0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YALIYOTANGULI HIJRA, (KUHAMA KWA MTUME ﷺ.


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Baada ya kukamilika kwa mkataba wa Al-Aqaba wa pili, na Uislamu kufanikiwa kuanzisha Dola yake katikati ya jangwa lililojaa ukafiri na ujinga, na kwa kuzingatia hali ngumu ambayo Uislamu tokea mwanzo wa Da’awa yake uliyapata pale Makka, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () aliwaruhusu Waislamu kuhama na kwenda Yathrib (Madina).

Katika jumla ya vikwazo vya Hijra vilikuwa ni mtu kupoteza maslahi yake ya kidunia na kupelekea kujitoa mhanga, kwa kuacha mali na kuhatarisha maisha yake. Jambo ambalo linaweza kummaliza tu pale atakapoanza safari yake ya Hijra.

Waislamu walianza kuhama huku wakiwa wanayaelewa mambo yote hayo. Mushirikina wakawazuia wasihame, kwa sababu ya yale ambayo walikuwa wanayaogopa miongoni mwa hatari za Waislamu kukusanya nguvu zao nje ya eneo la Makka. Mfano wa hayo:

1. Abu Salama (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa mtu wa kwanza kuhama, alihama kabla ya Ba’ia Al-Aqabah Al-Kubra (kubwa) kwa muda wa mwaka mmoja, kwa mujibu wa mapokezi ya Ibn Ishaq, akiwa pamoja na mkewe na mtoto wake. Alipokuwa tayari kwa safari, wakweze walimwambia, ’Wewe umetushinda, Lakini huyu mtu wetu (mke wake Abu Salama) hatukuachii uende naye.” Abu Salama (Radhi za Allah ziwe juu yake) akanyang’anywa mkewe na hilo likawafanya nduguze Abu Salama (Radhi za Allah ziwe juu yake) wakasirishwe na jambo hili alilofanyiwa ndugu yao, wakasema, ”Hatumwachi mwanetu kwa mama yake kwani mmemnyang’anya kutoka kwa ndugu yetu.” Wakavutana kumnshindania yule mtoto na kuondoka naye.

1. Abu Salama (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaelekea Madina peke yake ilhali mkewe baada ya kuondoka mumewe na kupotea kwa mwanawe akawa anatoka kila siku asubuhi nje kwenda kwenye ardhi yenye changarawe huku akilia mpaka jioni, aliendelea katika hali hiyo kwa muda wa mwaka mzima. Mmoja kati ya ndugu zake akamhurumia. Akasema: ”Kwa nini hanmiruhusu nikamfariji huyu maskini? Mmemtenganisha na mume wake na mtoto wake. Wakamwambia, ”Ungana na mume wako kama unataka”, akataka mtoto arejeshwe kwa jamaa zake ndugu wa mume wake. Akatoka akiwa anakusudia kwenda Madina, safari ambayo inafikia kiasi cha kilometa mia tano  na hakuwa na mtu yeyote pamoja naye miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka alipofika mahali paitwapo Tani’im. Alikutana na ’Uthman bin Twalha bin Abi Twalha na baada ya kuielewa hali yake, alifuatana naye mpaka akamfikisha Madina. Alipouona mji wa Qubaa alisema; Mume wako yuko katika kijiji hiki, ingia kwenye kijiji kwa baraka za Mwenyezi Mungu (ﷻ) kisha ’Uthmani akaondoka kurejea Makka. (1)

2. Suhayb (Radhi za Allah ziwe juu yake) alipotaka kuhama makafiri wa Kikuraishi walimwambia, ”Ulikuja hapa ukiwa mnyonge na lofa, mali yako imekuwa nyingi na kutajirika na kufikia hali hii ambayo umeifikia ndio sasa unataka kuondoka na mali yako? Tunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hilo halitakuwa.” Suhayb (Radhi za Allah ziwe juu yake) akawauliza, ”Je, mnaonaje nikiwapeni mali yangu yote mtaniacha niende zangu? Wakasema, ”Ndiyo.” Akasema, ” Kwa hakika mimi nimewapeni mali yangu yote.” Mtume wa Mwenyezi Mungu () akapata khabari na akasema, ”Amepata faida Suhayb, amepatafaida» (2).

3. Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Ayyashi bin Abi Rabia (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Hisham ibn Assi bin Wail (Radhi za Allah ziwe juu yake), waliahidiana kukutana asubuhi siku iliyofuata, kisha wahame kuelekea Madina. Walikutana ’Umar na Ayyash lakini Hisham alizuiwa.

Walipofika Madina walishukia Qubaa, Abu jahli na ndugu yake Al-Harith walikuja kwa Ayyash. Wakamwambia, ”Hakika mama yako ameweka nadhiri kuwa hatochana nywele zake na hatokaa kwenye kivuli hadi akuone. Kwa hiyo mhurumie.” ’Umar akamwambia, ”Ewe Ayyash, kwa hakika kwa jinsi mambo yalivyo, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (ﷻ) watu wako wanakusudia kukufitini na Dini yako, kwa hiyo tahadhari nao.” ”Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu (ﷻ), kama chawa watamuudhi mama yako kiasi cha kutosha bila ya shaka yoyote atachana nywele zake, na joto la jua la Makka likimzidi atajifunika.” Ayyash akaamua kutoka nao, ili ahalalishe kiapo cha mama yake. ’Umar akamwambia, “Kama ukiwa umechukuwa uamuzi huo chukua ngamia wangu huyu kwani ngamia huyu ni bora na mwepesi, usiache mgongo wake, na iwapo utapata mashaka kuhusu jambo lolote kutokana na watu hawa, jiokoe ukiwa juu ya Ngamia huyu.” Akatoka akiwa juu ya ngamia huyo pamoja nao, mpaka walipokuwa njiani, Abu Jahl akamwambia, ”Ewe mtoto wa ndugu yangu, Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika ngamia wangu amekuwa mzito, ni bora tukapokezana? Akasema, ”Si vibaya, niko tayari kufanya hivyo”, akampigisha magoti, waliposhuka na wote kuwa chini walimrukia na kumkamata kisha wakamfunga kamba, na kuingia naye Makka wakati wa mchana na hali ya kuwa amefungwa. Wakawa wakiwanadia watu; “Enyi watu wa Makka wajinga ndio waliwao, wafanyieni wajinga wenu hivi kama’ tulivyomfanya sisi huyu (3)

Hii ni mifano mitatu ya yale ambayo Mushrikina walikuwa wakiwafanyia wale ambao walikuwa wanataka kuhama. Pamoja na yote haya walitoka watu, makundi kwa makundi wanafuatana. Baada ya miezi tokea Mkataba wa Al-Aqabah Al-Kubra, Waislamu hawakubakia Makka isipokuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (), Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Ali (Radhi za Allah ziwe juu yake), wengine ni wale waliozuiliwa na Mushirikina kwa kulazimishwa. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () alifanya maandalizi yake akingojea siku atakayopewa amri ya kutoka, akiwa na Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake). (4)

Bukhari amepokea kutoka kwa Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake); Alisema Mtume wa Mwenyezi Mungu () kuwaambia Waislamu; ”Hakika nimeuona mji wenu wa kuhamia, una mitende iliyo kati ya majabali mawili. Wakahamia baadhi yao Madina na sehemu kubwa ya wale waliokuwa wamehamia Habasha walihamia Madina. Abubakar (alikuwa amejiandaa kuhama kuelekea Madina. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () akamwambia, “Polepole usiwe na haraka, ninatarajia kupewa ruhusa ya kuhama.” Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamwuliza, “Hivi unalitarijia jambo_ hilo?.” Akasema, ”Ndiyo.” Abubakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaizuia nafsi yake na kumsubiri Mjumbe wa Mwenyezi Mungu () afuatane naye; “na akaanza matayarisho ya safari kwa kuwaandaa wanyama wake wawili kwa kuwapa chakula kizuri kwa muda wa miezi minne. (5)


1) Ibn Hislmm, juzuu 1, Uk. 468-470.
2) lbid. Iuzuu 1, Uk. 477.
3) Hisham pamoja na ’Iyash walibaki wamefungwa na Makafiri hadi alipofanya Hijra Mtume (). Mtume () siku moja alisema, ‘Ni nani ataniletea ’Iyash na Hisham? Akajibu Al-Walid bin Al-Walid, ‘Mimi nitakuletea ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.’ Akaondoka Walid kwa kujificha mpaka Makka, huko akamkuta mwanamke akiwapelekea wakina ‘Iyash ‘_na Hisham chakula, akamfuatilia mpaka akafika sehemu waliyofungwa. Ilikuwa ni katika nyumba isiyokuwa na dari, ilipofika jioni alipanda ukuta na akawafungua pingu zao na kuwabeba kwenye ngamia wake hadi Madina (Angalia, Ibn Hisham, juzuu 1, Uk 474-476. Sahihil Bukhari, Juzuu 1, Uk. 558.)
4) lZaad Ma’ad, Iuzuu 2, Uk. 52. 282.
5) Sahihil Bukhari, juzuu 1, Uk. 553.

Begin typing your search above and press return to search.