HARAMU ( 1 )
يقول رب العزة سبحانه : {قل إنما حرم ربي الفواحش ما ظهر منها وما بطن والإثم والبغي بغير الحق وأن تشركوا بالله ما لم ينزل به سلطانا وأن تقولوا على الله ما لا تعلمون} الأعراف:33
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu
[Sema (uwaambie): “Mola wangu ameharimisha (Haya: Ameharimisha) mambo machafu, yaliyodhihirika na yaliyofichika, na dhambi na kutoka katika taa (ya wakubwa) pasipo haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia dalili (ya kusema kishirikishwe naye) na (ameharimisha) kusema juu ya Mwenyezi Mungu msiyoyajua.] [Al Araaf: 33]
Tambua kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu hajahalalisha ila jambo jema na hajaharamisha ila jambo baya.
Aliulizwa mmoja katika waarabu kwanini umesilimu, akasema “ sijaona kitu katika maneno au vitendo vinavyopendeza katika akili na utu wa mwanadamu isipokuwa uislamu umelihalalisha jambo hilo na umelisisitiza kufanyiwa kazi , na sijaona kitu katika maneno au vitendo vinavyochukiza katika akili na utu wa mwanadamu isipokuwa uislamu umeharamisha na kukemea jambo hilo.
Ni nini haramu ?
Ni zipi athari za haramu ?
Ni vipi vigawanyo vya haramu ?
Kwanini tunatumbukia katika matatizo ya haramu ?
Ni upi msimamo wa muislamu juu ya haramu ?.
MAANA YA HARAMU
Haramu kilugha ni kinyume cha halali na ni kile ambacho haifai kukiendea. Imam Arraazy.
Na Haramu kisheria ni kila alichokitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake wakiache kwa ulazima na adhabu kali kwa yule atakayekwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu Subhanahu wata’ala.
Kuhalalisha na kuharamisha ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na haifai kiumbe chochote kuingilia au kujihusisha na haki hii ya ALLAH Jalla jalaaluh.
دخل عدي بن حاتم وكان نصرانيا على النبي عليه الصلاة والسلام، وسمعه يقرأ قول الله تعالى: اتخذوا أحبارهم ورهبانهم أربابا من دون الله
قال: يا رسول الله ما اتخذناهم أربابا، لم نسجد لهم، قال: [ألم يحلوا لكم الحرام ويحرموا عليكم الحلال فأطعتموهم؟ قال: بلى، قال: فذلك عبادتكم إياهم] مختصر ابن كثير مجلد 2 ص 137
Siku moja alikuja Udeyy bin Haatim (alikuwa mnaswara) kwa bwana Mtume MUHAMMAD ﷺ akamsikia anasoma Qur’ani aya hii akasema ewe Mtume ﷺ hatujawafanya miungu na wala hatujawasujudia, akasema Mtume ﷺ je hawajahalalisha haramu na hawajaharamisha halali ? akasema naam, akasema Mtume ﷺ basi hiyo ndio ibada yenu juu yao. [Mukhtasar wa Ibn Kathiir , Mjeledi wa 2 , ukurasa wa 137 ] .
Kila unayemtii katika jambo ambalo ndani yake kuna maasia basi ujue umemshirikisha Mwenezi Mungu mtukufu.
Kila kinachopelekea katika haramu ni haramu , zinaa ni haramu ALLAH Subhanahu wa Ta’ala ameseme katika Qur’ani:
{وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا} الإسراء:32
[Wala mskikaribie zinaa. Hakika hiyo(zinaa) ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa).] [Al Israa: 31]
Na wala hajasema na musifanye uzinifu , ni wajibu wa kila mtu kujiweka mbali na kila njia yenye kupelekea katika uzinifu kama picha chafu , kumgusa mwanamke asiyekuwa halali yako na mengineyo …
Halali iko wazi na haramu iko wazi na haramu iko wazi , na likikuchanga baina ya halali na haramu basi jiepusheni kuhofia kuingia katika haramu .
Uislamu umekataza kuuza kitu chochote cha haramu au kukitoa zawadi maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akiharamisha jambo anaharamisha na thamani yake.
جاء رجل إلى النبي وذكر للنبي عليه الصلاة والسلام أن عنده خمرا، وأنه يعلم بتحريم الله عز وجل له فقال: يا رسول الله أفلا أكارم بها اليهود (أي أهديها إلى اليهود) فاليهود يشربون الخمر، فقال عليه الصلاة السلام: [إن الذي حرمها حرم إهداءها] رواه الحميدي في مسنده
Alikuja mtu mmoja kwa bwana mtume Muhammad ﷺ akamueleza kuwa ana pombe nymbani kwake na anajuwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kaharamisha , akasema kumwambia mtume ﷺ je naweza kuwakirimu mayahudi kuwapatia zawadi ? kwani mayahudi wanakunywa pombe , akasema Mtume ﷺ hakika yule aliyeharamisha pombe ndiye aliyeharamisha kuitowa zawadi . [Imepokelewa na Al Humaydiy katika Musnad yake].
Inaendelea
©Abu-Khalfan Assarawi
[email protected] / [email protected]
+255656333678
03/03/2017