0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

FADHLA YA KUMSWALIA MTUME ﷺ

FADHLA YA KUMSWALIA MTUME

Anasema Mwenyezi Mungu alietukuka katika kitabu chake kitukufu:

{إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا}

[Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu]     [Suratul Ahzab aya ya 56.]

Makusudio ya aya hii tukufu kwamba Mwenyezi Mungu alietukuka amewaeleza waja wake utukufu wa mja wake na Mtume Muhammad wake ﷺ kwake yeye huko mbinguni, yakwamba yeye Mwenyezi Mungu anamsifia Mtume kwa Malaika wake walio karibu nae, na yakwamba Malaika wanamswalia yeye Mtume, kisha Mwenyezi Mungu akawaamrisha waja wake walio Ardhini kumswalia na kumatakia salamu Mtume ili akusanye sifa kwao kwa watu wote walio mbinguni na walio Ardhini. kama alivyosema Ibn kathir (Allah amrehemu.)

Na makusudio ya kumswalia Mtume ﷺ ni kumuombea dua kwa njia maalum na kulitukuza jambo lake Mtume ﷺ .

Wanasema wanazuoni: Swala ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume ni rehema yake na radhi zake, na kumsifia kwake kwa Malaika, na swala ya Malaika ni dua kwa Mtume na kumuombea msamaha, na swala ya Waislamu kwa Mtume ni dua kwake na kumuombea msamaha na kutukuza jambo lake.

Na fadhla ya kumswalia Mtume ﷺ ni kubwa asema Mtume ﷺ:

أتاني جبريل فقال: يا محمد أما يرضيك أن ربك عز وجل يقول: إنه لا يصلي عليك من أمتك أحد صلاةً إلا صليت عليه بها عشراً، ولا يسلم عليك أحد من أمتك تسليمة إلا سلمت عليه عشراً؟ فقلت: بلى، أي ربي

[Alinijia Jibril akasema: Ewe Muhammad haikuridhishi wewe yakwamba mola wako alietukuka anasema: Hakika hakuswalii wewe yeyote katika umma wako swala moja isipokua namswalia yeye mara kumi , na hakutakii salamu yeyote katika umma wako salamu moja isipokua nitamtakia salamu mara kumi ? Nikasema : ndio mola wangu].

Hadithi hii ni sahihi ameipokea imam Ahmad na wengineo.

Anasema Swahaba: aliamka Mtume Muhammad ﷺ siku moja nafsi yake ikiwa safi inaonekana katika uso wake furaha, wakasema ewe Mtume wa Mungu umeamka leo nafsi yako ikiwa safi na uso wako una furaha ? Akasema:

أجل، أتاني آت من ربي فقال: من صلى عليك من أمتك صلاة كتب الله له بها عشر حسنات، ومحا عنه عشر سيئات، ورفع له عشر درجات، ورد عليه مثلها      وراه أحمد

[Ndio amenijia mwenye kuja kutoka kwa mola wangu akasema : atakaekuswalia katika umma wako swala moja Mwenyezi Mugnu atamuandikia kwa swala ile thawabu kumi , na atamfutia madhambi kumi , na atamnyanyua daraja kumi na atmrudishia mfano wake]

[Impokewa na Ahmad]

Na hadithi hii ina njia nyingi ambazo zinaifanya hadithi hii iwe na nguvu.

Na imekuja katika baadhi ya mapokezi ya kwamba Mtume  ﷺ alisujudu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu alipoletewa wahyi kuhusu hilo:

[وما من عبد يصلي عليَّ إلا صلت عليه الملائكة ما دام يصلي عليَّ فليقلَّ العبد من ذلك أو يكثر]     رواه الطبراني

[Na hakuna mja atakaeniswalia mimi isipokua nae Malaika watamswalia maadamu ananiswalia basi mja afanye hilo kwa uchache au afanye kwa uwingi]    [Imepokewa na At Twabraniy] 

Na imepokelewa kutoka kwa  Ibnu Mas’uud radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume ﷺ amesema :

[إن لله تعالى ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام]     رواه النسائي

[Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika wanaotembea katika Ardhi wananifikishia mimi kutoka kwa umma wangu salamu]     [Imepokewa na Annasai]

Na imepokelewa kutoka kwa Ammar bin yasir radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume amesema:

[إن لله تعالى ملك أعطاه سمع العباد فليس من أحد يصلي عليَّ إلا أبلغنيها، وإني سألت ربي أن لا يصلي عليَّ عبد صلاة إلا صلى عليه عشر أمثالها ]     رواه الطبراني

[Hakika Mwenyezi Mungu ana Malaika amempa maskizi ya waja basi hakuna yeyote atakaeniswalia mimi isipokua aninifikishia, na hakika yangu mimi nimemuomba mola wangu yakwamba haniswalii mimi mja Swala moja isipokua yeye atamswalia mara kumi mfano wake].    [Imepokewa na At Twabraniy]

Hivyo basi dua ya Mtume ﷺ kwa ajili yetu imejibiwa, kwa hivyo kila anaemswalia Mtume Muhammad ﷺ Swala yake inamfikia Mtume wetu kupitia Malaika maalum,
Na nyongeza ya hilo Mwenyezi Mungu anamswalia mfano wake mara kumi asema Mtume ﷺ:

[أكثروا الصلاة علي فإن الله وكل بي ملكاً عند قبري فإذا صلى علي رجل من أمتي قال لي ذلك الملك: يا محمد إن فلان ابن فلان صلى عليك الساعة]    رواه الديلمي

[Fanyeni wingi kuniswalia mimi kwani Mwenyezi Mungu ameniwakilishia malaika kwenye kaburi langu basi akiniswalia mtu katika Umma wangu yule malaika huniambia: Ewe Muhammada hakika fulani mtoto wa fulani amekuswalia katika mda huu]    [Imepokewa na Ad Daylamiy na Hadithi Hasan] .

Na katika Hadithy nyingine Mtume ﷺ anasema:

[ما من أحد يسلم عليَّ إلا رد الله عليَّ روحي حتى أرد عليه السلام]    رواه أبودود وهو حديث حسن

[Hakuna yeyote atanisalimia mimi isipokua Mwenyezi Mungu ananirudishia roho yangu mpaka nimjibu salamu yake]     [Imepokelewa na Abu Daawud nayo ni hadithi mzuri.]

Na Amesema tena Mtume ﷺ:

[حيثما كنتم فصلوا عليَّ فإن صلاتكم تبلغني]     رواه أبوداود

[Popote mtakapokua niswalieni mimi kwa hakika swala zenu zinanifikia]     [Imepokewa na Abuu Dawud].

Mtume ﷺ na ameondoka katika ulimwengu huu, na muumini anataka kiunganishi na Mtume wake ﷺ basi Mwenyezi Mungu akatufanyia njia hii ya moja kwa moja, basi tunapomswalia Mtume wetu ﷺ anafikishiwa kwa jina yakwamba fulani amemswalia , kisha na yeye pia anatujibu salamu.

Makala haya yameandikwa na

Sheikh Muhammad Swaleh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.