pia wameenda baadhi ya wanachuoni wakasema kuwa najisi ikiondoka na kupotea athari yake kama vile rangi au harufu au tamu yake basi chombo kile huwa ni twahara.
Kwa sababu lengo la kuondoa najisi ni kuondosha ile najisi ilioko kwenye nguo ikiwa itaondoka kwa kitu chochote kile kama banzin au mafuta ya taa basi kitu kile hutwahirika.
Ameulizwa Sheikh Ibnu Uthaymin Mungu amrehemu katika Majmuuil Fatawa. “Je najisi hutwahirika kwa kitu kingine kisichokuwa maji? Na bukhari inaosafishiwa nguo kwenye sehemu za kufulia nguo ni yenye kutwahirisha?
“Akajibu kuondosha najisi si ibada iliokusudiwa, bali ni kuondosha ule uchafu wa najisi kwa hivyo kitu chochote chenye kuondosha najisi na ikaondosha na kuondosha athari yake, basi huwa kitu kile ni chenye kutwahrisha najisi ile, sawa iwe ni kwa maji au petroli au kitu chochote chenye kuondosha, uchafu wa njisi basi huhisabiwa ni chenye kutwahirisha. Hata kauli ambao ndio sawa alioichaguwa Sheikhul Islam Ibnu Taymiyah, lau najisi itaondoka kwa jua na upepo basi hutwahirika ile sehemu. Kwa sababu ni Kama nilivyosema uchafu wa wanajisi ukipatikana sehemu huwa sehemu ile ni najisi,na itakapoondoka sehemu ile hurudi kwenye asili yake, nao ni utwahara.
Kwa hivyo na kitu chochote chenye kuondosha najisi na athari yake, isipokuwa husamehewa rangi ilioshinda kuondoka. Kwa hivyo tunasema Bukhari inaosafishiwa nguo ikiwa itaondosha najisi basi huwa ni yenye kutwahirisha”.
Kwa hivyo kupitia kwa misimamo hiyo miwili ya wanchuoni,najisi ikikauka na kupotea athari yake huwa kitu kile ni twahara, lakini msimamo wa jamhuri ni kujitoa kwenye shaka na khilafu
Na Allah ndie mjuzi zaidi.