AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
‘Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ni mtu mwenye kuhieshimika mno na asiyechezewa, kwa hakika kusiliimu kwake kuliibua vurugu na kuwagonganisha Mushirikina na kuwafanya kuwa ni wanyonge na dhalili. Kukawavika Waislarnu nguvu, utukufu na furaha.
Ibn Ishaq amepokea kutoka kwa “Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa; ”Wakati niliposilimu nilifikiria ni nani katika watu wa Makka aliyekuwa na uadui mkubwa zaidi kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) nikakumbuka kuwa ni Abu Jahl, nilikwenda nyumbani kwake na kumgongea mlango, baada ya kufungua mlango na kunikaribisha aliniuliza; “Ni jambo gani ambalo limekuleta?” Nikamjibu kuwa nimekwenda kumueleza kuwa sasa nimékwisha kumwamini Mwenyezi Mungu (ﷻ) na Mjumbe wake Muhammad (ﷺ), na nimeyakubali yale ambayo amekuja nayo. Baada ya maneno hayo, Abu Iahal aliubamiza mlango usoni mwangu na kuniapiza, ”Mwenyezi Mungu akuchukie na ayachukie mabaya yote uliyokuja nayo. (1)
Ibni Al-Jawzy alisema vile vile kuwa ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema baada ya kusilimu kwake, kuwa ilikuwa ni kawaida ya Makuraishi kuwa mtu anapoingia katika Uislamu walimvaa na kupigana , lakini wakati niliposilimu (Umar) nilikwenda kwa mjomba wangu, Al-‘As bin Hashim nikamfahamisha kusilimu kwangu (hakusema kitu) akaingia ndani. ’Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) anaendelea kusema kuwa: ‘Nikaenda kwa mtu miongoni mwa wakubwa wa Kikuraishi (Abu jahl) nae nilipomfahamisha pia akaingia ndani.’ (2)
Ibni Hisham na Ibn Al-]awzy nao pia kwa ufupi wametaja kuwa ‘Umar aliposilimu alikwenda kwa Jamil bin Mu’ammar Al-Jumahy, aliyekuwa mzungumzaji mzuri miongoni mwa Makuraishi na kumueleza kuwa yeye amesilimu. Kwa sauti ya juu kabisa (huyu Jamil) akatoa ulingano kuwa Ibn Al-Khattab ametoka katika dini. “Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliyekuwa nyuma yake wakati huo alimkanusha kwa vile alisema uongo, na kusema yeye ameingia katika Uislamu, Makuraishi wakahamaki na kuanza kupigana nae, walipigana kwa kipindi kirefu mpaka ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaelemewa na kukaa chini. Wakasimama na kumzunguka na yeye akawaambia: “’Panyeni mtakalo fanya, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (ﷻ) laiti tungelikuwa watu mia tatu, tungewaacheni nyinyi au mngetuachia sisi.” (3) Baada ya hapo Mushirikina walimtafuta nyumbani kwake wakikusudia kumwua.
Bukhari amepokea kutoka kwa Abdillah bin ’Umar, kuwa alisema: “Wakati Umar akiwa yumo nyumbani kwake amejaa khofu, ghafla alimjia Al-’As bin Waili Al-Sahmy (Abu Amru) akiwa na nguo mbili za rangi moja zilizo nzuri na_ kanzu iliyikuwa na pindo la hariri, alikuwa akitoka miongoni mwa watu wa Banu Sahm, nao walikuwa ni marafiki Wakati wa Ujahilia, akamuuliza “Una nini?” Akamjibu kuwa, Jamaa zako wamedai kuwa wataniua kwa sababu niméingia katika Uislamu. Nae akamwambia, ’Basi usihofu, maana sasa hakuna njia ya kukufikia hilo tena baada ya kulisema kwangu umekuwa katika amani.’ Al-‘As akatoka na kukutana na watu jangwani, akawauliza; ”Mmekusudia kwenda wapi?” ‘-Nakajibu, ”Kwa Ibn Al-Khattab ambaye ametoka katika dini.” Ibn Al-‘As akawaeleza kuwa, ’Hakuna njia ya kumuendea kumdhuru’, hivyo wakamuacha na kutawanyika. (4)
Katika mapokezi ya Ibnu Ishaq anasema: ”Wallahi,.walikuwa kama watu waliokuwa wamevaa nguo na Wakavuliwa kwa aibu iliyowafika kwa kuadhirika kwao. (5)
Baada ya hapo Mushrikina wa Makka hawakumfanya kitu tena “Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake). Mujahid amekeoa kutoka kwa Ibn Abbas ya kuwa “Nilimuliza ‘Umar bin Al-Khattab, kwa sababu gani ameitwa Al-Faruq?” (yaani mwenye kutenganisha baina ya haki na batili). Nae akamjibu kuwa, Hamza alisilimu kabla yangu kwa siku tatu, kisha akanisimulia kisa cha kusilimul kwake, na mwishoni mwake akasema kuniambia: Wakati niliposilimu nilimwuliza Mtume (ﷺ), “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) hivi sisi si tupo katika njia ya haki tukifa au tukiwa hai?.” Akajibu; bila shaka tupo katika haki
na akaendelea kusema: ”Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko katika Qudra Yake, kwa hakika nyinyi mko katika haki mkiwa hai‘ au mmekufa” Nikauliza, “Kwa nini, tunalingania kwa siri?, Ninaapa kwa Yule Ambaye_ Amekutuma na ukweli, kwa hakika lutatoka na kuutangaza Uislamu wetu hadharani.” Baada ya hapo tukatoka katika safu mbili Hamza akiongoza safu moja na mimi nikiongoza safu ya pili. Tulikwenda mpaka tukaingia msikitini mchana kweupe na mara Mushrikina wa Kikuraishi kutuona sisi (mimi na Hamza) ikawachukiza hali hiyo na kuwapa huzuni ambayo haijawahi kuwapata mfano wake. Siku hiyo ndiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu akaniita mimi Al-Faruuq” Ibn Masoud (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akisema: “‘Hatukuwa tukiweza kusali mbele ya Al-Ka’aba mpaka ‘Umar aliposilimu”,(5)
Imepokewa kutoka kwa Suhayb bin Sinan Al- Roumy (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema kuwa; ’Wakati ‘Umar aliposilimu ulidhihiri Uislamu na ukawa unalinganiwa bila ya kificho na tukawa’ fukikaa pembezoni mwa Al-Ka’aba tukifanya ibada zetu. Tulilipiza kisasi kwa yule aliyetufanyia uzito na tukamrudishia baadhi ya yale aliyokuwa akitufanyia.’
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Masoud (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa amesema: (Kutokea siku aliposilimu Umarr tulianza kupata nguvu. (6)