SOMO LA FIQHI
Hukumu ya kuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ
Kuuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ si miongoni mwa masharti ya Hija wala nguzo zake wala wajibu zake. Hilo ni sunna, na inafaa ifanywe wakati wowote.
Na ni wajibu liwe lengo la ziara ni kuswali kwenye huo Msikiti na sio kaburi. Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa akisema kumpokea Mtume ﷺ kuwa alisema:
[لَا تُشَدُّ الرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلَاثَةِ مَسَاجِد: الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ، وَمَسْجِدِ الرَّسُولِ ﷺ ، وَالمَسْجِدِ الأَقْصَى] رواه مسلم
[Hakufungwi safari isipokuwa kwenda kwenye misikiti mitatu: Msikiti wa Haram, Msikiti wa Mtume ﷺ na Msikiti wa Aqswa] [Imepokewa na Muslim.].
Amesema Shekhe wa Uislamu Ibnu Taimiyya: “Iwapo lengo lake la safari ni kuzuru kaburi ya Mtume ﷺ na sio kuswali kwenye Msikiti wake…. Basi msimamo wa maimamu na wengi wa wanavyuoni ni kuwa hili halikuwekwa na Sheria wala halikuamrishwa…Na Hadithi kuhusu kuzuru kaburi ya Mtume ﷺ zote ni dhaifu kwa itifaki ya wajuzi wa Hadithi, bali ni Hadithi zilizobuniwa. Hakuna yoyote miongoni mwa wakusanyaji wa Vitabu vya Sunna za Mtume ﷺ aliyepokea Hadithi hizo, na hakuna yoyote aliyesimamisha hoja kutegemea hadithi yoyote katika hizo” [Majmuu’ al- Fataawaa, juzu. ii, uk. 26].