ELIMU YA MIRATHI
Ni msingi unaojulikana katika kutimiza haki ya kila mwenye kustahiki kurithi, kulingana na mafunzo na maadili ya kiislamu.
HEKIMA ILIYOTUMIKA KATIKA MIRATHI
Mwenyezi Mungu amejaalia mirathi kuwa ni nidhamu iliyonyooka na kuwa ni kanuni iliyo na hekima na hupatikaniwa ndani yake Rehma na uadilifu.
Hekima iliyotumika katika elimu ya mirathi
Mwenyezi Mungu amefanya ugavi wa mirathi ni nidhamu iliyonyooka na sharia iliyo na hekima ndani hake, hupatikaniwa ndani yake Rehma na Uadilifu.miongoni mwayo:
a) Uislamu umejaalia mirathi ni kwa pote maalum la watu ili kuondosha mizozo ,ugomvi na fitna kwa jamii ,wasidai mirathi wasio husika.
b) Mwenyezi Mungu amejaaliwa mirathi ni moja kati ya sababu za kumiliki.
c) Imekuwa kiwango cha mwanamke kuwa ni nusu ya kiwango anacho rithi mwanamume kwa sababu mwanamume ndiye mwenye majukumu mengi kuliko mwanamke ,mfano wa majukumu ulipaji wa mahari,matumizi ya nyumba na utazamaji wa wazee .
Mbali na hayo tukiregea katika sharia za kiislamu tunapata mirathi ya mwanamke na mwanamume yapo kati hali thalathini na nne (34).
– Mwanamume hurithi sawa na mwanamke katika hali kumi (10).
– Mwanamke hurithi Zaidi ya mwanamume katika hali kumi (10).
– Mwanamke humzuia mwanamume kurithi katika hali kumi (10).
– Mwanamume hurithi Zaidi ya mwanamke katika hali nne (4).
d) Uislamu umempa kila mmoja kiwango maalum cha mirathi ili kuepuka ugomvi na ukatano wa kizazi.
e) Mke wa marehemu anapewa kiwango maalum cha mirathi ni kuukirimu ushirikiano wa kindoa uliokuwepo .
HAKI AMBAZO ZINAAMBATANA NA MALI YA MAREHEMU.
1. Kukafiniwa (kununua sanda), kuchimbiwa kaburi na mambo ambayo yanahusika na maiti (katika
mazishi).
2. Kulipa deni adaiwalo.
3. Kutekeleza wasia ambao ameacha, na usizidi wasia huo thuluthi moja ya mali.
4. Kugawanywa mali kwa wale wanaostahiki kurithi.
** Asili ya Mada hii ni kitabu Uadilifu wa Mirathi ndani ya Uislamu kilicho andikwa na Manswab Mahsen Abdulrahman Al-Ridai Al Jufry