June 21, 2021
0 Comments
SOMO LA FIQHI
MAANA YA ISTIHADHA
Istihadha: Ni kutiririka damu kutoka kwenye tupu ya mwanamke ikawa haikomi kabisa au ikatike kwa kipindi kichache.
TOFAUTI BAINA YA DAMU YA HEDHI NA YA ISTIHADHA
| DAMU YA ISTIHADHA | DAMU YA HEDHI |
| Nyekundu nyepesi | Nyeusi nzito |
| Haina harufu | Ina harufu mbaya yenye kuchukiza |
| Inaganda (inashikana) | Haigandi (haishikani) |
| Inatoka kwenye kishipa cha uzao cha karibu | Inatoka mwisho wa uzao |
| Damu ya kuashiria kasoro, ugonjwa na uharibikaji | Damu ya afya na ya kawaida |
| Haina wakati maalumu | Inatoka wakati maalumu |