0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUAMINI KADARI

KUAMINI KADARI

Ni lazima kwa kila Muislamu kuwa na itikadi ya kwamba kheri na shari ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na ujuzi wake na mapendeleo yake, lakini kufanya kheri na shari kwa mja ni kwa khiyari yake na uchungaji wa jambo na makatazo ni wajibu kwa mja haifai kumuasi yeye Mwenyezi Mungu kisha kusema Mungu amenikadiria.
Kuamini kadari ni nguzo moja katika nguzo sita za Imani, ambayo mwenye kukanusha nguzo hiyo Mwenyezi Mungu hamkubalii yeye na haitimu imani ya mtu ila kwa kuamini kadari. Nguzo hii ni kubwa, mwenye kuwa nayo hupata utulivu na kujibu masuali mengi na mwenye kulemewa nayo huwa hapati kitu.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala’:

{إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ}   القمر:49

[Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.]   [Al-Qamar:49].

Na Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ }      الأعلى:1-3

[Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa,Aliye umba, na akaweka sawa, Na ambaye amekadiria na akaongoa]    [Al-A’alaa : 1 – 3].

Na imethibiti katika hadithi sahihi ya kwamba Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam alikuwa na masahaba zake, akamjia Jibril kwa sura mtu katika watu akamuuliza kutokana na masuali ya Dini. Katika masuali hayo; akamuliza Imani ni nini? Mtume akamwambia:

[أن تؤمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر ، وتؤمن بالقدر خيره وشره]

[Imani ni kuamini Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume yake na Siku ya Mwisho na kuamini Kadari kheri yake na shari yake.]

Akasema Jibril: umesema kweli. Mwisho wa hadithi Mtume ﷺ Akawaambia waliokua naye: Je mnajua aliyekua akiuliza? Wakasema Mungu na Mtume wanajua zaidi, Akawaambia huyu ni Jibril amekuja kuwafundisha Dini yenu”]     [imepokewa na Muslim].
Hadithi hii ina Tufundisha kujua nguzo sita za imani na yaliyokusanyika katika nguzo hizo nayo ni dini
Ndugu Muislamu Kadari ni ilimu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu iliyotangulia vitu kabla ya kuandikwa, aliyo pambanuliwa kuwa yatakuwa. Hivyo basi ni kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi kwa miaka khamsini elfu. Na uhakika wa kuamini kadari una dhamini mambo manne:
1. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala ameumba kila kitu kwa kadari.
2. Kila kitu kimeandikwa kwenye (lawhul-mahfudh)
3. Ujuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kujua kila kitu.
4. Kila kitu kinakuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala.
Kwa hivyo, kuamini kadari ni kuamini ujuzi wa Mwenyezi Mungu Mtukuf wa kila kitu kabla ya kufanyika. Na halifanyiki jambo lolote nje ya ufalme wake. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) anayo ilimu ya kila kitu. Ni wajibu kwa kila Muislamu kuamini ya kuwa Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala ameandika makadario ya viumbe vyote katika ubao uliohifadhiwa kabla ya kuumba mbingu na ardhi kwa miaka Khamsini elfu kama ilivyothibiti katika Hadithi iliyo sahihi, na kama alivyotoa khabari Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala katika kitabu chake Kitukufu:

{أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ يَسِيرٌ}   الحج:70

[Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.]     [Al-hajj 70]
Kuamini kadari ni kuamini jambo lolote Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) akitaka linakua na mabalo halitaki liwe halitakua. Analolitaka liwe halina budi liwe na matakwa yote yako chini ya matakwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hamutaki jambo likawa ila atake Mwenyezi Mungu Mtukufu, wala hamuwezi katika jambo asipotaka Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), Yeye ni mjuzi Mwenye hekima.
Jua Ewe Muislamu ya kwamba, itikadi ya Jabriya haina mahala katika Uislamu. Na katika itikadi ya Muislamu; Mwanadamu ni mwenye kuchaguzwa na hakua ni mwenye kwenda kama upepo bali anachagua ima achague njia ya kheri au njia ya shari.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ}   البلد:10

[Na tukambainishia zote njia mbili? ]     [Al-balad:10].

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا }      الشمس:9-10

[Hakika amefanikiwa aliye itakasa, Na hakika amekhasiri aliye iviza.]    [ Ashamsu 9-10].

Na ilmu ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) iliyotangulia na maandishi yake hayakuwa ni yenye kuungwaungwa na katika hilo ni kwasababu ya kusimamisha hoja juu ya waja na halipatikani jambo lolote ila Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) analijua kwa ukamilifu wa ilmu yake.
Na kama tunavyo jua baadhi ya watu wanafanya maasi kisha wanategemezea kadari. Haifai kutegemezea kadari pindi unapo fanya makosa. Si sawa mwanadamu kuchukua hoja kwa kadari juu ya kufanya maasia. Na kuna mengi sana kuhusu kuamini kadari lakini tutakoma hapa. Mwenyezi Mungu atuafikie kila la kheri na atuepushe na kaila

 SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH HAMMAD QASIM

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.