0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MJADALA WA BUNGE NA KUAFIKIANA KUMWUA MTUME ﷺ


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya kukamilika mkutano mapendekezo ya ufumbuzi yalianza kutolewa, na baada ya mjadala mrefu: Abul-Aswad alisemaz “Tumtoe katika nchi yetu na hatujali wapi atakwenda wala wapi ataangukia, kwani tutakuwa tumekwisha kulitengeneza jambo letu na umoja wetu utarudi kama ulivyokuwa huko nyuma.” Mzee wa Najdi naye akachangia; “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu haya si maoni wala rai nzuri. Hivi hamuoni uzuri wa maneno yake na utamu wa matamshi yake, na uwezo wake wa kushawishi nyoyo za watu, kutokana na yale anayoyaleta? Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kama mtafanya hivyo hamuwezi kuwa katika amani, kumwacha aishi kafika kabila lolote la Waarabu ni makosa kwani atakuja nao (Wakisha kuwa wafuasi wake) kuja kukupigieni kisha awakanyageni nyinyi pamoja na watu hao katika nchi yenu, na baada ya hapo atawafanyia lile analolitaka, toeni rai nyingine isiyokuwa hiyo.‘ Abul-Buhfury alisema: ”Tumfugie chumbani katika chuma na tumfungie mlango na kisha yampate yale ambayo yaliwapata watu miongoni mwa washairi waliokuwa kabla yake (Zuhair, na Nabigha) na waliopita katika wao kutokana na aina hii ya kifo.” Mzee wa Najdi akasema: ”Hapana: Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu nayo hii si rai nzuri vile vile. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu iwapo mtamfunga – kama mnavyosema itatoka da’awa yake kupitia mlango mwingine, ambao mmeufunga na itafika kwa Masahaba zake, kwa hiyo watawajia na kukushambulieni na kumpokonya kutoka mikononi mwenu, baada ya hapo watajifakharisha kwenu kwa wingi wao, mpaka wawashinde. Maoni yenu haya si ya busara hivyo tafuteni rai nyingine.”

Baada ya Bunge kuyakataa mapendekezo haya mawili, yalitolewa mapendekezo mengine mabaya ambayo wajumbe wote waliyakubali. Mapendekezo hayo aliyatowa mkubwa wa waovu wa Makka, Abu Jahal bin Hisham. Abu Jahal alisema; ”Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ya kuwa na mimi nina maoni katika jambo hili, sikuwaona mkiyataja katika maoni hayo”, Wakasema, ”Ni maoni gani hayo ewe Abal -Hakam?’ Akasema: ”Ninaonelea tuchukue kutoka kila kabila kijana aliye imara, mwenye nasaba atakayetuwakilisha, kisha tumpe kila Kijana katika wao upanga mkali na baada ya hapo waende kwake na kumpiga kwa panga hizo (kwa pamoja) pigo moja wamwue. Bila shaka baada ya hapo tutapumzika naye. Kwa kufanya hivyo damu yake itagawanyika katika makabila yote, na Banu Abdi Manafi hawataweza kupigana na jamaa zao wote, na kwa hivyo wataridhia fidia kutoka kwetu.” Mzee wa Najdi akasema: ”Maneno ni haya aliyosema mtu huyu, haya ndiyo maoni yanayofaa.” Bunge la Makka likaafiki mapendekezo hayo mabaya. Wabunge wakarejea majumbani kwao na azma ya kuyatekeleza maamuzi hayo haraka iwezekanavyo.


1) Ibn Hisham, Juzuu 1,Uk. 480-482.

Begin typing your search above and press return to search.