AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Yalipokamilia Maamuzi ya dhulma ya kumwua Mtume (ﷺ), aliteremka Jibril (Alayhi Salaam) akiwa na wahyi kutoka kwa Mola wa viumbe Aliye Mtukufu na Alimueleza njama za Makuraishi dhidi yake na kuwa Mwenyezi Mungu (ﷻ) Amempa ruhusa ya kuhama na akampangia wakati wa kuhama kwa kusema: ”Usiku huu Usilale juu ya tandiko lako unalolalia kila siku.” (1)
Mtume (ﷺ) akaenda kwa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) mchana ili wamalizie taratibu za safari yao ya Hijra. Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisemaa “Wakati sisi tumekaa nyumbani kwa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) mchana, alisema msemaji kumwambia Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake), Angalia, Huyu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) amejifunika uso’, ulikuwa ni wakati ambao si kawaida yake kutujia kuna jambo lililomletaz Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema, ”Ukombozi ni wake, kwa baba yangu na mama yangu, kuna jambo lililomleta saa hizi.” Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisemaa ”Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ), akapiga hodi akaruhusiwa, akaingia”, na akasema Mtume (ﷺ) kumwambia Abubakar (r.a), ”Watoe nje walioko ndani”, Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: ”Kwa hakika hawa ni watu wako – ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Mtume (ﷺ) akasema, “Kwa hakika mimi nimeruhusiwa kuhama.” Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema: ”Ninaomba nifuatane na wewe ninakukomboa kwa baba yangu na mama yangu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ).” Naye Mtume (ﷺ) akajibu, ”Ndiyo (2)
Baada ya kukamilisha mazungmnzo yao juu ya mpango wao wa kuhama Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alirejea nyumbani kwake, akiungojea usiku.
Kuzingirwa kwa Nyumba ya Mtume (ﷺ )
Wakubwa wa waovu wa Makuraishi waliutumia mchana wao katika maandalizi kwa ajili ya kuutekeleza mpango uliokwisha amuliwa na Bunge lao wakati wa asubuhi. Kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo walichaguljwa viongozi kumi na wawili: –
1. Abu Jahli bin Hisham
2. Al- Hakama bin Abiy Al-’Assi
3. ’Uqbah bin Abiy’Muait-i
4. Al-Nadhri bin A1-Harith
5. Umayya bin Khalaf
6. Zam’a bin Al – Aswad
7. Tuaymah bin Adiyy
8. Abu Lahb
9. Ubay bin khalaf
10. Nabih bin Al-Hajjaji
11. Ndugu yake Munabbihi bin Al- Hajjajim. (3)
Ibn Ishaq amesema, ”Kilipoingia kiza walikutana makafiri mlangoni mwa nyumba ya Mtume (ﷺ ) wakimsubiri atakapolala wamvamie. Walikuwa na mategemeo makubwa ya kufanikiwa kwa njama hizo. Abu Jahl alisimama kwa kiburi na kuwahulubia wenzake walioizingira nyumba ya Mtume (ﷺ ) kwa kufanya maskhara na kumcheza shere Mtume (ﷺ ), “Muhammad anadai kwamba iwapo mtamfuata katika dini yake mtakuwa wafalme wa Waarabu na Waajemi, na kisha kufufuliwa baada ya kufa kwenu mmefanyiwa mabustani kama mabustani ya Jordan. Iwapo hamtamfuata na kufanya kazi mliyotumwa basi atakuchinjeni, na baadaye mtafufuliwa baada ya kufa kwenu, kisha mtatupwa motoni na kuchomwa (4) Walikuwa wamekubaliana kumwua baada ya nusu ya usiku, wakaupitisha usiku wakiwa macho wakingojea saa ya kupulizwa kipenga. Mwenyezi Mungu (ﷻ) ni Mwenye Kushjnda hila zote. Uko mikononi Mwake Ufalme wa mbinguni na ardhini, Anafanya Alitakalo, na Yeye Ndiye Anayenusuru viumbe, kwa hakika Aliyafanya yale ambayo Alimwahidi kwayo Mtumé (ﷺ). Baada ya hapo Anamkumbusha Mtume (ﷺ) :
وَإِذۡ يَمۡكُرُ بِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيُثۡبِتُوكَ أَوۡ يَقۡتُلُوكَ أَوۡ يُخۡرِجُوكَۚ وَيَمۡكُرُونَ وَيَمۡكُرُ ٱللّهُۖ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلۡمَٰكِرِينَ
”Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango ” (8:30) 2 9 1
Mtume (ﷺ) Anaiacha Nyumba yake:
Pamoja na ukamilifu wa maanaalizi ya Makuraishi katika kuutekeleza mpango wao, kwa hakika walishindwa vibaya sana. Usiku huo Mtume wa Mwenyezi (ﷻ) alimwambia Ali bin Abu Twalib; ‘Lala juu ya tandiko langu, na jifunike shuka yangu hii ya kihadharami ya kijani, hakitapenya kwako kitu unachokichukia.’ Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikuwa akilala katika shuka yake hiyo. (5)
Kisha, Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alitoka na kuzipenya safu zao, akachukua gao la mchanga, akawa anaunyunyiza juu ya vichwa vyao, wakati huo Mwenyezi Mungu (ﷻ) Ameyakamata macho yao hawamuoni, akatoka huku akisoma:
وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ سَدّٗا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدّٗا فَأَغۡشَيۡنَٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni. (36: 9)
Katika wao hakuna aliyesalimika, wote walikuwa wamewekwa mchanga katika vichwa vyao. Mtume (ﷺ) akaenda nymnbani kwa Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake), wakatokea katika mlango mdogo katika nyumba ya Abubaka (Radhi za Allah ziwe juu yake) na kuondoka usiku huo huo mpaka wakafika katika pango la Thouri uelekeo wa Yemen. Wazingiraji walikuwa bado wanasubiri kufika kwa saa ya kupigwa kipenga, na nyuma kidogo kabla ya kufika kwa muda huo kuliwadhihirikia kushindwa kwao.
Alikuja mtu ambaye hakuwa pamoja nao tokea mwanzo, akawaona wakiwa mlangoni kwa Mtume (ﷺ) akawauliza; ”Ni kitu gani mnachokingojea hapa?.” Wakamjibu; “Muhammad.” Akawaambia, ”Mmetoka kapa na mmepata hasara, ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, amewapitieni na nyote amekunyunyizieni mchanga vichwani mwenu, na ameondoka kama alivyokuwa amepanga.” Wakasema, ”Kwa hakika hatukumwona,” Wakasimama huku wakikung’uta michanga kutoka vichwani mwao,-kabla ya kuchukua hatua yoyote usiku ule walichungulia katika upenyo wa mlango na wakamwona mtu amelala katika tandiko la Mtume (ﷺ), wakasema, ”Kwa hakika Muhammad bado amelala na ile ni shuka yake, waliendelea na hali hiyo mpaka wakapambazukiwa”, na Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasimama kutoka katika tandiko. Wakafedheheka. Wakamwuliza kuhusu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w), akawajibu, ”Sina ujuzi wa khabari zake.