0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ARBAIN NAWAWIY HADITHI YA 10 KUHIMIZA KUTUMA TUMO LA HALALI


الحديث العاشر


“إن الله طيب لا يقبل إلا طيبا”


عن أبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قاَل رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم : [إنَ الله تعالى طَيِّبٌ لا يَقْبَلُ إلا طَيِّباً، وإنَّ الله أَمَرَ المُؤمِنينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلينَ فقال تعالى: {يا أَيُّها الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيَّباتِ واعمَلُوا صالحاً}  وقال تعالى: {يا أَيُّها الَّذِينَ آمَنُوا كلُوا مِنْ طَيِّباتِ ما رَزَقْناكُمْ}  ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إلى السَّماءِ يا رَبُّ يا رَبُّ، ومَطْعَمُهُ حَرَامٌ، ومَشْربُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ وغُذِّيَ بالحَرَامِ، فأَنَّى يُسْتَجَابُ لهُ

رَوَاهُ مُسْلِمٌ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى



HADITHI YA10


KUHIMIZA KUTUMA TUMO LA HALALI .


Kutoka kwa Abu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye alisema: Amesema Mtume Rehma na amani ziwe juu yake, [Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwema na hakubali ila kilicho chema tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha Waumini kufanya yale aliyowaamrisha Mitume, na Yeye Alie tukuka kasema “Enyi Mitume Kuleni katika vitu vyema na mfanye yaliyo sawa” . Mwenyezi Mungu alie tukuka akasema :” Enyi mlioamini kuleni katika vitu vyema ambavyo tumekuruzukuni” Kisha akataja (kisa cha yule) mtu aliyesafiri safari ndefu, kachafuka na kajaa mavumbi na huku anayanyua mikono yake mbinguni akisema “Ewe Mola! Ewe Mola! Nipe kadhaa, nikinge na kadhaa wakati chakula chake cha haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na kivazi chake ni cha haramu, na anashibishwa na haramu, je, vipi atajibiwa (dua zake?)]    [Imepokelewa na Al-Bukhari na Muslim]


SIKILIZA SHEREHE YA HADITHI HII NA USTADH MUHAMMAD RAJAB

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.