HUKMU YA KUTAWADHA NA MAJI YALIO INGIA MENDE
Swali : Mende/Kombamwiko akiingia kwenye maji kidogo ambao hajafikia Qullatayn maji yale hunajisika?
Jibu: kuingia wadudu ambao hawana damu kama vile mende,inzi na wengineo kwenye maji au yasio kuwa maji basi hayanajiski. Hata maji yakawa ni kidogo,hata kama atafia ndani na huu ndio Msimamo wa Jamhuri ya wanchuoni. Maji yale yatakuwa yafaa kutumia katika ibada kama kujitwahirishia au ada kama kunywa na
kupikia,kwa Hadihti iliopokelewa na imamu Bukhari:
عن أبي هريرة ـرضي الله عنه ـ أن النبي صلى الله عليه و سلم قال:إذا وقع الذباب في شراب أحدكم فليغمسه كله ثم ليطرحه، فإن في أحد جناحيه داءً، وفي الآخر دواءً.
Kutoka kwa Abuu Hurayra radhi za Mungu zimfikie yeye,kwamba Mtume rehma na amani zimfikie yeye, asema:
[Inzi anapo ingia katika kinywaji cha mmoja wenu basi naamzamishe yeye mzima kisha amtoe,kwa sababu kwenye ubawa wake mmoja uko na ungonjwa,na mwengine uko na dawa].
Asema Ibnul Qayyim katika kitabu chake ‘Al-Zzaad’ hadithi hii ni dalili ilo wazi kwamba inzi anapo kufa kenye maji au vitu vya majimaji,havinajisiki,na hii ndio kauli ya jamhuri ya wanachuoni. Wala hajulikani katika Salaf (watu wema walio tangulia) mwenye kukhalifu hilo. Kisha hukmu yake ikaenea kwa wadudu wote wasio kuwa na damu ya kutirizika kama vile,nyuki, na Zanbur (wasp) na Ankabut (spider) na mfano wa hao.
Na baadhi ya wanchuoni wamemtoa Mende wa choni na kila mdudu alitokamana na najisi, wakasema kila mdudu alitoka kwenye kitu twahara huwa ni twahara. Mdudu alitoka kwenye najisi huwa ni najisi.
Kiufupi ni kuwa wadudu wasio kuwa na damu wanapo ingia kwenye maji au kitu chochote, kitu kile au maji yale huwa ni twahara wala si najisi.
Wallahu aalam.