June 22, 2021
0 Comments
SOMO LA FIQHI
Maelekezo
1. Ni juu ya Muislamu kutoingia kwenye zahma pamoja na wenye kutufu ili asijitie kwenye tabu yeye na kuwatia wenzake, katika kutaka kulisalimia jiwe jeusi ama kulibusu, na vilevile hata fanya raml kufanya haraka katika kuzunguka alkaba ikiwa atawaudhi wenye kufanya twafu.
2. Ataomba kwenye Twawafu kwa atakavo weza, na Twawafu haina Dua maluum isipokuwa yale yalio tanguliya, na lau atasoma Qur’ani katika Twawafu yake hakuna ubaya wowote kufanya hivyo.
3. Kufanya idhtibaa (kufungua bega) ni sunna katika Twawafu ya Umrah au Twawafu ya Quduum katika mizungu yote.
4. Na mwanamke ajiepushe kudhihirisha mapambo katika Twawafu yake na kujipaka manukato, na kuinuwa sauti katika kuleta dhikri na dua