AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Katika mwezi wa Dhul Qa’dah katika mwaka wa kumi wa Utume, mwishoni mwa mwezi wa Juni na Julai mwaka wa 619 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mung-u (ﷺ) alirejea Makka kwa lengo la kuanza upya kuutangaza Uislamu miongoni mwa makabila, na kwa mtu mmoja mmoja. Kwa vile msimu wa Hijja ulikuwa ukikaribia watu walikuwa wanaanza kuja Makka kwa wingi, wengine kwa miguu ‘na wengine kwa wanyama wa kila aina wanaopandwa, kutoka katika miji ya mbali, kwa madhumuni ya kutekeleza ibada zao za Hijja na kufanya biashara, katika masiku yaliyokuwa yakijulikana.
Mtume (ﷺ) aliinyakua fursa hii na akaitumia kwa kuwaendea kabila baada ya kabila, akiwaita kwenye Uislamu kama alivyokuwa akifanya tokea mwaka wa nne wa Utume.
Makabila Aliyoyatangazia Uislamu.
Al-Zahry amesema tumejulishwa kuwa, miongoni mwa makabila ambayo Mtume (ﷺ) aliyaendea na kuyaita na akajidhihirisha kwao ni Banu ’Amir bin Swaa Swaa, Muharib bin Khafswa, Fazara, Ghassan, Murra, Hanifa, Sulaym, Absi, Banu Nassr, Banu Al-Bukaa, Kinda, Kalb, Al-Harithi bin Ka’ab, ’Udhrah na Al-Hadha’rima, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeitikia wito wa Mtume (ﷺ) miongoni mwao (1)
Makabila haya yalitangaziwa Uislamu kuanzia mwaka wa nane wa Utume mpaka msimu wa mwisho kabla ya Hijra. Haiwezekani kutaja mwaka maalum wa kutangazwa Uislamu kwa makabila yote.
Al-Mansour aliye mwanachuoni mkubwa anaeleza kuwa yapo makabila ambayo kutangazwa kwa Uislamu kwao kulifanyika katika msimu wa mwaka wa kumi. (2)
Kwa hakika Ibn Ishaq ameelezea namna alivyokuwa anawalingania na majibu yao, hapa tutataja maelezo hayo kwa ufupi: – .
1) Banu Kalb: inaelezwa kuwa Mtume (ﷺ) alikwenda katika kabila moja miongoni mwao wanaoitwa Banu Abdillah akawalingania kumfuata Mwenyezi Mungu (ﷻ) na akaonesha kwao nia yake njema kiasi chakuwaambia; ”Enyi Banu Abdillah kwa hakika Mwenyezi Mungu (ﷻ) Amelzfanya zuri jinn la baba yenu.” Lakini hawakukubali kamwe kuliamini lile alilokuwa akiwatangazia.
2) Banu Hanifa: Alikuwa akiwafuata katika majumba yao na kuwalingania katika kumtii na kumfuata Mwenyezi Mungu (ﷻ) na akawathibitishia nia njema aliyokuwa nayo kwao. Lakini hakukuwahi kutokea watu miongoni mwa Waarabu waliokuwa na majibu mabaya sana kwake kuliko wao.
3) Banu ‘Amir bin Swaa Swaa: Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikwenda kwao na kuwalingania kumtii na kumfuata Mwenyezi Mungu (ﷻ) na akawadhihirishia nia njema aliyo kuwa nayo kwao. Bahira bin Firas (mtu mmoja miongoni mwao) akasema, ”Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu laiti kama mimi ningemkamata Kijana huyu, Makuraishi wangenila kwa sababu yake”; kisha akasema; ”]e, unaonaje iwapo sisi tutakupa ahadi juu ya mambo yako”, kisha Mwenyezi Mungu (ﷻ) Akakupa ushindi dhidi ya wale ambao wanakupinga, jambo hilo litakuwa ni letu baada yako? ” Akawajibu; “Jambo ni la Mwenyezi Mungu analiweka Annpopataka.” Wakamwambia, ”Hivi itakuaje sisi tujitolee mhanga kwa ajili yako na baada ya kupata ushindi watu wengine waliteke? Hatuna haja na jambo lakk.” Hivyo wakaukataa wito wake.
Wakati Banu ’Amir waliporejea kwao, walizungumza na mzee wao ambaye hakwenda Makka msimu huo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, wakamweleza; ”Ametujia Kijana wa Kikuraishi kutoka katika kabila la Banu Abdil Muttwalib, anadai kuwa yeye ni ‘ Mtume, anatulingania kwenye kumnusuru na anatutaka tusimame nae pamoja na tutoke nae kwenda kwenye miji yetu.” Alipoyasikia maneno hayo yule mzee akaweka mikono yake juu ya kicnwa chake, na kisha akauliza; ”Je jambo hilo lina nafsi ya kudirikiwa?, Je, linaweza kutafutwa na kufuatiliwa baada ya kuponyoka? Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya fulani imo mikononi mwake, haijapata kutokea kutoka kwa watoto wa Ismail .(Alayhi salaam) mtu kudai Utume na kama ni hivyo kwa hakika huo Utume hi jambo la kweli, ni yepi yalikuwa maoni yenu kwake?.” (3)