0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HALI ZA ALIYE KWENYE ISTIHADHA

SOMO LA FIQHI

HALI YA KWANZA:

Awe na ada inayojulikana ya siku zake za hedhi kabla ya kujiwa na istihadhah:

Huyo atahesabu siku za kadiri ya ada yake kuwa ni hedhi na zinazosalia katika mwezi ni istihadhah, kwa hadithi ya ‘Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Fatimah binti Abi Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Mimi sitwahiriki, je niache kuswali? Mtume akamwambia

[اجتنبي الصلاة أيام حيضك ثم اغتسلي وتوضئي لكل صلاة ، ثم صلي]

[Acha kuswali kadiri ya siku zako za kuingia hedhini, kisha oga na utwadhe kila Swala kisha uswali]    [Imepokewa na Bukhari.].

HALI YA PILI:

Asiwe na ada inayojulikana, lakini anaweza kupambanua baina ya damu ya hedhi na damu ya istuhadhah:
Basi huyu atatumia upambanuzi wake, kwa ilivyothubutu kwamba Fatimah binti Hubaish Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa kwenye damu ya istihadha, Mtume akamwambia:

[إن دم الحيض دمٌ أسود يُعرِف، فإذا كان ذلك فأمسِكي عن الصلاة، فإذا كان الآخر فتوضَّئِي وصلِّي]

[Hakika damu ya hedhi, ni damu nyeusi inayojulikana. ikija, acha kuswali, na ikija ile nyingine tawadha na uswali, kwani damu hiyo ni kishipa]   [Imepokewa na Abu Daud.].

HALI YA TATU:

Asiwe na ada Maalumu na asiweze kupambanua:
Basi huyo atatumia ada za wengi wa wanawake, hivyo basi hedhi itakuwa ni siku sita au saba katika kila mwezi, ataanzia mwanzo wa kipindi anapoona damu, na siku zilizosalia zitahesabiwa ni istihadha. Hii ni kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia Hamnah binti Jahsh Radhi za Allah ziwe juu yake.

فتحيَّضي ستَّة أيَّامٍ أو سبعةً، ثمَّ اغتسلي، فإذا اسْتَنْقَأْتِ فصلِّي أربعةً وعشرين، أو ثلاثةً وعشرين، وصُومي وصلِّي؛ فإن ذلك يُجزئُك، وكذلك فافعلي كما تحيضُ النساءُ

[Basi hesabu kuwa wewe uko hedhini kwa siku sita au siku saba kisha oga, ukitakasika, basi swali kwa masiku ishirini na tatu na Ufunge na uswali, kwani hilo linakutosheleza. Na ufanye hivyo kama wanavyohidhi wanawake]    [Imepokewa na Abu Daud na At Tirmidhiy.]

Kwa hivyo atafanya kama wanavyotwahirika wanawake wengine, kulingana na nyakati zao za hedhi na utwahara.

HALI YA NNE:

Awe na ada Maalumu na aweze kupambanua:
Huyu atazingatia ada na siyo kupambanua, kwa kuwa ada ina udhibiti zaidi kwa mwanamke. Na anaposahau ada yake basi atatumia upambanuzi.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.