0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ATHARI YA MASIA KATIKA MAISHA YA BINADAMU

ATHARI YA MASIA KATIKA MAISHA YA BINADAMU

Himidi zote na shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu alieumba Mbingu na Ardhi akaumba na binadamu kwa malengo ya kumuabudu yeye peke yake. Aliyeweka Twaa na Maasia, mwenye kumtii ataingia peponi na mwenye kumwasi ataingia motoni. Swala na Salamu zimshukie kipendi chetu Mtume Muhammad ﷺ Yeye na Aali zake na Swahaba zake wote.

Hakika maasia yana athari mbaya kwa mtu mmoja bali kwa mujitamaa wote. Na wala hakuna shaka ya kwamba maasia wanayo fanya watu usiku na mchana athari ambayo inaangamiza mtu mmoja na jamii yote na maisha yote. Kwa hivyo, nguzo ya maisha na kutengenea kwa maisha ni katika twaa na kwa msimamo juu ya amri ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na kufuata sharia ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyo safi. Na kujiepusha na twaa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)ni kumfuata shetani.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعَنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً ۖ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ ۙ وَنَسُوا حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُوا بِهِ ۚ وَلَا تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىٰ خَائِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاصْفَحْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ

[Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.]    [Al-Maidah : 13].

ATHARI YA MAASIA

1- Nyoyo kuwa ngumu
2- Kubadilisha maneno ya Allah (Subhaanahu wa Taala) bila ya kujali
3- Raana ndani ya moyo nayo moyo kuwa mweusi. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala (Si hivyo! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao kwa maovu waliyoyachuma). Inaonyesha ya kwamba maasia yana athari mbaya sana, nazo ni kuwa nyeusi nyoyo za watu wenye kuasi hapo huwa hazijui mema wala mabaya, haziamrishi mema wala hazikatazi mabaya.
4- Kusahau kitabu cha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala. Na tunaposahau maagizo ya Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala) ni kuishi maisha mabaya. Kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ}

[Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu. Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona? (Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa.]             [Twaha: 124-126]

– Athari kubwa ya maasia na iliyo khatari ni ugomvi baina ya mja na Mola wake.
– kuwa mzito kumtii Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)
– Kukosekana hifadhi ya Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)
– Kusalitiwa na maadui na kuwa dhaifu mbele ya adui pamoja na kuondolewa utisho kutoka katika nyoyo za maadui
– Kudhihiri njaa na kuondoshwa baraka katika riziki.

SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ATHMAN SHEE


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.