AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Mushirikina walipowaona Masahaba wa Mjumbe’ wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) wamejiandaa na wametoka, wamebeba mali na wamewaongoza watoto kuelekea kwa Al- Awsi na Al-Khazraji (Madina), mambo hayo yaliwakera na kuwahuzunisha. Jémbo hilo liliwaathiri kwa sura ambayo haijawahi kutokea mfano wake. Ilijengeka mbele yao hatari ya uhakika iliyo kubwa ambayo ilikuwa inaugawa mfumo mzima wa utawala na wa uchumi wao wa kipagani.
Kwani walikuwa wanayaelewa yaliyo katika uwezo wa Mtume Muhammad (ﷺ), miongoni mwa upeo wa nguvu za kuathiri pamoja na ukamilifu wa mbinu za uongozi. Walikuwa wanajua pia yaliyo kwa Masahaba zake katika azma, unyofu na utayari wao wa kujitoa muhanga kwa sababu yake na kwa sababu ya Dini yao. Pia walikuwa wakiyajua yaliyo kwa makabila ya Ausi na Khazraji katika nguvu na umadhubuti, mbali na uwezo wao wa kiakili, na yaliyo kwa wenye akili katika makabila mawili hayo katika dhamira na hisia za amani na wema na kuitana katika kuacha uhasama na chuki kati yao, baada ya kuonja machungu ya Vita vya wenyewe kwa wenyeweu kwa kipindi cha miaka mingi.
Mji wa Madina upo katika eneo lenye umuhimu mkubwa kwa kuwa kwenye njia ya kibiashara inayopita ufukweni mwa Bahari Nyekundu, kutoka Yemeni kwenda Sham. Watu wa Makka walikuwa wanafanya biashara kwa kwenda Sham kwa kiasi cha mtaji wa robo millioni ya Dinari za dhahabu kwa mwaka, mbali na zile ambazo walikuwa nazo watu wa Twaif na miji mingine. Ni jambo lenye kueleweka kuwa ustawi wa biashara hii ulitegemea sana utulivu na usalama katika njia hiyo. Hayakuweza kufichika yale waliyohofia Makuraishi miongoni mwa hatari kubwa kwa kuimarika kwa wito wa Kiislamu katika Yathrib, pamoja na hofu ya mapambano ya watu wake dhidi yao.
Mushirikina walihisi ‘ukubwa wa hatari iliyokuwa inatishia kuwepo kwao, wakawa wanatafuta njia muafaka ili kuiondoa hatari hii ambayo chimbuko lake lilikuwa ni huyu mchukuzi wa bendera ya wito wa Uislamu, Muhammad (ﷺ). Mnamo siku ya Alkhamisi, tarehe 26 Safar, mwaka wa kumi na nne wa Utume sawa na tarehe 12/9/622 283- C.E. (1)
baada ya miezi miwili na nusu takriban kutokea mkataba wa Al-Aqaba al-Kubra, Bunge la Makuraishi Lilikutana Katika jumba la mikutano mchana, (2) na kujadili ajenda hatari kabisa katika historia yake. Mkutano huo ulihudhuriwa na wabunge wote wa makabila ya Makuraishi ili wadurusu mpango wa mwisho utakaohakikisha kummaliza mbebaji wa bendera ya wito Wa Kiislamu na kuondoa kabisa nguvu za mwangaza wake. Watu muhimu waliohudhuria katika mkutano huu wa hatari miongoni mwa wabunge wa makabila ya Makuraishi ni:
1. Abu Jahli bin Hisham ambaye aliwakihsha kabila la Banu Makhzoum.
2. Zubair bin Muh”im na Tuayma bin Adiyy, na Al-Harith bin ’Aamir wakiwa wawakilishi wa Banu Nawfel bin Abdi Manafi.
3. Shayba na ’Utba watoto wawili wa Rabia na Abu Sufyan bin Harbi wakiwa wawakihsha wa Banu Abdi Shamsi bin Abdi Manafi.
4. Al-Nadhri bin Harith (naye ndiye yule ambaye alikuwa amemtupia Mjumbe wa Mwenyezi (ﷺ) matumbo ya ngamia), huyo aliwawakilisha Banu Abdi Daari.
5. Abu Al-Bakhtari, Hisham na Zamua Bin As-wadi na Hakim bin Hizam waliwakihsha Banu Assad bin Abdul-Uzza.
6. Nabih na Munabbih watoto wawili wa Hajjaji waliwakilisha kabila la Banu Jum’ah.
Walipofika kwenye jumba la mkutano kufuatana na wakati ambao ulipangwa aliwatokea Iblis katika sura ya mzee mwenye heshima zake, aliyevaa nguo nzito, akasimama mlangoni, wakamwuliza, “Ni nani wewe?.” Akasema: “Mimi ni mzee katika watu wa Najdi, nimelisikia lile ambalo mmeahidiana kwalo kwa hiyo nimehudhluia pamoja nanyi, ili nisikie yale ambayo mnayasema, na mpate maoni na Nasaha.” Wakasema: “Ingia”, akaingia pamoja nao.