0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYOTIA MSUKUMO WA SUBIRA NA UVUMILIVU


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Walisimama watu wenye busara hali ya kuwa wametosheka na wenye akili miongoni mwao, wakijiuliza, ‘Waislamu walitumia mbinu gani zilizowawezesha kufika kwenye upeo huu, lengo hili na hali hii yenye kuelemea katika kuidhibiti nafsi kuliko kukubwa? Ni kwa vipi waliweza kuvumilia mateso makubwa ya kimwili ambayo yanasabibisha nyoyo kushikwa na hofu kuu kwa kuyasikia tu?.

Kwa kuliangalia hili ambalo linazishughulisha nyoyo, tunaona tuanze kupitia zile sababu zilizopelekea hali hii:

1. Sababu ya msingi katika hili inayoweza kutajwa mwanzo kwa kuiainisha, imejengwa katika Kumwamini Mwenyezi Mungu (ﷻ) Peke Yake na Kumwelekea kwa ukweli. Inaaminika kuwa Imani iliyo na yakini ikichanganyika na kusadikishwa kwa moyo, uzito wake huwa sawa na jabali lisiloyumba. Mwenye kuwa na Imani iliyo madhubuti na yakini huziona taabu za kidunia, kwa vyovyote zitakavyo kuwa, ni kitu kidogo, huwa ni sawa na mwani wenye kuelea katika mafuriko yenye nguvu, ambayo yamekuja ili yavivunje vizuizi ambavyo ni madhubuti na ngome ambazo ni imaré. Kwa hivyo, hatojali jambo lolote katika taabu hizo, zaidi ya yale anayoyapata miongoni mwa utamu wa Imani, na ubora wa kufuata kwake, na bashasha ya yakini yake:

فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذۡهَبُ جُفَآءٗۖ وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمۡكُثُ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ

[..Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi….] (13 :17) Kutokana na msingi huu pekee ndiyo sababu nyingine zinazoupa nguvu uthibitifu huu na ukubwa wa subira hujitokeza.

2. Uongozi unaovuta nyoyo, Mtume () alikuwa ndiyo kiongozi wa juu wa umma wa Kiislamu, si hivyo tu alikuwa pia ni kiongozi wa wanadamu wote. Alikuwa amepambwa na uzuri wa tabia, ukamilifu wa nafsi na ubora wake na alikuwa na sifa zote zilizo tukufu, mambo ambayo huvuta nyoyo na ambayo hakupata kupewa mtu yeyote mfano wake. Alikuwa juu ya kilele cha utukufu, ubora, kheri, wema na wakati wote alijiepusha na maovu ya aina zote. Alijipamba na uaminifu na ukweli katika hali zote na njia zote za kheri kwa namna ambayo hakuna aliyemtilia shaka katika sifa miongoni mwa maadui zake, sembuse wapenzi wake na marafiki zake. Alikuwa hatamki chochote isipokuwa wote waliolisikia huwa na uhakika wa ukweli wake.

Walikutanika watu watatu miongoni mwa Makureishi na kila mmoja wao alikuwa ameisikiliza Qur’an”kwa njia ya siri akiwa mbali na mwenzake, kisha ikafichuka siri yao. Mmoja miongoni mwa wale watu watatu akamwuliza Abu Jahli: ”Nini maoni yako kuhusu yale ambayo umeyasikia kutoka kwa Muhammad? Akahoji: ’Nimesikia nini? Tumegombana sisi na Banu Abdi Manafi, kama ni utukufu wao, tulikuwa tunalisha nao wakilisha, wameshambulia na sisi tumeshambulia na kama wao wametoa na sisi tumetoa mpaka tulipokuwa sawa sawa juu ya vipandwa na tukawa kama farasi wawili wa mashindano.” Wakasemar ‘Sisi tuna Mtume ambaye unamjia wahyi kutoka mbinguni’; ’Sasa ni lini sisi tutalipata hilo? Nininaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hatutamwamini milele na hatutomsadikisha.’

Abu Jahli alikuwa anasema, ”Ewe Muhammad hakika hatukukadhibishi isipokuwa tunayakadhibisha yale ambayo umekuja nayo”; Mwenyezi Mungu () Akateremsha aya lsemayo;

فَإِنَّهُمۡ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَٰكِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ يَجۡحَدُونَ

[…Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.] (6:33) (1)

Ipo siku moja makafiri walimtia aibu mara tatu, katika mara ya tatu akawaeleza, ”Enyi Makuraishi nimewajieni na jumbo tukufu”, neno lile likawaingia kiasi cha kuwa yule aliyekuwa ni adui yake mkubwa akawa anamtendea vizuri.

Wakati walipomtupia matumbo ya ngamia na hali ya kuwa amesujudu, aliwaapiza. Kwa sababu ya kuapizwa wakaondokewa na furaha, wakapatwa na kero na kukosa raha, wakawa na uhakika kuwa wao ni watu wenye kuangamia. Alimwapiz? ’Utba bin Abu Lahb, na kwa kuapizwa alikuwa na uhakika na kupatwa na lile ambalo ameapizwa. Wakati alipomwona simba, alisema, ”Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Muhammad ameniua, na hali ya kuwa yeye yuko Makka.”

Ubayy bin Khalaf alikuwa anakamia kumwua Mtume (). Naye Mtume () alimwambia; “Bali mimi ndiye nitakayekuuwa apendapo Mwenyezi Mungu.” Ubayy alipochomwa shingoni mwake wakati wa vita vya Uhud na kupata mparuzo mdogo tu. Akawaakilalamika kwa kusema: ’Hakika yeye alikuwa ameniambia huko Makka kuwa, kwa hakika mimi ndiye nitakaye kuua na lau angenitemea mate basi anganiua (2) Wakati Sa’ad bin Muadh akiwa Makka alipata kumwambia Ubayy bin Khalaf, ’Kwa hakika nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ()’ akisema kuwa wao (Waislamu) watakuua.” Akapata mfadhaiko mkubwa sana na akaahidi kuwa hatatoka Makka. Wakati Abu Jahli alipomlazimisha kutoka katika siku ya Badri alinunua ngamia mwenye mbio sana, ili amuwezeshe kukimbia. Mke wake alimwambia, “Ewe Abu Sufyan hivi umeyasahau yale ambayo alikwambia ndugu yako wa Yathrib (Madina)? Akajibu, ”Hapana, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu sitaki kuvuka pamoja nao isipokuwa mahali palipo karibu” (3)

Hivi ndivyo ilivyokuwa hali ya maadui zake Mtume ().

Ama kuhusu masahaba na marafiki wake alichukua kwao mahali pa roho na nafsi zao, na akakaa kwao mahali badili ya moyo na macho yao. Mapenzi ya kweli yakawa yanamiminika kwake kama maporomoko, na nyoyo za watu zilivutika kwake mfano wa chuma kwenye sumaku. Athari ya mapenzi yao kwake ilifikia kiwango cha wao kuridhia miili yao ifanywe vyovyote vile.

Siku moja Abubakar bin Abu Kuhafa (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikanyagwa na alipigwa kipigo kikubwa sana katika mji wa Makka. Miongoni mwa watu waliomshambulia alikuwemo ’Utba bin Rabia aliyekuwa akimpiga kwa ndara zake mbili, zilizokuwa zimebandanishwa, kwa kuzielekeza usoni kwake. Alipanda juu ya tumbo la Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) mpaka ikawa mtu hawezi kutofautisha uso wake na pua yake kwa kipigo alichokuwa anampa. Bin Taym walimbeba Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika nguo na kumpeleka mpaka nyumbani kwake, wakiwa hawana shaka kuwa amekwisha kufa.

Baadae Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alizungumza kwa kuuliza: “Kumemtokea nini Mtume wa Mwenyezi Mungu (), wakachukizwa na swali lake na wakamlaumu. Kisha wakasimama na wakamwambia mama yake Ummu Al-Khair, ”Angalia Usimlishe au kumnywesha kitu chochote”, alipokaa naye faragha alimwuliza, ”Amefanywa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu ()?. Akasema: ”Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (ﷻ) sijui jambo lolote kuhusu rafiki yako.” Akamuagiza, ”Nenda kwa Ummu Jamil, binti Al-Khattab umwulize kuhusu Mtume ).” Akatoka na kwenda kwa Ummu Jamil na kumueleza, ”Kwa hakika nimetumwa na Abubakar, anakuuliza kuhusu Muhammad bin Abdillah.” Akasema, “Simjui Abubakar wala Muhammad bin Abdillah, na iwapo unapenda niende pamoja na wewe kwa mtoto wako nitakwenda.” Akajibiwa, “Ndiyo.” Wakaondoka pamoja na wakamkuta Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika hali ya ugonjwa, Ummu Jamil akasema kwa kupiga kelele, “Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika watu ambao wamekufanyia hivi ni watu waovu na makafiri, na ninataraji kuwa Mwenyezi Mungu (ﷻ) Atawaadhibu kutokana na vitendo vyao viovu.” Akauliza tena, ”Amefanywa nini Mtume wa Mwenyezi Mungu ()?. Akajibiwa, ”Huyu hapa mama yako anasikia.” Hapo akaelezwa hakuna jambo alilosema juu yako, akaelezwa kuwa Mtume yuko salama na mwenye hali nzuri. Akauliza, ”Yuko wapi?.” Akajibiwa, katika nyumba ya Ibn al-Arqam.’ Akasema; ”Kwa, hakika Mwenyezi Mungu ni shahidi yangu, sitokula chakula wala kunywa kinywaji chochote mpaka nikamwone Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ).” Wakampa muda akapumzika mpaka alipotulia na watu nao wakatulia na kutoka naye akiwa anawaegemea mpaka walipomfikisha nymnbani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (). (4)

3. Hisia za kuhusika na majukumu, masahaba walikuwa na hisia kamili ya yale ambayo yalikuwa chini ya usimamizi wao, miongoni mwa majukumu mapevu na makubwa sana, na kuwa haikuwezekana kuyakwepa na kuwa mbali nayo kwa hali yoyote ile. Kwani mwisho wa kukwepa au kuyakimbia majukumu hayo kwa vyovyote vile ungekuwa ni mbaya na wenye madhara makubwa kwa jamii, kuliko yale yaliyokuwa yakiwasibu kwa kukandamjzwa na kuteswa kwa kupokea na kuikubali Imani mpya. Walikwishabaini hasara ambayo wangeipata na ambayo ingewapata wanaadamu wote baada ya wao kuyakimbia majukumu. Haiwezi kulinganishwa kwa hali yoyote na mashaka ambayo walikuwa wanakabiliana nayo ikiwa ni matokeo ya uvumilivu wao.

4. Kuiamini akhera, imani hii ni miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakiwapa nguvu Waislamu na kuwajengea hisia ya kuwa na yakini kuwa majukumu yao mbalimbali yalikuwa ni katika kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu (ﷻ), Mola wa viumbe vyote, Aliye na khabari ya matendo yote ya wanaadamu, madogo na makubwa. Jambo lililowatia hamasa kwa kujua kuwa baada ya uhai huu wa duniani, mtu ataelekea kwenye neema za kudumu, au kwenye adhabu za milele motoni kufuatana na jinsi yeye mwenyewe alivyotii, au kutotii na kutekeleza amri za Muumba (ﷻ). Kwa yakini hii, Masahaba walikuwa wakiyapitisha maisha yao kwa kuogopa na kutarajia Rehema za Mola Wao, wakiogopa Adhabu Zake, na walikuwa,

 يُؤۡتُونَ مَآ ءَاتَواْ وَّقُلُوبُهُمۡ وَجِلَةٌ أَنَّهُمۡ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ رَٰجِعُونَ

[Wanakitoa kile ambacho wanakitoa huku nyoyo zao zikiwa na khofu kuwa wao kwa Mala wao watarudi.”] Walikuwa wanaelewa kuwa dunia pamoja na shida zake na neema zake, hailingani na akhera hata kwa kiasi cha ubawa wa mbu, imani na maarifa haya yenye nguvu yaliwarahisishia Masahaba mambo na kuwawezesha kukabiliana na matatizo ya dunia, mashaka na machungu yake, mpaka wakafikia kiwango cha kutoijali dunia na kutoipa umuhimu wowote.

1. Qur’an:- Wakati huu mgumu na wa kutisha katika historia ya Uislamu zilikuwa zikishushwa aya, zilizosimamisha hoja na ushahidi juu ya misingi ya Uislamu. Mafundisho yote ya Kiislamu yalikuwa yakizunguka katika misingi hiyo. Aya hizo zilikuwa zikishuka kwa uzuri na utaratibu wenye nguvu na wenye kuvutia, na zilikuwa zinawaongoza Waislamu kwenye misingi ambayo Mwenyezi Mungu (ﷻ) Ameikadiria kujengeka juu yake jamii ya wanaadamu iliyo bora ulimwenguni nayo ni jamii ya Kiislamu – na kuamsha hisia za Waislamu na hamasa zao katika hili jambo la kusubiri na ukakamavu, inawapigia kwa hilo mifano, na inawawekea wazi yaliyo ndani yake miongoni mwa mambo ya hekima.

أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُمۖ مَّسَّتۡهُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ

[Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.] (2:214)

الٓمٓ (1) أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن يُتۡرَكُوٓاْ أَن يَقُولُوٓاْ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا يُفۡتَنُونَ (2) وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَيَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَلَيَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَٰذِبِينَ (3)

[”Alif Lam Mym. Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo.]  (29:1, 2, 3)

Kama ambavyo Aya zilivyokuwa zikijibu hoja za makafiri na wapingaji wengine majibu yaliyowanyamazisha na kuwakosesha hoja kabisa. Kisha kuwatahadharisha na adhabu iwapo wanaendelea na upingaji na upotevu wao, na hilo ni katika malipo ya matendo maovu, huku ukitolewa ushahidi wa matukio ya adhabu za Mwenyezi Mungu (ﷻ) kwa watu waliotangulia.

Ushahidi wa kihistoria ambao unafahamisha juu ya utaratibu wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) kwa wale walio na Radhi Zake na kwa wale wanaopinga Amri Zake. Mara zote aya zilizoshushwa zilikuwa zikielezea maudhui kwa upole na kutekeleza haki ya kufahamisha na kuongoza na kuelekeza, ili watu waache yale mambo ya upotevu ulio wazi.

Qur’an ilikuwa inawaongoza katika ulimwengu mwingine, na ilikuwa ikiwatajia miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakishuhudiwa ya ulimwengu, uzuri wa Mola wa viumbe na Ukamililfu wa Uungu Wake, na alama za Rehema na Upole na kwa Radhi Zake. Mambo haya yaliwatia shauku kubwa Masahaba na hawakukubali jambo lolote lisimame na kuwakwaza mbele yao.

Ndani ya aya hizi kulikuwemo pia maagizo kwa Waislamu na kubashiriwa kwa rehema, radhi na pepo kutoka kwa Mola wa viumbe, vitu ambavyo vinatajwa kuwa ni neema zenye kudumu. Aya za Qur’an zilikuwa pia zinawapa wao sura za maadui zao miongoni mwa makafiri waliovuka mipaka, na ikasemwa kuwa madhalimu watahukumiwa na watazuiliwa kisha watakokotwa na kutupwa motoni – huku wakiambiwa – onjeni adhabu za moto.

Bishara za Mafanikio: –

Pamoja na yote hayo, tokea siku ya kwanza walipokutana Waislamu walikuwa wakielewa kuwa watakumbana na matafizo ya kukandamizwa na kuteswa. Hata kabla ya hapo walikuwa wanajua pia kuwa kuingia katika Uislamu maana yake ni kujitafutia misiba na vifo. Tokea siku yake ya kwanza Da’wa ililenga kwenye kuumaliza ujinga uliopea, kutoa mafunzo ya msingi ya Uislamu na kueleza kuwa malengo yake ya msingi ni kutawala na kuongoza ulimwengu. Ili wito wake uuongoze umma wa Watu na Jummya ya wanaadamu kwenye matendo yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (ﷻ) na uwatoe katika tabia ya kuwaabudu watu na kuwaelekeza kwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu (ﷻ ) Peke Yake.

Qur’an ilikuwa ikishushwa pamoja na bishara hizi, wakati mwingine kwa njia za uwazi na wakati mwingine kwa njia ya mafumbo. Katika hivyo vipindi vigumu ambavyo dunia ilifanywa finyu kwa Waislamu na kukaribia kuwanyonga na kuyamaliza maisha yao, Aya zilikuwa zikishushwa na maelezo ya yale ambayo yaliwatokea Mitume waliotangulia na watu wao ambao walisimama kwa kuwakadhibisha na kuwapinga. Aya za Qur’an zilikuwa zinakusanya mambo na kutaja hali ambazo zilikuwa zinakubaliana na halii za Waislamu wa Makka na makafiri, na kisha Aya kutaja yale ambayo yaliwapata watu wengine miongoni mwa watu waliotangulia, kuangamizwa kwa makafiri na madhalimu wengine na kurithishwa na kutoshelezwa kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu (ﷻ) katika ardhi na miji mbalimbali.

Kafika visa hivi zilikuwemo ishara za wazi kuwa hata wao wa Makka’ wangeshindwa tu huko mbele na Waislamu watafaulu pamoja na kufaulu kwa mafunzzw ya Uislamu.

Katika vipindi hivi zilishuka aya zilizoweka wazi utabiri wa kushinda kwa Waislamu, kama tunavyosoma maneno ya Mwenyezi Mungu Aliye Mlukufu;

وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ (171) إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ (172) وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ (173) فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ (174) وَأَبۡصِرۡهُمۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ (175) أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ (176) فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمۡ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلۡمُنذَرِينَ (177)

[ Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.Basi waachilie mbali kwa mda.Na watazame, nao wataona.Je! Wanaihimiza adhabu yetu?Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.] (37: 171 – 177)

Na Amesema,

سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ

[ Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.] (54:45)

Na Amesema,

جُندٞ مَّا هُنَالِكَ مَهۡزُومٞ مِّنَ ٱلۡأَحۡزَابِ

[Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.] (38:11)

Na zilishuka aya kuhusu wamnini waliohama kwenda uhabeshi:-

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

[Na wale walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa,bila ya shaka tutawaweka duniani kwa wema; na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti kuwa wanajua!]  (16:41)

Upo wakati makafiri wa Makka walimwuliza Mtume () kuhusu kisa cha Yusuf (Aayhi Salam) na Mwenyezi Mungu () Akateremsha aya ifuatayo:

لَّقَدۡ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخۡوَتِهِۦٓ ءَايَٰتٞ لِّلسَّآئِلِينَ

[Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanao uliza.] (12: 7)

Watu wa Makka wenye kuuliza, watayapata yale waliyoyapata ndugu zake miongoni mwa kushindwa na watajisalimisha kama walivyojisalimisha. Mwenyezi Mungu () Amesema na hali ya kuwa Anawataja Mitume :-

فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَقُلۡ أَنذَرۡتُكُمۡ صَٰعِقَةٗ مِّثۡلَ صَٰعِقَةِ عَادٖ وَثَمُودَ (13) إِذۡ جَآءَتۡهُمُ ٱلرُّسُلُ مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّا ٱللَّهَۖ قَالُواْ لَوۡ شَآءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَٰٓئِكَةٗ فَإِنَّا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ

[ Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A’di na Thamudi,Walipo wajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angeli taka Mola wetu Mlezi bila ya shaka angeli wateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyo tumwa.] ( 14:13-14)

Qur’an imetaja matukio mengi, kwa mfano wakati vita vilipokuwa vimepamba moto kati ya Wafursi na Warumi, Makafiri walikuwa wanapenda Wafursi wapate ushindi kwa sababu wao ni Mushirikina wenzao, na Waislamu walikuwa wanapenda kushinda kwa Warumi kwa kuwa wao walikuwa wakimwamini Mwenyezi Mungu (), Mitume, Wahyi, Vitabu na Siku ya Mwisho. Mwenyezi Mungu () Aliteremsha bishara nyingine kuhusu vita hiyo, nayo ni kushinda kwa Warumi katika muda ulio kati ya miaka mitatu mpaka tisa-. Mwenyezi Mungu () Hakuishia katika bishara hii tu bali Aliweka wazi na bishara nyingine ambayo ni ya kuwanusuru Waumini wakati Aliposema ;

وَيَوۡمَئِذٖ يَفۡرَحُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ (4) بِنَصۡرِ ٱللَّهِ

[ Na siku hiyo Waislamu watafurahi kwa Nusra ya Mwenyezi Mungu. (Atakayowapa wao nayo ni kuwashinda makureishi  siku hiya)] (30 :4 , 5)

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () alikuwa akisimama mwenyewe nyakati tofauti na kuwaelezea watu juu ya bishara hizi. Wakati wa musimu alikuwa akisimama kati ya watu katika masoko ya ’Ukadh, Mijan, na Dhil-Mijaz, na kufikisha ujumbe wake. Mtume () hakuwa akiwabashiria pepo tu, lakini alikuwa akiwaambia watu wote kwa uwazi kabisa,  “Enyi watu semeni, Hakuna Mala apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (ﷻ) mtafuzu na mtawamiliki kwa tamko hilo Waarabu, watawafuateni kwa tamko hilo Waajemi na wakati mtakapokufa mtakuwa wafalme peponi.” (Impokewa na Ttirmidhy)

Tumekwisha kuyatanguliza yale ambayo Mtume () alimjibu ‘Utba bin Rabia wakati alipotaka wafanye mapatano kwa kuzingatia matakwa ya kidunia na yale ambayo aliyafahamu na kayataraji ‘Utba kutokana na kudhihiri kwa mambo ya Mtume (). Vilevile yale ambayo Mtume () aliyoyajibu katika ujumbe wa mwisho uliokuja kwa Abu Twalib, kwani aliwawekea wazi kuwa yeye kutoka kwao alikuwa anataka tamko moja tu, ambalo kwa tamko hilo Waarabu wote wangeliwafuata na kwa tamko hilo hilo wangeliwamiliki Waejemi.

Khabbab bin Al Aratt (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema, ”Nilimwendea Mtume () akiwa katika kivuli cha Al-Ka’aba na hali ya kuwa shuka yake ameifanya mto, hii ilikuwa ni baada ya kupata matatizo makubwa sana kutoka kwa Mushirikina. Nikamweleza, ’Kwa nini humuombi Mwenyezi Mungu () Atuondolee adha hizi za Washirikina?.”‘ Mtume () alikaa kimya na huku uso wake umegeuka na kuwa mwekundu sana. Akajibu:

لقَدْ كانَ مَن قَبْلَكُمْ لَيُمْشَطُ بمِشَاطِ الحَدِيدِ، ما دُونَ عِظَامِهِ مِن لَحْمٍ أوْ عَصَبٍ، ما يَصْرِفُهُ ذلكَ عن دِينِهِ، ويُوضَعُ المِنْشَارُ علَى مَفْرِقِ رَأْسِهِ، فيُشَقُّ باثْنَيْنِ ما يَصْرِفُهُ ذلكَ عن دِينِهِ، ولَيُتِمَّنَّ اللَّهُ هذا الأمْرَ حتَّى يَسِيرَ الرَّاكِبُ مِن صَنْعَاءَ إلى  حَضْرَمَوْتَ، ما يَخَافُ إلَّا اللَّهَ، زَادَ بَيَانٌ: والذِّئْبَ علَى غَنَمِهِ  وفي رواية (ولكنكم تستعجلون)

”Alikuwa mmoja wenu katika umma zilizopita akichomwa mwilini mwake kwa chanuo la chuma likipita kwenye nyama hadi kwenye mifupa yake (kwa mateso) Iakini halimtoi hilo katika Dini yake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu  Atalitimiza jambo hili mpaka itafikia hatua mtu atatoka Sanaa mpaka Hadhramout hakuna anaemuogopa isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake — na mpokeaji akaongeza — na mbwa mwitu na mbuzi wake”, na katika upokezi mwengine, ”Isipokuwa nyinyi mnafanya haraka. “130

Bishara hizi hazikuwa zikitolewa kwa kificho au kwa siri, bali zikitolewa waziwazi hadharani na makafiri walikuwa wakizijua kama walivyokuwa wakizijua Waislamu. Ilifikia hatua, Al-Aswad bin A]-Muttalib na wapambe wake wanapowaona Masahaba wa Mtume (), wanakonyezana kwa kuwadhihaki na kusema wamewajieni wafalme wa ardhi, watashinda wafalme wa Kisra na Kaisar, kisha wanapiga makofi kwa kush’angilia.

Kwa bishara hizi, za wakati wa mbele ulio mtukufu wenye mwangaza katika dunia, pamoja na yaliyokuwa ndani yake miongoni mwa matarajio mema yaliyo makubwa yenye kufikia ukomo katika kufuzu kwa kupata pepo, Masahaba walikuwa wanaona kuwa mateso na manyanyaso waliyokuwa wakiyapata kutoka kila upande, na misiba iliyowazunguka kutoka pande zote haikuwa ni kitu cha kuwashitua sana. Yote hayo waliyafananisha na kiwingu cha wakati wa Kaskazi ambacho baada ya muda mfupi kingetoweka.

Mtume () hakuacha kuzilisha roho zao, kwa kuzipendesha Imani yenye kuvutia, na alikuwa akizitakasa nafsi zao kwa kuwafundisha Qur’ani na Sunna. Aliwalea malezi mazuri ya Kiislamu na alikuwa akizipeleka roho zao katika mashukio ya“ utukufu wa nafsi, usafi wa moyo, uzuri wa tabia na kujikomboa kutoka katika utawala wa vitu vya kimaada. Kupambana na matamanio ya nafsi na kuwavuta kuelekea kwa Mola wa viumbe vyote vya mbinguni na ardhini.

Mtume () alikuwa akiwatoa katika giza na kuwapeleka kwenye nuru, alikuwa akiwachukua kwa uvumilivu pamoja na maudhi yao na kusamehe kuliko kuzuri. Akawafundisha jinsi ya kuziteza nguvu nafsi na wakazidi kuzama katika Dini na kujitenga mbali na matamanio na badala yake kujihimiza katika mambo yanayoridhiwa na Mwenyezi Mungu (). Akawafanya kuwa na shauku ya kuingia peponi na kuwa na pupa katika kutafuta elimu, kuielewa Dini, kuidhibiti nafsi, kuvishinda vishawishi mbalimbali, kuzishinda hisia za ulipaji kisasi na kuwa wenye kusubiri, utulivu na heshima.


1) Ttirmidhy, Iuzuu 2, Uk. 132. 211.
2) Ibn Hisham, juzuu 2, Uk. 84. 21.
3) Sahillil Buklznri, Juzuu 2, Uk. 563.
4) Bidaya wa Nihaya, Juzuu 3, Uk. 30. – .
*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk 209-224

Begin typing your search above and press return to search.