SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hikma ya kuwajibisha kutoa Zaka?
Jawabu: Hekima ya watu kuwajibika kutoa Zaka ni kama zifuatavyo:
1. Ni kuzisafisha nafsi na kuzitakasa kutokana na ubakhili, na madhambi, na makosa, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ} التوبة:103
[Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao] [suratu At-Tawbah: 103]
2. Kusafisha mali na kuikuza, na kutia baraka ndani yake, kwa kauli ya Mtume ﷺ:
{ما نقصت صدقة من مال} رواه مسلم
[Sadaka haipunguzi chochote (inapotolewa) katika mali] [Imepokewa na Muslim.].
3. Ni mja kupewa mtihani katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na katika kutanguliza mapenzi yake kwa Mungu zaidi kuliko mapenzi yake ya kupenda mali.
4. Kuwaliwaza mafakiri na kuziba pengo la mahitaji ya wenye haja, jambo ambalo linaongeza mapenzi, na linatimiliza kiwango cha juu sana katika usaidizi wa kijamii baina ya waislamu wa eneo moja.
5. Kujizoezesha katika kutoa kwa njia ya Mwenyezi Mungu.
FADHLA YA KUTOA ZAKA
Suali: Ni zipi Fadhla ya kutoa zaka?
Jawabu: Fadhlaya kutoa zaka ni kama zi fuatavyo:
1. Ni sababu ya kupata Rehema za Mwenyezi Mungu, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
[Na rehema yangu inaweza kukienea kila kitu. Lakini nitawaandikia (kweli kweli kabisa) wale wanaojikinga na yale niliyowakataza, na wanaotoa Zaka na wanaoziamini Aya zetu] [Al-A’raf: 156]
2. Ni sharti ya kupatikana Nusra ya Mwenyezi Mungu, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌالَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ ۗ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ
[Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia dini yake.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Wale ambao tukiwamakinisha, (tukiwaweka uzuri) katika ardhi husimamisha Swala na wakatoa Zaka] [Al-hajj 40-41]
3. Ni sababu ya kufutiwa madhambi, Amesema Mtume ﷺ:
[وَالصَّدَقَةُ تُطْفِئُ الْخَطِيئَةَ كَمَا يُطْفِئُ الْمَاءُ النَّارَ] رواه الترمذي
[Na sadaka hufuta madhambi kama vile maji yanavyozima moto] [Imepokewa na Tirmidhi.].