BUSTANI YA WATU WEMA
– وعنْ أَنسٍ رضِيَ الله عنْهُ قَالَ : لمَّا ثقُلَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم جَعَلَ يتغشَّاهُ الكرْبُ فقَالتْ فاطِمَةُ رَضِيَ الله عنْهَا : واكَرْبَ أبَتَاهُ ، فَقَالَ : « ليْسَ عَلَى أبيك كرْبٌ بعْدَ اليَوْمِ » فلمَّا مَاتَ قالَتْ : يَا أبتَاهُ أَجَابَ ربّاً دعَاهُ ، يا أبتَاهُ جنَّةُ الفِرْدَوْسِ مأوَاهُ ، يَا أَبَتَاهُ إِلَى جبْريلَ نْنعَاهُ ، فلَمَّا دُفنَ قالتْ فاطِمَةُ رَضِيَ الله عَنهَا : أطَابتْ أنفسُكُمْ أَنْ تَحْثُوا عَلَى رسُول الله صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم التُّرابَ ؟ روَاهُ البُخاريُّ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Kutoka kwa Anas bin Maalik Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume ﷺ: alipozidiwa Mtume ﷺ na uchungu wa Mauti akawa anapata shida (kwa sababu ya uchungu), Faatimah Radhi za Allah ziwe juu yake akasema: “Ee uchungu gani unaomshika baba yangu.” Mtume ﷺ akasema: [Hatopata tena shida Baba yako baada ya leo.] Alipofariki (Mtume ﷺ) Faatimah Radhi za Allah ziwe juu yake akasema: “Ewe baba yangu ameitika wito wa Mola wako! Ewe baba yangu Jannah ya Al-Firdaws ndio mashukio yako. Ewe baba yangu! Kwa Jibril tunamuombeleza!” Na Alipozikwa, Fatwima alisema: [Nyoyo zenu zimeridhika kwa kumiminia mchanga Mtume wa Mwneyezi Mungu ﷺ?] [Imepokewa na Bukhari]