0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

BAADA YA KUFA

BAADA YA KUFA

Nini kufa? Kufa ni kuepukana roho na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ala yake na kumuepusha mtu na amali yake na watoto wake na mke wake. Kufa inakata utamu wa maisha ya kilimwengu na kwenda ulimwengu mwengine. Mtu ambae alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu amepata khasara baada ya kufa. Na yule ambae alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na ina kamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba Mtu anapo kufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote. Kudhania hivyo ni kosa kubwa bali hakika Mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya Akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

Njooni tuangalieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam zina semaje kujibu suala; Ni nini baada ya kufa ?
Hakika Qu’rani imebainisha wazi na Hadithi za Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam yatakayo tokea baada ya kufa. Wakati anapokufa Mwanadamu na akazikwa, jambo la kwanza linalompata ni fitina ya kaburi.

Imepokewa katika sahihi mbili ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Anas Bin Malik Akipokea kutoka kwa Mtume ﷺ:

إِنَّ الْعَبْدَ إِذَا وُضِعَ فِي قَبْرِهِ وَتَوَلَّى عَنْهُ أَصْحَابُهُ وَإِنَّهُ لَيَسْمَعُ قَرْعَ نِعَالِهِمْ ، أَتَاهُ مَلَكَانِ فَيُقْعِدَانِهِ فَيَقُولَانِ : مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ لِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ؟ فَأَمَّا الْمُؤْمِنُ فَيَقُولُ : أَشْهَدُ أَنَّهُ عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ ، فَيُقَالُ لَهُ : انْظُرْ إِلَى مَقْعَدِكَ مِنَ النَّارِ قَدْ أَبْدَلَكَ اللَّهُ بِهِ مَقْعَدًا مِنَ الْجَنَّةِ فَيَرَاهُمَا جَمِيعًا ، قَالَ قَتَادَةُ : وَذُكِرَ لَنَا أَنَّهُ يُفْسَحُ لَهُ فِي قَبْرِهِ ، ثُمَّ رَجَعَ إِلَى حَدِيثِ أَنَسٍ , قَالَ : وَأَمَّا الْمُنَافِقُ وَالْكَافِرُ فَيُقَالُ لَهُ : مَا كُنْتَ تَقُولُ فِي هَذَا الرَّجُلِ ؟ فَيَقُولُ : لَا أَدْرِي ، كُنْتُ أَقُولُ مَا يَقُولُ النَّاسُ ، فَيُقَالُ : لَا دَرَيْتَ وَلَا تَلَيْتَ وَيُضْرَبُ بِمَطَارِقَ مِنْ حَدِيدٍ ضَرْبَةً ، فَيَصِيحُ صَيْحَةً يَسْمَعُهَا مَنْ يَلِيهِ غَيْرَ الثَّقَلَيْنِ

[Hakika mja anapo wekwa katika kaburi lake na wakaondoka watu wake, Anasikia mlio wa viatu vyao. Akasema wanamjia Malaika wawili wakamkalisha wakamuambia unasemaje juu ya mtu huyu. Akasema: Ama Muislamu atasema: Nilikuwa nikishuhudia ya kwamba ni mja wa Mwenyezi Mungu na ni Mtume wake. Akasema: Ataambiwa angalia makao yako motoni umebadilishiwa pepo Atayaona makao mawili. Amesema Qatada tumeelezwa: hukunjuliwa kaburi lake. Ama mnafiki na Kafiri ataulizwa unajua nini juu ya Mtu huyu atasema sijui nilikuwa nikisema walivyokuwa wakisema watu ataambiwa hukujuwa na wala hukutaka kujua atapigwa nyundo ya chuma moja moja, atapiga ukelele watasikia watu wote wasiokuwa viumbe aina mbili (wanadamu na majini)].     [Imepokewa na Bukhari]

Na imepokewa na Abu Ayyub radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Amesema:

[خرج رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بعدما غَربت الشَّمس، فسَمع صوتًا، فقال: [يَهودُ تُعذَّب في قبورها

[Alitoka Mtume ﷺ na jua limetoka, Akasikia sauti ya Yahudi ana adhibiwa katika kaburi lake’]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Kwa hivyo, Alikuwa Mtume haswali swala yeyote ila alikuwa akijilinda na adhabu ya kaburi. Na akaamrisha hivyo watu wake].
Kisha ataadhibiwa kafiri na mnafiki. Na Mu’mini atastarehe. Basi tujiulize nafsi zetu, je tumeandaa jawabu ya masuali ya kaburini. Ewe mja wa Mwenyezi Mungu, hakika hiko ni kiyama kitakuja hakina shaka. Na baada yayote atawafufuwa Mwenyezi Mungu walioko kwenye makaburi. Na dalili ni Aya tukufu:

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ  قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ}  يس:78-79}

[Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye ihuisha mifupa nayo imekwisha mung’unyika?Sema: Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.]  [Yaasin : 77 – 79].

Halafu atawakusanya watu wote kwa ajili ya hisabu. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ:

مَن يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا

[Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake]   [Al-Israa :97]

Haya ndiyo matukio ya kuogopesha utawaona wabaya na madhalimu na wanafiki wameinamisha vichwa vyao, hawarudishi macho yao, wala hasemi siku hiyo ila aliye pewa ruhusa na Mwenyezi Mungu ﷻ. Na nyoyo siku hiyo zimefika kooni wamekasirika na madhalimu hawana muombezi wala rafiki mwenye kutiiwa. Na siku hii kiasi chake ni miaka khamsini alfu.
Wakati huo watu watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala. hakuna pa kufichika. Siku hiyo watu watatoka makaburini vikundi vikundi kwa ajili ya kuona vitendo vyao. Na itaanza hisabu. Amesema Mtume ﷺ:

يجاء بالكافر يوم القيامة فيقال له أرأيت لو كان لك ملء الأرض ذهبا أكنت تفتدي به فيقول نعم فيقال له قد كنت سئلت ما هو أيسر من ذلك

[Ataletwa kafiri siku ya kiama aambiwe waonaje lau ungekuwa na mjazo wa ardhi dhahabu ungalijikomboa? atasema ndiyo. Ataambiwa umeulizwa ambalo ni sahali kuliko hilo]. [Imepokewa na Bukhari]

Na katika mapokezi mengine:

[أردت منك ما هو أهون من هذا وأنت في صلب آدم أن لا تشرك شيئا فأبيت إلا أن تشرك بي]

[Nimekuuliza ambalo ni sahali kuliko hili na wewe uko katika mgongo wa Adam usimshirikishe Mwenyezi Mungu ﷻ ukakataa ila unishirikisha na viumbe vingine].
Ndugu Muislamu haya ni baadhi ya yale yatakayo tokea siku ya kiama, mbali na yale tuliyo ghafilika nayo. Na kila mmoja katika sisi atakuwa juu ya yale aliyo yafanya katika maasi. Ewe hakimu, Ewe rais, utatubiya lini? rudi kwa Mwenyezi Mungu ﷻ . Utamwambia nini Mola wako. Je hukumbuki neno la Mtume ﷺ:

[ما من عبد يسترعيه الله رعية يموت يوم يموت وهو غاش لرعيته إلا حرم الله عليه الجنة]     متفق عليه

[Hakuna mchungaji yoyote aliye pewa uchungaji na Mwenyezi Mungu, atakufa siku atakayo kufa na yeye ni mdanganyifu ila Mwenyezi Mungu atamuharamishia pepo].  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Enyi mawaziri na manaibu hamuogopi Mwenyezi Mungu kwa mliyo yabeba juu ya mabega yenu. Je mume jiandaa vipi na hali hii ya utisho miongoni mwa fitina ya kaburi na adhabu yake kukusanywa kwa ajili ya hisabu. Nini mume jianda na siku hiyo. Ewe Mwenye kufanya khiyana, Je utawacha lini khiyana zako, utasimamisha lini swala. Rudi kwa Mwenyezi Mungu ﷻ. Na wewe mwizi utaaacha lini wizi wako kwa hakika huna budi lazima upitie njia hii ngumu. Na wewe barobaro umejiandaa vipi na siku hii. Je umejiandaa na siku ya kufa. Na wewe msichana wadhani ya kwamba kifo hakitakuja kwako?
Na baada ya hapo zifunguliwe vitabu. Na wenye kupewa vitabu ni aina mbili; ni mwenye kupokea kitabu kwa mkono wa kulia, na mwenye kupewa kitabu kwa mkono wa kushoto. Kisha iwekwe mizani kwa uadilifu siku ya kiama. Baada ya hayo itakuja sirat na kila mmoja atapitia njiya hiyo. Tunamuomba Mwenyezi Mungu ﷻ atuafikie tuweze kufaulu katika siku hii nzito.

SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH YUSUF ABDI

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.