HUKMU YA KUINGIA CHOONI NA KASETI ZA QUR’ANI
Swali : Yafaa mtu kuingia Chooni na kaseti ya Qur’ani au na simu ilohifadhi ndani yake Qur’ani?
Jawabu: Kwanza kabisa ni makruhi mtu kuingia Chooni na kitu chochote kulichoandikwa jina la Mwenyezi Mungu au kitu chochote kilichoandikwa chochote kuhsu Qur’ani Tukufu.
Na Madhehebu ya Jamhuri ya Wanachuoni katika dhehebu la Imamu Abuu Hanifa na Imamu Malik na Shafii Mungu awarehemu kuwa ni Makruhu mtu kuingia Chooni na Dirhamu ilioandikwa jina la Mwenyezi Mungu na haikusitiriwa, Lakini ikiwa limesitiriwa basi huondoka ukaraha wake, na huu ni msimamo Vile vile wa Imam Ahmad katika moja ya riwaya zake,
Ama kuingia Chooni na kaseti za Qur’ani au Simu ilohifadhiwa ndani yake Qur’ani na ikawa haikuwekwa nje ya Screen basi itakuwa yafaa kwa sababu haingii katika katazo waliloelezea Wanachuoni kuwa ni Makruhu kuingia Chooni na kitu chochote kilichoandikwa Jina la Mwenyezi Mungu kwa kutopatika herufi zilizo wazi ndani yake.
Na Allah ndie mjuzi zaidi