BUSTANI YA WATU WEMA
عن أَبِي هريرة رضي اللَّهعنه أن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: « بَيْنمَا رَجُلٌ يَمْشِي بطَريقٍ اشْتَدَّ علَيْهِ الْعَطشُ ، فَوجد بِئراً فَنزَلَ فيها فَشَربَ ، ثُمَّ خرج فإِذا كلْبٌ يلهثُ يَأْكُلُ الثَّرَى مِنَ الْعَطَشِ ، فقال الرَّجُلُ : لَقَدْ بلَغَ هَذَا الْكَلْبُ مِنَ العطشِ مِثْلَ الَّذِي كَانَ قَدْ بَلَغَ مِنِّي ، فَنَزَلَ الْبِئْرَ فَملأَ خُفَّه مَاءً ثُمَّ أَمْسَكَه بِفيهِ ، حتَّى رقِيَ فَسَقَى الْكَلْبَ ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَه فَغَفَرَ لَه. قَالُوا: يا رسولَ اللَّه إِنَّ لَنَا في الْبَهَائِم أَجْراً ؟ فَقَالَ: « في كُلِّ كَبِدٍ رَطْبةٍ أَجْرٌ » متفقٌ عليه
وفي رواية للبخاري : « فَشَكَر اللَّه لهُ فَغَفَرَ لَه ، فَأدْخَلَه الْجنَّةَ
وفي رواية لَهُما : « بَيْنَما كَلْبٌ يُطيف بِركِيَّةٍ قَدْ كَادَ يقْتُلُه الْعطَشُ إِذْ رأتْه بغِيٌّ مِنْ بَغَايا بَنِي إِسْرَائيلَ ، فَنَزَعَتْ مُوقَهَا فاسْتَقت لَهُ بِهِ ، فَسَقَتْهُ فَغُفِر لَهَا بِهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake amepokea kutoka kwa Mtume ﷺ Amesema: [Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitembea njiani, akashikwa na kiu, akaona kisima. Akateremka ndani na akanywa maji, kisha akatoka, mara akamuona mbwa ana hema anakula mchanga kwa sababu ya kiu. Yule mtu akasema: Mbwa huyu amepatwa na kiu kama kile kilichonipata. Akateremka kisimani, akaijaza maji khufu yake halafu akaizuia kwenye mdomo wake, akapanda hata akafika juu, akamnywesha mbwa yule. Mwenyezi Mungu Akamlipa na Akamghufuria.] Maswahaba wakauliza: Kwani sisi tuna ujira katika Wanyama? Akawajibu: [Kunywesha kila kilicho hai ni sadaka.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Na katika Riwaya ya Bukhari: [Mwenyezi Mungu Akamlipa na Akamghufuria na akamuingiza Peponi]
Na katika Riwaya nyingine ya Bukaari na Muslim : [Mbwa aliokuwa akizunguka kando ya kisima, alikaribia kufa kwa kiu, mara mwanamke wa kikahaba katika wana wa Israiyl akamuona akaivua khuffu yake, akachotea maji na akamnywesha, akasamehewa kwa kitendo hicho.]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله