ASILI YA UTATU MTAKATIFU
Mwana Historia na Msomi wa zamani Edward Gibbon katika kuueleza utatu mtakatifu anasema hivi:
“Kadiri wakristu wanavyoendelea kutafuta jibu sahihi kutokana na fikra yenye makosa, basi wajue
Wako katika giza la kuchanganyikiwa, na bila shaka watapingana wenyewe kwa wenyewe.”
Asilimia kubwa ya wakristu wanajua kihakika kuwa utatu mtakatifu hauna misingi ya Mola au vitabu vitukufu, na ndio kwa maneno ya Edward Gibbon, utatu mtakatifu umeleta utesi mkubwa baina yao , hivi kwamba Jehova Witness hawakubali kabisa fikra hii na kilicho salia kwa ndugu wakristu ni kwao kuingia kwenye suluhu ya matatizo yao yote nao ni UISLAM. Utatu Mtakatifu ni kitendawili kwa ulimwengu wa ukristu, na ROMAN CATHOLIC wametumia mbinu zote duniani ili fikra hii ipate nguvu, lakini kila wanapo jenga kunaporomoka kwa haraka.
Muasisi wa fikra hii na ile maarufu kama “The Catholic Creed” asema ;
“Kuna Baba mmoja, na kuna Mwana na Roho Mtakatifu ni mungu
mmoja, na si waungu watatu,
Bali mmoja”
Ndugu msomaji twajua sote kuwa Baba hawezi kuwa na umri sawa na mwana, jambo la pili roho mtakatifu na mwana ni viumbe, twaulize ni katika hali gani wote huyeyuka na kuwa na kuwa mmoja? Haya ndiyo mashaka ya huyo atakaye kuwa mkristu, ima uyabebe mashaka hayo au uukubali Uislam. Athnasia muasisi wa fikra hii ya utatu mtakatifu,alikuwa kasisi wa Alexandria, huko misri alilenga fikra hii idumu kwa mda mrefu, kwa hivyo wakaweka mikakati maalum namna ya kuwasaza wapinzani kama Jehova witness, Appostolic church ambao ni maadui wa utatu.
Katika makundi ya kwanza kuukataa utatu mtakatifu ni Ebionites kutoka Nazareth ambao walimtambua Nabii Yesu Mwana wa Maryam kama mmoja wa Manabii wakubwa waliotimilizwa na Mola muumba. Twajua sasa kuwa kutoka mwaka wa 318-325, kulikuwa na mjadala mkubwa baina ya Arius, kiongozi wa la Appostolic waliopinga utatu, na Bishop Alexander wa R.C, hapa ukweli ukabainika na uadui wao ukashamiri hata leo.
Baadhi ya walio pinga utatu, waliingiza hii fikra ya mungu kuwa BABA ili kuhafifisha utatu kunako miaka kati ya 180-210 .
we walipinga vikali lakini waweza kuona iblis alivyowavuruga watu akili zao.
Kasisi Pothinus wa Lyons [France] aliuwawa kwa kupinga utatu, na kasisi Iraneus aliyemrithi akamwandikia Pope wa zama zake akimrai asimamishe mauaji kwa wanaopinga utatu.
Kasisi Tertullia anayesemekana kuliongoza kanisa la Afrika aliendeleza sana matumizi ya neon Trinity linalo tokana na neon la kilatin Trinitas, waweza kuona kulikuwa na mikakati maalum ya kuendeleza fikra hii.
Ili kupunguza makali ya utatu, kasisi Arius akaelta uzushi mwingine kuwa Yesu ni mwana wa mungu na fikra ikashika hata leo baadhi ya makanisa kushikilia kuwa Yesu ni mwana wala si mungu, lakini Emperor Constantine aliualikia mkutano mkuu [General Assembly] wa kanisa katoliki mwaka wa 325 huko Nicea, ambapo makasisi 318 walihudhuria ili kuusimamisha ukristu, na kuikuza imani hii ya utatu. Kabla udongo haujakauka Emperor Theodosius wa Rome alialikia mkutano mwingine mwaka wa 381A.D ambapo makasisi 186 walihudhuria na ni katika mkutano huu ambapo maagizo kadhaa yalipitishwa, kwanza ilikuwa ni kuutambua orthodox.
Jambo linguine ni kuwa huyu mtawala hakuutambua tu utatu mtakatifu, bali alitoa amri kuwa kila anaye upinga utatu lazima atiwe katika hukumu ya kufa, wengi waliuwawa kwa amri hii ya mwaka wa 383 A.D.
Karne ya 17, John Biddle wa kanisa la Unitarian Church nchini Uingereza alichapisha jarida lenye anwani “Hoja 12 kupinga kuwa Roho mtakatifu ni mungu” mwaka wa 1645, John Biddle alifungwa jela, na baada ya kutumikia kifungo, aliitwa na bunge la Uingereza, lakini akakataa kwenda, lakini bunge likaanza kutunga mswaada dhidi yake, na mwaka wa 1648, bunge likapitisha sheria inayoitwa “SEVERE ORDINANCE ACT” inayosema;
“Anyone who denies trinity, or divinity of jesus or the holy spirit would suffer Death
The benefit of clergy”
Hapa utaona serikali inauhami ukristu kupitia bunge lao na hata leo mambo ni hayo hayo. Wakristu wa leo yawafaa mno kuzipongeza serikali za dunia na Constantine ambaye aliueneza utatu kwa nguvu za dola yake kwa takriban miaka mia tatu [300] .
Kabla ya haya yote alikuweko Emperor Nero alitoa amri ya kuuwawa kila aliyekuwa mkristu katika himaya yake, na wengine husema huenda Constantine alikuwa anawasahaulisha wakristu hayo mauaji ya halaiki. Edward Gibbon anaieleza zama hizi za kutisha hivi:
“They died in torments, and their torments were embattled by insults and devisions. Some were nailed on the crosses, others were sewn up in skins of wild beasts and exposed to wild dogs, others were smeared with combustible materials and were used to illuminate the darkness of night…………. Those who survey with curious eyes, the revolution of mankind may observe the gardens and the circus of Nero on the Vatican which were polluted with the blood of first Christians…………….” .
Katika utawala wa Diocletian amri ilitolewa kuwauwa wote waliopinga utatu mtakatifu, makanisa mengi yakatiwa moto, na zaidi ya makasisi wao 2000 wakauwawa, la kusikitisha ni kuwa leo Rome ndio makao makuu ya ukristu!. Wale waliochukua kuuongoza ukristu, POPE, walikuwa ni watu wa ajabu sana, mfano Constantine alimwuua mwanawe crispus na mkwewe fausta kwa sumu, Ma-pope wengine walifuata nyayo hizo hizo.
1.Pope Benedict IX – 1032—–1048
– Alikuwa mlawiti wa waume na wanawake
-Alikuwa akifanya tendo la ndoa na wanyama
-Alikuwa ni mwuaji
-Alikipenda sana ushirikina
-Aliabudu shetani
2. 2.Pope Gregory VIII ——– 1073-1085
-Aliamuru Biblia isisomwe kabisa
-Kila aliyepatikana aliuwawa tu
3. 3.Pope Boniface VIII——— 1294-1305
-Alikuwa haamini mwenyezi mungu
-Alikuwa ni msenge
-Alikuwa akila nyama wakati wa lent
4. 4.Pope John XXIII—————- 1410-1415
-Alikuwa mwizi wa baharini
-Alikuwa kasisi siku moja tu,
-Siku iliyofuata alichaguliwa kuwa POPE
IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.