JE WATAKA KUWA MUISLAMU
Ndugu mpendwa hakuna mpingamizi zozote za mtuku kuwa Muislamu,hakuna pesa mtu analipa au labda kujaza fomu,au kwenda kwa sheikh na kutoa Ada Fulani. Kusilimu ni rahisi sana tena sena sivyo kama vile wengi wanavyo fikiria.
VIPI MTU ANAKUWA MUISLAMU?
Mtu kuwa muislamu ni kuamini na kuitakidi itikadi sahihi ya kumuabudu Mungu mmoja pake yake, bila ya kumshrikisha na kitu chochote kile.Na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hafanani na kitu chochote, na kumuamini kuwa Nabii Muhammad ni Mtume wa Mungu kama vile Manabii walio Mtangulia.
Na Imani hii ni lazima kukubali ndani ya Moyo wako na kuitamka kwa Ulimi wako nao ni kusema maneno yafauatayo:
Sikiliza Shahada ya Kusilimu |
ASH’HADU ANLAA ILAHA ILLA ALLAH,WA’ASH’HADU ANNA MUHAMMAD RASULULLAH
MAANA YA MANENO HAYA
Nakiri kwa Moyo na kutemka kwa ulimi ya kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwneyezi Mungu mmoja,na nakiri kwa Moyo na kutemka kwa ulimi ya kuwa Mtume Muhammad Rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume wa Mungu.
Ukisha kuamini na kuitakidi itikadi hii basi huwa ushakuwa Muislamu,na kulazimika kufanya na kutenda yaliolazimishwa na Uislamu .
Ndugu mpendwa fanya haraka ujiunge na Dini ya haki, Dini ya Manabii wote,na Dini inayotambulika Mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama Mwenyezi Mungu anasema:
[Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu]Â Â Â [2:19]
Na amesema tena:
[Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.]Â [2:85]
Ikiwa umeona haki na wataka kusilimu popote pale ulipo basi wasiliana nasi
Baruwa pepe [email protected]
Au tutumi ujumbe mfupi kwa Whatsapp nambari hii
+966569618011
Inshallah tutakufatia mwalimu atakae kufunza dini yako,bora utujulishe nchi yako na mji unaokaa.
Mungu akubariki na akuonyeshe njia ya uongofu nji ya haki.