0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ADABU ZA KWENDA HAJA

SOMO LA FIQHI

Dini ya uislamu imefunza kila kitu,hakuna jambo kubwa wala dogo ila limeelezewa,na katika yaliofunza ni adabu za kwenda haja,ni mambo gani awajibika afanye mwenye kutaka kwenda choni,na ni mambo gani ni haramu na ya chukiza kufanya yote hayo yamefundishwa katika uislamu,na hii ni kuonesha uzuri wa dini hii.

Suali: Ni mambo gani awajibika kufanya mwenye kutaka kwenda haja?

Jawabu: Mambo Yanayopasa kufanya wakati wa kwenda haja ni haya yafuatayo:

1. Kufunika uchi usionekane na watu wakati wa kwenda haja, kwa neno lake Mtume ﷺ:

[ستر ما بين أعين الجن ، وعورات بني آدم ، إذا دخل أحدهم الخلاء أن يقول : بسم الله]  رواه الترمذي

[Kuweka kizuizi baina ya macho ya majini na uchi wa binadamu angiapo chooni mmoja wenu ni aseme “Bismillah”]      [Imepokewa na Tirmidh.]

2. Kujiepusha asiingiwe na najisi nguoni mwake au mwilini mwake, na akiingiwa na najisi yoyote aioshe. Kwa hadithi iliyothubutu kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alipita kwenye kaburi mbili na akasema:

[ وما يعذبان في كبير ؛ أما أحدهما فكان لا يستتر من البول ]    رواه أبوداود

[Hawa wawili wanaadhibiwa. Na hawaadhibiwi kwa jambo kubwa. Ama huyu hakuwa akijihifadhi na mkojo]       [Imepokewa na Abu Daud]

3. Kujiosha kwa maji au kujipangusa kwa mawe, kwa hadithi ya Anas bin Malik t kuwa alisema:

كان رسول الله صلى الله عليه وسلم : يدخل الخلاء فأحمل أنا وغلام نحوي إداوة من ماء وعنزة فيستنجي بالماء

[Mtume ﷺ alikuwa akiingia chooni, na mimi nikimbebea, pamoja na mtoto kama mimi, chombo cha maji na bakora, akachukua maji akajisafishia nayo]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Suali: Nimambo Yanayoharamishwa kufanya wakati wa kwenda haja?

Jawabu: Mambo yanayohamishwa kufanya wakati wa kwenda haja ni haya yafuatayo:

1. Kuelekea kibla au kukipa mgongo wakati wa kwenda haja jangwani. Ama kwenye majengo, lililo bora zaidi ni kuacha kujilazimisha na hilo, kwa kauli yake Mtume ﷺ:

 [إذا أتيتم الغائط فلا تستقبلوا القبلة بغائط ولا بول ، ولا تستدبروها ، ولكن شرقوا أو غربوا ]    متفق عليه

[Mkienda haja kubwa msielekee kibula, na msikipe mgongo kwa kukojoa wala kwa haja kubwa, lakini elekeeni mashariki au magharibi]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Kuingia haja kwenye njia ya watu kupita au kwenye kiuvuli na sehemu za wao kukaa. Mtume ﷺ amesema:

[اتَّقُوا اللاعِنَيْنِ ” قَالُوا : وَمَا اللاعِنَانِ يَا رَسُولَ اللَّهِ ؟ قَالَ : الَّذِي يَتَخَلَّى فِي طَرِيقِ الْمُسْلِمِينَ وَفِي ظِلِّهِمْ]     رواه مسلم

[Ogopeni vitu viwili vinavyosababisha mtu kulaniwa. Wakasema: ni vitu gani hivyo ewe mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni(kitendo cha) yule anayeingia haja kwenye njia ya watu kupita au kwenye kivuli cha watu kukaa]       [Imepokewa na Muslim.]

3. Kuingia na Msahafu chooni, kwa kuwa kitendo hiko kinaonesha dharau kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

Suali: Ni yapi Yanaopendekezwa kufanya wakati wa kwenda haja?

Jawabu: Yanayopendekezwa kufanya wakati wa kwenda haja ni haya yafuatayo:

1. Kujiepusha na watu wakati wa kwenda haja jangwani

Aseme angiapo chooni:

[بسم الله ، اللهم إني أعوذ بك من الخبث والخبائث]       رواه البخاري ومسلم

[Kwa jina la Mwenyezi Mungu. Ewe Mwenyezi Mungu! Mimi najilinda kwako kutokana na Mashetani wa kiume na wa kike]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Kutanguliza mguu wa kushoto angiapo chooni na mguu wa kulia atokapo.

Aseme anapotoka:

[غفرانك]    رواه أبوداود

[Naomba msamaha wako.]       [Imepokewa na Abu Daud.]

Suali: Ni yapi Yanao chukiza kufanya wakati wa kwenda haja:

Jawabu: Yanao chukiza kufanya wakati wa kwenda haja ni haya:
1. Kusema wakati wa kwenda haja (chooni) au kuzungumza na watu isipokuwa kwa haja (dharura).

 عن ابن عمر قال [مر رجل على النبي صلى الله عليه وسلم وهو يبول فسلم عليه فلم يرد عليه]   رواه مسلم

Kutoka kwa  Ibn Umar kwamba [mtu mmoja alipita kwa Mtume ﷺ naye yuwakojoa, akamsalimia Mtume, asimrudishie salamu]      [Imepokewa na Muslim.]

2. Kuingia chooni na kitu chochote chenye utajo wa Mwenyezi Mungu aliyetukuka, isipokuwa akichelea kuwa kitaibwa na mfano wake, kwa kuwa Mtume ﷺ alikuwa akiingia chooni akiiweka pete yake.

3. Kushika tupu kwa mkono wa kulia au kutamba au kupangusa kwa mawe kutumia huo mkono, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

لا يُمسِكن أحدكم ذكره بيمينه وهو يبول ، ولا يتمسح من الخلاء بيمينه ، ولا يتنفس في الإناء]     رواه البخاري]

[Asishike mmoja wenu dhakari (tupu ya mbele) yake kwa mkono wa kulia wake akiwa yuwakojoa wala asijipanguse kwa mkono wake wa kulia baada ya kwenda haja wala asivuvie kwenye chombo]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

4. Kukojoa kwenye mpasuko na pango ili asidhuriwe na wadudu wanaotembea au adhuriwe na wao.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.