0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

BARAKA ZA MTUME MUHAMMAD ﷺ KWA BANU SA’AD

BARAKA ZA MTUME MUHAMMAD ﷺ KWA BANU SA’AD


Kwa sababu ya Baraka za Mtume Halima aliona mambo ambayo aliyasimulia kwa kustajabishwa kwake na tumwache yeye mwenyewe atueleze hilo kwa ufafanuzi:

Ibni Ishaq anasema, Halima aliwahi kusimulia kuwa siku moja alikuwa akitoka katika mji wake pamoja na mume wake, na mtoto wake mdogo akiwa ananyonya, alikuwa ni mmoja miongoni mwa kundi la wanawake katika Banu Sa ad bin Bakr, waliokuwa wakitafuta watoto wa kunyonyesha. Jambo hilo lilikuwa katika mwaka wa ukame mwaka wa njaa ambao haukubakisha kitu chochote kwetu, amesema: “Nikatoka nikiwa juu ya punda wangu mwenye rangi nyeupe, pamoja na Ngamia wetu, ambaye naapa kwa Jina Mwenyezi Mungu Ngamia wetu, ambaye naapa kwa Jina Mwenyezi Mungu alikuwa hatutolei sisi tone la maziwa. Usiku pia tulikuwa hatulali kwa jinsi mtoto alivyokuwa akilia kwa sababu ya njaa. Katika nyumba yangu sikuwa na kitu kinachoweza kumtosha, matumaini yetu yote yalikuwa ni katika kusubiri mvua.

Nilitoka nikiwa juu ya punda wangu,kwa hakika nilikuwa nikiomba msaada kwa wasafiri wenzangu mpaka hilo likawa gumu kwao, nilijikongoja hivyo hivyo kwa unyonge mpaka tukafika Makka, tukiwatafuta watoto wa kunyonyesha. Katika sisi hakuna Mwanamke ambaye hakuonyeshwa kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Kila aliyekwenda kwao na kufahamishwa kuwa mtoto ni yatima aliondoka, maana kila mmoja alikuwa anataraji mapato kutoka kwa baba wa mtoto. Kila mmoja alikuwa akiwaza yatima ni kitu gani ni kipi ambacho anaweza kufanya mama yake na Babu yake? Kwa hiyo, hatukumtaka kwa sababu hiyo. Kila mwanamke katika msafara wetu alimpata mtoto wa kumnyonyesha isipokuwa mimi. Tulipokuwa tunajiandaa kurudi nilimwambia mume wangu, ‘Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu , kwa hakika mimi ninaona vibaya kurudi nikiwa kati ya wenzangu na sikupata mtoto wa kumnyonyesha, ninaapa kwa Mwenyezi Mungu nitarudi kwa yule mtoto Yatima nikamchukue.’
Mume wangu hakupinga na akasema, ‘Hakuna ubaya ukifanya hivyo,huenda Mwenyezi Mungu Akatujaalia Baraka kwa ajili yake. Nikamuendea na kumchukua, nilifanya hivyo kwa vile mimi sikumpata mwingine.’ “Nilipomchukua nilirejea naye kambini kwangu, nilipomuweka mapajani mwangu ili kumnyonyesha, matiti yangu yalitoa maziwa, akanyonya mpaka akatosheka, na ndugu yake naye akanyonya mpaka akatosheka, kisha wakalala. llikuwa ni mara ya kwanza kulala naye. Mume wangu akasimama na kuelekea alipo Ngamia wetu, alishangazwa maana ghafla alimkuta amejaa maziwa, akakamua nikanywa mimi pamoja naye mpaka tulipotosheka kabisa na kushiba. Tulilala usiku mwema. Ilipofika asubuhi mume wangu aliniambia, ‘Je, wajua! ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ewe Halima, kwa hakika umemchukua mtoto mwenye kubarikiwa!’, Nikasema, ‘Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu , hakika ninataraji hilo’. Kisha tukatoka, ‘Mimi nikampanda punda wangu, nikamchukua mtoto. Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu , kwa hakika mwendo niliokuwa nakwenda haukuweza kufikiwa na yeyote katika msafara wetu, punda wao hawakuweza kitu chochote katika kuyakata masafa kama nilivyokuwa ninafanya. Wenzangu wakaniambia kwa mshangao, ‘Ewe mtoto wa Abu Dhuayb, nenda polepole na sisi, kwani huyo si Yule punda wako, ambaye ulikuwa umetoka naye?’ Nikawahoji, ‘Kwa nini?’ Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu hakika punda huyu ndiye Yule yule’, 
wakawa wanasema: ‘Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu kwa hakika punda huyu ana jambo.’ Tukaenda mpaka tukafika majumbani kwetu katika miji ya Banu Saad, na siijui ardhi yoyote katika ardhi ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa na ukame mkali kama ilivyokuwa ardhi ya Banu Saad wakati huo. Tulipofika naye, mbuzi wangu wakawa wanarudi jioni hali ya kuwa wameshiba na wana maziwa mengi, tukawa tukikamua na kunywa. Wakati huo hakuna mtu aliyekuwa akikamua maziwa kutoka katika mifugo yake,mpaka jamaa zetu wakawa wakisema kuwaambia wachungaji, hasara ni yenu, wachungeni wanyama wenu pahala anapochungia mchungaji wa binti Abu Dhuayb. Hata hivyo mbuzi wao walikuwa wakirudi na njaa na hawatoi tone 
la maziwa, na mbuzi wangu walikuwa wakirudi wameshiba wakiwa na maziwa mengi sana, tulifahamu kuwa Mwenyezi Mungu Ametuongezea kheri. Hali iliendelea hivyo mpaka ilipokamilika miaka yake miwili ya kunyonyeshwa na nikamwachisha ziwa. Mtoto alikuwa akikua kwa namna isiyofanana na makuzi ya watoto wengine, alipofikisha miaka miwili alikuwa ni kijana aliye mkubwa.” “Tukampeleka kwa mama yake na hali ya kuwa sisi tunatamani sana aendelee kukaa kwetu, kutokana na yale ambayo tulikuwa tunayaona miongoni inwa baraka zake, tukazungumza na mama yake’, nikamwambia, “Mw ache mtoto wangu kwanza mpaka akomae, kwani ninahofia asije akapata magonjwa ya kuambukiza ya Makka. Hatukuacha kumkazania mpaka akaturuhusu kurudi naye.
Kwa hivyo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliendelea kuishi kwa Banu Saad mpaka alipofikisha umri wa miaka minne au mitanow tokea kuzaliwa kwake. Wakati huo ndipo lilipotokea tukio la kupasuliwa kwa kifua chake. *


 * Arraheeq Al Makhtuum 


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.