0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

USUSIAJI WA KIJAMII KWA UJUMLA


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Katika kipindi Cha majuma manne yalitokea matukio makubwa manne upande wa Mushirikina. Kwanza, katika muda huo mchache alisilimu Hamza; Pili, akasilimu Umar; Tatu, Mtume () alikataa makubaliano nao; Nne, mkataba wa pamoja baina ya Banu Al-Mutwalib na Banu Hashim wa kumlinda na kumhami Mtume (ﷺ). Mambo yote haya yaliwachanganya Mushirikina na walifahamu kuwa lau wakiamua kumwua Mtume () basi Makka nzima ingemwagika damu na huenda kwa hilo wangemalizika. Kwa utambuzi huo wa mambo wakabadilisha mikak’ati yao na kuelekea kwenye dhulma ya chini zaidi kuliko kuua.

AHADI YA DHULMA NA UADUI

Katika kuendeleza njama zao dhidi ya Mtume () Makuraishi walikusanyika katika sehemu iitwayo Wadi AI- Muhassab sehemu iliyokuwa chini ya milki ya Banu Kinana Khaifu ya Banu Kinana (Khaifu-ni sehemu ambayo imeporomoka katika kitako cha jabali kisha ikanyanyuka na kuwa mbali ya mapito ya maji katika jangwa la Al-Muhassab). Hapo walipeana kiapo cha kusaidiana dhidi ya Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib kuwa: Wasioleane nao, wasifanye biashara nao, wasichanganyikane nao, na wasiseme nao mpaka watakapo mkabidhi kwao Mtume wa Mwenyezi Mungu () kwa ajili ya kumwua; Makubaliano hayo yaliandikwa katika waraka ambao ndani yake waliweka mkataba huo wa ahadi_ wadhulma na uadui, ambamo miongoni mwa masharti yake yalikuwa ni: Wasikubali kutoka kwa Banu Hashim suluhu ya aina yoyote milele, na wasiwe na huruma yoyote na watu wa kabila la Banu Hashim mpaka hapo watakapomkabidhi Mtume (ﷺ) kwao ili wamuue.

Ibnul Qayyim, anasema, inasemekana kibao cha waraka huo kiliandikwa na Mansour bin Ikrima bin Amir bin Hashim bin al-Harith, lakini kwa usahihi zaidi ni Baghiidh bin Amir bin Hashim, ambaye Mtumc (ﷺ) alimuapiza na hivyo kupooza mkono wake.

Baada ya mkataba huo kukamilika, kibao kilitundikwa ndani ya Al-Ka’aba, Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib wakatengwa wote, wakiwemo Waislamu na makafiri katika koo hizo, isipokuwa Abu-Lahb, wakazuiwa katika bonde la Abu Twalib, mwanzo mwa mwezi Muharram, Mwaka wa saba mpaka wa kumi toka kupewa utume, yaani kipindi cha miaka Mitatu.


1) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 192-193

Begin typing your search above and press return to search.