SOMO LA FIQHI
ADABU YA KUZURU MSIKITI WA MTUME ﷺ
1. Mwenye kuzuru afikapo msikitini ni sunna kwake atangulize mguu wake wa kulia na aseme:
[اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ] رواه مسلم
[Ewe Mola! Nifungulie milango ya rehema zako] [Imepokewa na Muslim.].
2. Ataswali rakaa mbili za kuuamkia msikiti, na ikiwa ataziswali kwenye sehemu ya Raudha (Bustani ya Pepo) basi ni bora zaidi.
3. Ni sunna kuizuru kaburi ya Mtume ﷺ na marafiki zake wawili: Abu Bakr kisha ‘Umar.
4. Ni sunna kwa mwenye kuuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ aswali Swala Tano ndani ya Msikiti wa Mtume, na amtaje Mwenyezi Mungu na kumuomba kwa wingi na kuswali sunna ya ziada hasa-hasa kwenye sehemu ya Raudha tukufu.
5. Ni sunna azuru msikiti wa Baqii’ kwa ajili ya kuswali humo, ingawa kuuzuru siku ya Jumamosi ni bora zaidi, kwa Hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:
[كَانَ رَسُولُ اللهِ ﷺ يَأْتِي مَسْجِدَ قُبَاءٍ رَاكِبًا وَمَاشِيًا فَيُصَلِّى فِيهِ رَكْعَتَيْنِ» وفي لفظ: «كَانَ يَأْتِي قُبَاءً» يَعْنِي كُلَّ سَبْتٍ] رواه مسلم
[Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akienda kwenye msikiti wa Qubaa’ akiwa anapanda na akiwa anatembea, na akiswali hapo rakaa mbili]. Na katika tamshi lingine: (Alikuwa akiujia msikiti wa Qubaa, yaani: siku ya Jumamosi] [Imepokewa na Muslim.].
6. Ni sunna kuzuru makaburi ya Baqii’ [ Baqii’: ni mahali ambapo Mswahaba wengi walizikwa hapo.], makaburi ya mashahidi na kaburi ya Hamza, kwa kuwa Mtume ﷺ alikuwa akiwazuru na kuwaombea na kusema:
[السلام عليكم أهلَ الديار من المؤمنين والمسلمين، وإنا إن شاء الله بكم لَلَاحقون، أسأل الله لنا ولكم العافية] رواه مسلم
[Amani iwashukie nyinyi watu wa nyumba za Waumini na Waislamu. Na sisi, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni wenye kukutana na nyinyi. Tunajiombea Mwenyezi Mungu uzima na tunawaombea na nyinyi] [Imepokewa na Muslim.].