SOMO LA FIQHI
KISIMAMO CHA IMAMU NA MAAMUMA KATIKA SWALA
1. Maamuma akiwa mmoja: Sunna ni asimame upande wa kulia wa imamu akiwa amekaribiana naye, kwa hadithi iliyopokewa na Ibnu ‘Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:
صليت مع النبي صلى الله عليه وسلم ذات ليلة فقمت عن يساره، فأخذ رسول الله صلى الله عليه وسلم، برأسي من ورائي فجعلني عن يمينه
[Niliswali pamoja na mtume ﷺ usiku mmoja nikasimama upande wake wa kushoto, na Mtume akashika kichwa changu kwa nyuma yangu akaniweka upande wake wa kulia] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
2. Jamaa iwapo ni ya watu wawili na zaidi: Imamu husimama mbele yao kati ya safu, kwa hadithi iliyopokewa na Jabir na Jabaar Radhi za Allah ziwe juu yao kwamba mmoja wao alisimama upande wa kulia wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ na mwingine upande wake wa kushoto. Jabir alisema: [Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akatushika mikono yetu pamoja akatusukuma mpaka akatusimamisha nyuma yake] [Imepokewa na Muslim.].