KINGA YA MUISLAMU
” قال صلى الله عليه وسلم ” من صلى علي صلاة صلى الله عليه بها عشراً
أخرجه مسلم 1/288
Amesema Mtume ﷺ [Yoyote atakaeniswalia mimi mara moja basi Mwenyezi Mungu atamswalia mara kumi.] [Imepokewa na Bukhari.]
[ وقال صلى الله عليه وسلم : [ لا تجعلوا قبري عيداً وصلوا علي ؛ فإن صلاتكم تبلغني حيث كنتم
أبو داود 2/218 وأحمد 2/367 وصححه الألباني
Na amesema Mtume ﷺ: [Musilifanye kaburi langu kuwa ni Idi (mahali pa kufanya ibada inayorejewa ) na niswalieni kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mulipo.] [Imepokewa na Abuu Daud na Ahmad na kusahihishwa na Al-Baaniy.]
[ وقال صلى الله عليه وسلم : [ البخيل من ذكرت عندهُ فلم يصل علي
الترمذي 5/551 وغيره
Pia amesema Mtume ﷺ [Bakhili ni yule ambaye nikitajwa haniswalii.] [Imepokewa na Al-Ttirmidhiy.]
[ وقال صلى الله عليه وسلم [ إن لله ملائكة سياحين في الأرض يبلغوني من أمتي السلام
النسائي ،والحاكم 2/421 وصححه الألباني
Na amesema Mtume ﷺ: [Hakika Mwenyezi Mungu ana malaika wanamzunguka katika ardhi, wananiletea salamu kutoka kwa ummah wangu.] [Imepokewa na Al-Nnasaai na Al-Haakim na kusahihishwa na Al-Baaniy.]
[ وقال صلى الله عليه وسلم [ ما من أحد يسلم علي إلا رد الله على روحي حتى أروُدَّ عليه السلام
أبو داود برقم 2041
Na pia akasema Mtume ﷺ: [Hakuna mtu yoyote anaeniswalia ila Mwenyezi Mungu hunirudisha roho yangu ili nimrudishie salamu.] [Imepokewa na Abuu Daud.]
SIKILIZA DUA HII