0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

 MAANA YA UISLAMU

Ni nini Maana ya Uislamu:

Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, na Kunyenyekea kwake kwa kumtii,na Kujiepusha na Shirk, na kuwa mbali na Washirikina.
Dalili ni neon lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

وَمَنْ أَحْسَنُ دِينًا مِّمَّنْ أَسْلَمَ وَجْهَهُ لِلَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ وَاتَّبَعَ مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا ۗ وَاتَّخَذَ اللَّهُ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلًا}       النساء:125}

“Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.”     [Al-Nnisaa: 125]

Na neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

فَإِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ}      الحج:34}

[Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu, tuJisalimishieni kwake na wabashirie wanyenyekevu]    [Al-Hajj:34

Na Amesema tena:

وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ}     لقمان:22}

“Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti.”     [Luqman:22]

Na Uislamu ndio Dini ya Mitume wote, Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema:

 إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ}       آل عمران:19}

[Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu]    [ Al-Imran: 19]

Na amesema tena:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ}     آل عمران:85}

[Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.]    [ Al-Imraan:85]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.