باب النهي عن تولية الإمارة والقضاء وغيرهما من الولايات لمن سألها أَوْ حرص عليها فعرَّض بها
عن أَبي موسى الأشعريِّ – رضي الله عنه -، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى النَّبيِّ – صلى الله عليه وسلم – أنَا وَرَجُلانِ مِنْ بَنِي عَمِّي، فَقَالَ أحَدُهُمَا: يَا رسول الله، أمِّرْنَا عَلَى بَعْض مَا ولاَّكَ اللهُ – عز وجل -، وقال الآخَرُ مِثلَ ذَلِكَ، فَقَالَ: { إنَّا وَاللهِ لاَ نُوَلِّي هَذَا العَمَلَ أحَداً سَألَهُ، أَوْ أحَداً حَرَصَ عَلَيْهِ} متفقٌ عَلَيْهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
83. MLANGO WA MAKATAZO YA KUSIMAMIA UONGOZI, HUKUMU NA MENGINEYO KATIKA MAMBO YA UTAWALA KWA ALIYEUOMBA AU AKAUFANYIA TAMAA KWA KUDOKEZEA
Imepokewa na Abû Mûsâ al-Ash‘ary (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mimi na watu wawili ambao ni binamu zangu, tulimwendea Mtume (ﷺ) , mmoja wao akamwambia: “Yâ Rasûlallâh, tufanye viongozi katika nchi uliyotawalishwa na Allâh.” Na yule mwengine akasema vivyo hivyo. Mtume (ﷺ) akawaambia: “Wallahi, sisi hatumtawalishi yeyote aliyeuomba (utawala) au aliyeufanyia tamaa.” [ Wameafikiana Bukhari na Muslim ].