0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ABU TWALIB ANAWAKUSANYA BANU HASHIM NA BANU ABDIL MUTTALIB


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Pamoja na hali na mazingira yake kubadilika, Abu Twalib hakuacha kuwa na khofu juu ya nini watafanya Mushirikina dhidi ya mtoto wa ndugu yake. Kwani alikuwa akiyaangalia matukio yote yaliyopita, hasa kwa kuzingatia  kuwa Mushirikina walimtishia kuwa kama ataendélea kumuunga mkono Mtume () watagombana naye.

Hawakukata tamaa, baadae walifanya mbinu za kutaka makubaliano ya kubadilishana mtoto wa ndugu yake na ‘Umara bin Al-Walid ili wamuue. Upo wakati Abu Jahal alikwenda kwa mtoto wa ndugu yake na jiwe kubwa ili amponde na alikuwa akifikiri pia jinsi ‘Utbah bin Uqba bin Abi ‘Mu’ait alivyotaka kumnyonga mtoto wa ndugu yake kwa shuka yake, na kukaribia kumwua.

Iko siku Ibn Al-Khattab alikuwa ametoka na upanga kwa madhumuni ya kwenda kummaliza mtoto wa ndugu yake. Abu Twalib alikuwa akiyazingatia matukio yote haya. Kila alipohisi hisia za shari moyo wake ulitetemeka sana, hasa ukizingatia kuwa kulikuwa na fumunu kuwa Mushirikina walikuwa wanafikiria kuvunja ahadi waliyowekeana ya kutomdhuru mtoto wa ndugu yake na kuwa wanapanga kumwua.

Yeye alikuwa anawaza kuwa Hamza au Umar peke yao, au wasiokuwa hao hawatoshi kumlinda mtoto wa ndugu yake, iwapo mmoja miongoni mwa Washirikina atafanya mashambulizi dhidi ya Mtume (). Jambo hili lilikuwa na nguvu kwa Abu ‘Twalib na haikuwa isipokuwa ni kweli tupu, kwani Mushirikina walikuwa tayari wamekwisha kubaliana kumwua Mtume wa Mwenyezi Mungu () bila ya kificho, na makubaliano hayo yaliletwa kama ishara katika kauli yake Mwenyezi Mungu ().

أَمۡ أَبۡرَمُوٓاْ أَمۡرٗا فَإِنَّا مُبۡرِمُونَ

” Ndiyo wameweza (wabaya hao) “kupitisha amri (yao) au sisi ndio wapitishuji (wa kila tunalolitaka)? (Bali sisi ndio wapitishao tunayoyataka) (43:79)

Abu Twalib alikuwa akijiuliza atafanya nini iwapo mambo yatakuwa ndiyo hayo? Kwa hakika, alipoona Makuraishi wanakusanyika dhidi ya mtoto wa ndugu yake, aliamua kuwategemea zaidi watu wa nymnbani kwake, miongoni mwa Banu’Hashim na Banu Al-Mutwah’b, watoto wa Abdi Manafi na akawashirikisha katika lile ambalo yeye alikuwa tayari amekwisha kuliazimia, katika kumlinda mtoto wa ndugu yake na kusimama nyuma yake. Waliomwifikia kwenye hilo ni pamoja na Waislamu, miongoni mwa Williokuwa makafiri kwa sababu ya ari na Ujirani wa Kiarabu, isipokuwa ndugu yake .Abu Lahb, yeye alijitenga nao, na ikaunugana pamoja na Makuraishi katika njama zao. (1)*


1) Ibnu Hishaam Juzaa 1, Uk 269. Mukhtasar Siratu Rasul Uk. 106
2) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 189-191

Begin typing your search above and press return to search.