0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

DARAJA ZA DINI


Daraja za Dini ni Tatu
Daraja ya kwanza: ni Uisalmu
Daraja ya pili: ni Imani
Daraja ya tatu: ni Ihsaan

MAELEZO

Mtu anapo piga shahada na Kushuhudia ya kuwa hapana Mola Apasae Kuabudiwa kwa haki ila Mwnyezi Mungu, na Kushuhudia kuwa Mtume Muhammad ni Mtume wa Mungu huwa Ashakuwa Muislamu,na anapo fanya matendo mema, na kufuata Mafunzo ya Uislamu hupanda daraja ya kuwa mua’min, na akizidisha twaa na akajitahidi kujikurubisha zaidi kwa mwenyezi mungu hufika daraja ya Ihsan,ikawa anapo fanya ibaada ni kama kwamba anamuona mwenyezi Mungu (S.W)

Ni ipi dalili ya Daraja za dini

Dalili ni hadithi ya Jibril iliyo Mash’huri alipo kuja kwa mtume kwa umbile la Mwanadamu na kumuliza Mtume kuhusu Uislamu na Imani na Ihsaan.

عَن عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال: بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:[ الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه سَبيلاً]. قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال : فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: [أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ وشَرِّهِ] قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:[ أنْ تَعْبُدَ الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك]. قال: فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: [ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ ]. قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:[ أن تَلِدَ الأمَةُ رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ ] ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً، ثُمَّ قال : [يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟] قُلْتُ: اللهُ ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال: [ فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ

رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khatwab Radhi za Mwenyeezi Mungu ziwe juu yake ambaye amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, hapo alitokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, akaweka magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu. Mjumbe wa Allaah Rehma na amani zimfikie yeye,alisema: [Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.]

(Akasema yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu Imani. Akasema (Mtume Rehma na amani zimfikie yeye) [Ni kumwamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake (Allaah alie tukuka )]. (Akasema Jibriyl): Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsaan. Akasema Mtume Rehma na amani zimfikie yeye, [Ni kumuabudu Allaah Sub’hanahu wata’aala kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona.] Akasema (Jibriyl): Niambie kuhusu Qiyaama. Akajibu (Mtume Rehma na amani zimfikie yeye) : [Hakuwa mwenye kulizwa ni mjuzi kuliko alie uliza]. Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu (Mtume Rehma na amani): [Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga mbuzi miguu chini, wenda uchi mafukara wakishindana kujenga majumba ya fahari.] Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo. Kisha akasema Mtume Rehma na amani [Ewe ‘Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? ] Nikasema: Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi. Akasema Mtume Rehma na amani [Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.]

[Imepokewa na Imam Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.