0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ARBAIN NAWAWIY HADITHI YA 38 ATAKAE MFANYIA UADUI WALII WANGU NIMEMTANGAZIA VITA


الحديث الثامن والثلاثون


“من عادى لي وليا فقد آذنته بالحرب”


عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال: قال رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : [إنَّ الله تَعالَى قَال : مَنْ عَادَى لي وَلِيّاً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُهُ عَلَيْهِ، وَلا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إلَيَّ بِالنَّوَافِلٍ حَتَّى أُحِبَّهُ، فإذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بهِ، وَيَدَهُ الّتي يَبْطِشُ بهَا، وَرِجْلَهُ الّتي يَمْشي بِهَا، وَلَئِنْ سَأَلِني لأعْطِيَنَّهُ، ولَئِن اسْتَعَاذَنِي لأُعِيذَنَّهُ]

رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



HADITHI YA 38


ATAKAE MFANYIA UADUI WALII WANGU NIMEMTANGAZIA VITA


Kutoka kwa Abu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye amesema kuwa Mtume ﷺ kasema: [Mwenyezi Mungu kasema: Anayeonyesha uadui kwa Walii Wangu (rafiki wa karibu, yaani mja mtiifu aliye karibu naye) , nitatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote ninachokipenda zaidi kama zile amali nilizomuwajibisha, na mja Wangu anazidi kukaribia Kwangu kwa amali njema zisizokuwa wajibu ili nimpende. Ninapompenda, Ninakuwa masikio yake anayosikilizia (yaani Allah atamjaalia asikie mazuri kama Qur’an, Dhikr, Mawaidha n.k. Na sio Muziki, Masengenyo, na Machafu mengine), macho yake anayoonea (yaani Allah atamfanya macho yake yawe yanatazama yale ya kheri), mikono yake ambayo anakamatia (Allah atafanya mikono yake ikamate vile vya halali na kufanya yale yanayomridhisha Allah), miguu yake anayoendea (na Allah ataifanya miguu yake isitembee kuyaendea ila yale mema, ya kheri na Atakayoridhika nayo Yeye Allah). Anaponiomba (kitu) bila shaka Ninampa, na anaponiomba ulinzi bila shaka Nitamlinda.]
[Imepokelewa na Al-Bukhari]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.