0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

708. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Sunnah Ya Kutoa Bishara Njema Na Kupongeza Kheri

باب استحباب التبشير والتهنئة بالخير


وعن أَبي موسى الأشعري – رضي الله عنه -: أَنَّهُ تَوَضَّأ في بَيْتِهِ، ثُمَّ خَرَجَ، فَقَالَ: لأَلْزَمَنَّ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، وَلأَكُونَنَّ مَعَهُ يَوْمِي هَذَا، فَجَاءَ الْمَسْجِدَ، فَسَألَ عَنِ النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم -، فَقَالُوا وجَّهَ هاهُنَا، قَالَ: فَخَرَجْتُ عَلَى أثَرِهِ أسْألُ عَنْهُ، حَتَّى دَخَلَ بِئْرَ أريسٍ، فَجَلَسْتُ عِندَ البَابِ حتَّى قضى رسول الله – صلى الله عليه وسلم – حاجتهُ وتوضأ، فقمتُ إليهِ، فإذا هو قد جلسَ على بئرِ أريسٍ وتوَسَّطَ قُفَّهَا، وكشَفَ عنْ ساقيهِ ودلاّهُما في البئرِ، فسلمتُ عَليهِ ثمَّ انصَرَفتُ، فجلستُ عِندَ البابِ، فَقُلْتُ: لأَكُونَنَّ بَوَّابَ رسولِ اللهِ – صلى الله عليه وسلم – الْيَوْمَ، فَجَاءَ أَبُو بَكْرٍ – رضي الله عنه – فَدَفَعَ الْبَابَ، فقلتُ: مَنْ هَذَا؟ فَقَالَ: أَبُو بَكْرٍ، فقُلتُ: عَلَى رِسْلِكَ، ثُمَّ ذَهبْتُ، فقلتُ: يَا رسول الله، هَذَا أَبُو بَكْرٍ يَستَأْذِنُ، فَقَالَ: {ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بِالْجَنَّةِ} فَأقْبَلْتُ حَتَّى قُلْتُ لأَبي بَكْرٍ: ادْخُلْ وَرسول الله – صلى الله عليه وسلم – يُبَشِّرُكَ بِالجَنَّةِ، فَدَخَلَ أَبُو بَكرٍ حَتَّى جَلَسَ عَنْ يَمينِ النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم – مَعَهُ في القُفِّ، وَدَلَّى رِجْلَيْهِ في البِئْرِ كَمَا صَنَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، وَكَشَفَ عَنْ سَاقَيْهِ، ثُمَّ رَجَعْتُ وَجَلَسْتُ، وَقَدْ تَرَكْتُ أخِي يَتَوَضَّأ وَيَلْحَقُنِي، فقلتُ: إنْ يُرِدِ الله بِفُلانٍ – يُريدُ أخَاهُ – خَيْراً يَأتِ بِهِ. فَإذَا إنْسَانٌ يُحَرِّكُ الْبَاب، فقلتُ: مَنْ هَذَا؟ فَقَالَ: عُمَرُ بن الخَطّابِ، فقلتُ: عَلَى رِسْلِكَ، ثُمَّ جِئْتُ إِلَى رسول الله – صلى الله عليه وسلم -، فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ وَقُلْتُ: هَذَا عُمَرُ يَسْتَأذِنُ؟ فَقَالَ: {ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بالجَنَّةِ} فَجِئْتُ عُمَرَ، فقلتُ: أَذِنَ وَيُبَشِّرُكَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – بِالجَنَّةِ، فَدَخَلَ فَجَلَسَ مَعَ رسول الله – صلى الله عليه وسلم – في القُفِّ عَنْ يَسَارِهِ وَدَلَّى رِجْلَيْهِ في البِئرِ، ثُمَّ رَجَعْتُ فَجَلَسْتُ، فَقُلتُ: إنْ يُرِدِ اللهُ بِفُلاَنٍ خَيْراً – يَعْنِي أخَاهُ – يَأْتِ بِهِ، فَجَاءَ إنْسَانٌ فَحَرَّكَ الْبَابَ. فَقُلتُ: مَنْ هَذَا؟ فَقَالَ: عُثْمَانُ بن عَفَّانَ. فقلتُ: عَلَى رِسْلِكَ، وجِئْتُ النَّبيَّ – صلى الله عليه وسلم – فأخْبَرْتُهُ، فقالَ: {ائْذَنْ لَهُ وَبَشِّرْهُ بِالجَنَّةِ مَعَ بَلْوَى تُصِيبُهُ} فَجِئْتُ، فقلتُ: ادْخُلْ وَيُبَشِّرُكَ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بِالجَنَّةِ مَعَ بَلْوَى تُصيبُكَ، فَدَخَلَ فَوجَدَ الْقُفَّ قَدْ مُلِئَ، فجلس وِجَاهَهُمْ مِنَ الشِّقِّ الآخرِ. قَالَ سَعيدُ بْنُ الْمُسَيَّبِ: فَأوَّلْتُهَا قُبُورَهُمْ.     متفقٌ عَلَيْهِ

وزاد في رواية: وأمرني رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم – بحفظِ الباب. وَفيها: أنَّ عُثْمانَ حِيْنَ بَشَّرَهُ حَمِدَ اللهَ تَعَالَى، ثُمَّ قَالَ: اللهُ المُسْتَعانُ


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa na Abû Mûsâ al-Ash‘ary (Radhi za Allah ziwe juu yake) alitawadha nyumbani mwake, kisha akatoka, akasema: “Leo mchana wote nitakuwa pamoja na Mtume (ﷺ).” Akaenda Msikitini, akamwulizia Mtume (ﷺ) , Maswahaba wakamwambia: “Ameelekea huku.” Anaeleza: “Nikatoka nyuma yake nikimwulizia. Akawa ameingia katika bustani lenye kisima cha Arîsi. Nikaketi mlangoni hata Mtume (ﷺ) akamaliza haja yake na akatawadha, nikamwendea, akawa ameketi katika ukingo wa kisima cha Arîsi, ameifunua miundi yake na miguu yake ameining’iniza katika kisima. Nikamsalimia kisha nikaondoka. Nikaketi mlangoni, nikasema: “Leo nitakuwa bawabu (mlinzi) wa Mtume (ﷺ) .” Akaja Abûbakar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akabisha mlango. Nikauliza: “Ni nani?” Akajibu: “Abûbakar.” Nikamwambia: “Subiri.” Nikamwendea Mtume (Radhi za Allah ziwe juu yake) nikamwambia: “Yâ Rasûlallâh, Abûbakar anaomba ruhusa (ya kuingia).” Akasema: “Mruhusu na umbashirie Pepo.” Nikamwendea Abûbakar nikamwambia: “Ingia, na Mtume (ﷺ) yuwakubashiria Pepo.” Abûbakar akaingia, akaketi kuliani mwa Mtume (ﷺ) pamoja naye katika ukingo, akaining’iniza miguu yake katika kisima kama alivyofanya Mtume (ﷺ) , na akaifunua miundi yake. Nikarudi nikaketi. Nilikuwa nimemwacha ndugu yangu akitawadha na akitaka kunifwata, nikasema (moyoni): Allâh Akimtakia kheri fulani (Ndugu yangu) Atamleta. Mara akaja mtu anautingisa mlango, nikauliza: “Ni nani?” Akajibu: “Ni ‘Umar bin al-Khattâb. Nikamwambia: “Subiri.” Nikamwendea Mtume (ﷺ) nikamtolea salamu na nikamwambia: “‘Umar anaomba ruhusa.” Akaniambia: “Mruhusu na umbashirie Pepo.” Nikamwendea ‘Umar, nikamwambia: “Amekuruhusu na Mtume (ﷺ) anakubashiria Pepo.” Akaingia na akaketi pamoja na Mtume (ﷺ) kushotoni mwake katika ukingo, akaining’iniza miguu yake kisimani. Nikarudi nikaketi. Nikasema: Allâh Akimtakia kheri fulani (Ndugu yangu) Atamleta. Akaja mtu anautingisa mlango, nikauliza: “Ni nani?” Akajibu: “Ni ‘Uthmân bin ‘Affân.” Nikamwambia: “Subiri.” Nikamwendea Mtume (ﷺ) , nikamweleza. Akaniambia: “Mruhusu na umbashirie Pepo pamoja na balaa itakayompata.” Nikaenda nikamwambia: “Ingia, Mtume (ﷺ) anakubashiria Pepo pamoja na balaa itakayokupata.” Akaingia, akakuta ukingo umejaa, akaketi mkabala wao upande mwingine.” Sa‘îd bin al-Musayyib amesema: “Nikafasiri makaburi yao yatakuwa ni kama walivyoketi.”  [ Wameafikiana Bukhari na Muslim] 

Riwaya nyingine imeongezwa: “Mtume (ﷺ) akaniamuru nichunge mlango.” Pia ikaeleza: “Uthmân alipobashiriwa, alimhimidi Allâh na akasema: “Allâh Ndiye Mwenye kuombwa msaada.”

Begin typing your search above and press return to search.