0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUMPENDA MWENYEZI MUNGU (SUBHAANAHU WA TA’AALA)

KUMPENDA MWENYEZI MUNGU (SUBHAANAHU WA TA’AALA)

Ni nini mapenzi? Mapenzi ni jambo ambalo watu wana shindana katika kupenda kitu. Mapenzi huonyesha ukweli wa mwenye kupenda kitu. Na tukisema kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume ni vipi? Ni kufuata kila walilo amrisha na kuacha kila walilo kataza, kama ilivyo kuja katika Qur’an.Mwenyezi Mungu (Subhanahu wa T’aala) Aseama:

{وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۖ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ}    الحشر:7

[Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu]   [ Al-Hashri:7]
Ndugu Muislamu, mada kama hii ni muhimu kwa kila Muislamu na inahitajia kila mmoja wetu, bali kuhakikisha yanayolazimu imani, hakuna imani kwa yeyote ambae hatahakikisha hilo, nalo si lingine ni Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wetu ﷺ na kuwaweka mbele kuliko yoyote.
Hakika mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni katika imani. Hawi muumini yoyote ila atangulize mapenzi ya kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuliko chochote alichokimiliki mali, watoto, wazazi na watu wote. Kama alivyo toa khabari juu ya hilo Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّهُ بِأَمْرِهِ ۗ وَاللَّهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ

[Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.]   [ Tawab : 24]
Amesema Qaadhi ‘Iyadh Mungu Amuwee radhi Inatosha Aya hii kuwa ni tanabahisho na ni dalili kubwa na ni huja juu ya ulazima wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Na kuonyesha uwajibu wake na ni haki kumpenda Mtume ﷺ. Wakati Mwenyezi Mungu Alipotangaza yoyote atakaye kuwa mali yake, watoto wake, mke wake ni bora kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume, kisha akawaahidi adhabu kali, kwa kusema: “Ngojeni amri ya Mwenyezi Mungu ije.
Kisha Akakamilisha Aya kwa kuwaita maasi, na Mwenyezi Mungu hawaongozi mafasiki.
Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ}    آل عمران:31

[Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.]   [Al-Imran : 31]

Amesema tena Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ}    الحجرات:1

[Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.]   [Al-Hujrat : 1]
Na kama ilivyo kuja katika Hadith. Imepokelewa na Anas (R.A.) Akisema: Amesema Mtume ﷺ:

[لا يؤمن أحدكم حتى أكون أحبَّ إليه من ولده ووالده والناس أجمعين]     رواه البخاري ومسلم

[Hawi na imani mmoja wenu mpaka anipende zaidi mimi kuliko mzazi wake na mtoto wake na watu wote]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Amepokea Anas kutoka kwa Mtume ﷺ akisema:

ثلاثٌ من كن فيه وجد بهن حلاوة الإيمان، من كان الله ورسوله أحبَّ إليه مما سواهما، وأن يحب المرء لا يحبه إلا لله، وأن يكره أن يعود في الكفر بعد أن أنقذه الله منه، كما يكره أن يقذف في النار     رواه البخاري ومسلم

[Mambo matatu ukiwa nayo unapata utamu wa imani; Ni kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake zaidi kuliko wengine. Na asimpende mtu ila kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na achukie kurudi katika ukafiri kama anavyo chukia kuingia motoni]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake yanao alama za kujulisha mapenzi yao. Wamezitaja na wakazibainisha Wanachuoni, zimetolewa katika Qur›an na sunnah na miongoni wa alama hizo:

ALAMA ZA KUJULISHA MAPENZI KWA MTUME ﷺ

1. Ni kufuata Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).

2. Ni kutekeleza Sunnah zake zote, kwa kumfuata Mtume na kufanya sunnah zake na kufuata maneno yake na vitendo vyake.

3. Na kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake na kujipamba kwa adabu za Mtume katika uzito na wapesi. Amesema Qaadhi Iyadh:R.A ‘Mwenye kupenda jambo huathirika na huathirika kwa kuliafiki. Asipokuwa hivyo, huwa si mkweli katika mapenzi yake.

Kuathirika na aliyoweka Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mapenzi ya nafsi na kufuata matamanio.

KWA FAIDA ZAIDI SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH YUSUF ABDI

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.