FADHILA ZA KUFUNGA SIKU YA ASHURAA
Kwanza: Kufunga siku ya Ashuraa inafuta madhambi ya mwaka uliyopita kwa kauli ya Mtume Muhammad ﷺ :
[صِيَامُ يَوْمِ عَرَفَةَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ وَالسَّنَةَ الَّتِي بَعْدَهُ وَصِيَامُ يَوْمِ عَاشُورَاءَ أَحْتَسِبُ عَلَى اللَّهِ أَنْ يُكَفِّرَ السَّنَةَ الَّتِي قَبْلَهُ] رواه مسلم
[Funga au Saum ya siku ya Arafah natarajia kwa Mweyezi Mungu intafuta madhambi ya mwaka uliyopita na mwaka unaokuja na funga siku ya Ashuraa natarajia kwa Mwenyezi Mungu itafuta madhambi ya mwaka uliyopita] [Imepokelewana Muslim.]
Na alikua Mtume ﷺ anachunga kuifunga siku ya Ashuraa kutokana na cheo kinachopatikana katika siku hiyo, kwani imepokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas Radhi za ALLAH ziwe juu yake na baba yake Amesema:
[مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَحَرَّى صِيَامَ يَوْمٍ فَضَّلَهُ عَلَى غَيْرِهِ إِلا هَذَا الْيَوْمَ يَوْمَ عَاشُورَاءَ وَهَذَا الشَّهْرَ يَعْنِي شَهْرَ رَمَضَانَ ] رواه البخاري
[Sijamuona mtume rehma na amani ziwe juu yake anachunga kufunga siku ambayo amaeifadhilisha kuliko masiku mengine isipokua siku hii siku ya Ashuraa na mwezi huu yaani mwezi wa Ramadhan.] [Imepokelewa na Imam Bukhary.]
Pili : Ama sababu ya kufunga Mtume Muhammad ﷺ siku ya Ashuraa na kuwahimiza watu kufunga siku hiyo ni kwa aliyoyapokea Bukhary kutoka kwa Ibnu Abbas Radhi za ALLAH ziwe juu yao Amesema:
قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ فَرَأَى الْيَهُودَ تَصُومُ يَوْمَ عَاشُورَاءَ فَقَالَ مَا هَذَا ؟ قَالُوا : هَذَا يَوْمٌ صَالِحٌ ، هَذَا يَوْمٌ نَجَّى اللَّهُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنْ عَدُوِّهِمْ فَصَامَهُ مُوسَى، قَالَ فَأَنَا أَحَقُّ بِمُوسَى مِنْكُمْ فَصَامَهُ وَأَمَرَ بِصِيَامِهِ
[Mtume alikuja katika mji wa Madina basi akawakuta mayahudi wanafunga siku ya Ashuraa akasema hii ni nini ? Wakasema : hii ni siku nzuri , hii ni siku ambayo Mwenyezi Mungu aliyowaokoa wana waisraeli kutokana na adui yao, basi Musa akaifunga siku hiyo, Mtume akasema mimi nina haki na Musa kuliko nyinyi basi akaifunga siku hii na akaamrisha kuifunga siku hii”]
Tatu: Kufutwa kwa madhambi kunakopatikana kwa kufunga siku ya Ashuraa maana yake ni madhambi madogo, Ama madhambi makubwa basi yanahitaji toba maalum.
Amesema Sheikhul Islam Ibnu Taymiyah ALLAH amrehemu: Na kafara au kufutwa kwa madhambi kwa sababu ya Twahara, na Swala, na kufunga Ramadhan , na Arafah , na Ashuraa ni kwa ajili ya madhambi madogo tu.