0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ALAMA ZA LAYLATUL QADR

ALAMA ZA LAYLATUL QADR

ALAMA ZA LAYLATUL QADR

1. Ni usiku ambao hauna joto wala baridi kali.
Kutoka kwa Jaabir ibn Abdillahi radhi za Allah ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume :

[إني كنتُ أريتُ ليلة القدر ثم نَسيتُها وهي في العشر الأواخر، وهي طلقة بلجة لا حارة ولا باردة]    [رواه إبن خزيمة]

[Nilikuwa nimeoneshwa Lailatu Al-qadr, kisha nikasahaulishwa, nayo iko katika nyakati za usiku wa kumi la mwisho, nao ni usiku wenye bashasha unang’ara usio na joto wala baridi]     [Imepokewa na Ibnu Khuzeymah].

2. Jua linatokeza Asubuhi yake jeupe halina Miale.
Anasema Ubeyi ibn Ka’ab radhi za Allah ziwe juu yake alipoulizwa kuhusu dalili za Lailatu Al-qadr:

[وأمارتها أن تطلع الشمس في صبيحة يومِها بيضاء لا شعاع لها]      [رواه إبن حبان]

[Na dalili yake ni kuchomoza kwa jua asubuhi yake likiwa leupe halina miale]. [Imepokewa na Ibnu Hibbaan]

Na katika upokezi wa Muslim: [Jeupe halina miale].

MAELEZO
1. Ni juu ya kila muislamu kuzidisha kufanaya ibada katika siku kumi za mwisho za mwezi wa ramadhani kwa sampuli ya ibada mbali mbali kwa sababu ni masiku bora ya mwaka.

2. Ni juu ya Muislamu asipoteze wakati wake katika masiku matukufu na msimu wa kheri kwa kufanya upuzi na mchezo na kuzurura masokoni, na kutembea sehemu zisizo kuwa nahaja.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.