0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

WAUMINI NJE YA MAKKAH


AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Kama Mjumbe’ wa Mwenyezi Mungu () alivyoutangaza Uislamu kwa makabila na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wakifika Makka, wakati wa msimu, aliutangaza pia Uislamu kwa watu binafsi, kutoka kwa baadhi yao yalipatikana majibu mazuri na kwa kipindi kifupi tu baada ya msimu kupita walimuamini watu wengi. Mfano wao:-

1. Suwaid bin Swamit, alikuwa ni mshairi mwerevu miongoni mwa wakazi kwa Yathrib (Madina). Jamaa zake walikuwa wakimwita kwa jina la Al-Kamil (mkamilifu) kutokana na ukakamavu aliokuwa nao, uzuri wa mashairi yake na ubora wa ukoo wake. Alikuwa amekwenda Makka kwa lengo la kufanya ibaada kama Ilivyokuwa ada ya Waarabu wakati ule.- Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akamlingania kuingia katika Uislamu, akasema; “Huenda yale uliyonayo ni sawa na yale niliyonayo”, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akamwuliza, “Ni jambo gani hilo kubwa ulilonalo?.” Akajibiwa; ”Hekima ya Luqman”, Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akamueleza, ”Kwa hakika maneno yako ni mazuri, lakini yale niliyonayo mimi ni bora zaidi kuliko yako – niliyonayo mimi ni Qur’an ambayo imeteremshwa na Allah (ﷻ) kwangu, ambayo ni Muongozo na Nuru.” Mtume (ﷺ) akamsomea Qur’an na alimweleza kuwa yale ni maneno mazuri na akamlingania afuate Uislamu na alipofika Madina akasilimu. Baada ya hapo hakuishi muda mrefu, aliuawa siku ya Buathi?” katika Uislamu mwanzoni mwa mwaka wa kumi na moja wa Utume.  (1)

2. Iyas bin Muadh alikuwa Kijana mdogo miongoni mwa wakazi wa Yathrib, alikwenda Makka akiwa kafika ujumbe wa Al-Awsi, wakitafuta makubaliano na Makuraishi dhidi ya jamaa zao katika Khazraji. Hilo liljkuwa ni’ nyuma kidogo kabla ya vita vya Buathi mwanzoni mwa mwaka wa Kumi na Moja wa Utume. Wakati huo hali ya uadui kati ya makabila mawili ulikuwa umezidi, na Al-Awsi walikuwa ni wachache kuliko Al-Khazraji; Mtume wa Allah (ﷺ) alipojua kufika kwao aliwafuata na kukaa nao, aliwauliza kama walikuwa tayari kuingizwa katika jambo ambalo ni bora zaidi kuliko lile ambalo lilikuwa limewaleta. Wakajibu kwa kuuliza swali; ‘Ni lipi jambo hilo?.” Mtume (ﷺ) akawaeleza, “Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu niliyetumwa kwa watu wote, ninawalingania wamuabudu Mwenyezi Mungu (s.w.t) na wasimshiriklkhe na kitu chochote. Na Ameniteremshia kitabu.” Baada ya maelezo hayo akawatajia Uislamu na akawasomea Qur’an. Baada ya kuisikiljza Qur’an Iyasi bin Muadhi alisema kuwaambia wenzake; ”Enyi jamaa zangu, ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu jambo hili ni bora zaidi kuliko lile ambalo limewaleta hapa.

Abu Al-Haisar Anas bin Rafii, mtu aliyekuwa mmoja. kati ya watu waliokuwa katika ule ujumbe, alichukua gao la mchanga wa changarawe nyembamba na kulimwaga usoni mwa Iyasi, na kusema; ”Achana nasi, ninaapa kwa Mungu wangu, kwa hakika tumekuja kwa jambo jingine na wala si hili.” Iyasi akanyamaza. Mtumé wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) hakuendelea kutoa maelezo yoyote. Walisimama na wakaondoka kuelekea Madina bila ya kufanikiwa kuuvunja ule mkataba na Makuraishi.

Baada ya kurejea kwao Yathrib, Iyasi hakuishi kwa muda mrefu akafariki dunia. Wakafi wote karibu na kifo chake alikuwa akitamka Tahalili na Takbira na alikuwa akimhimidi Allah (s.w.t) na Kumtakasa. Watu hawana shaka kuwa yeye alikufa akiwa Muislamu? (3)

3. Abu Dharr al-Ghifari: Yeye alikuwa ni miongoni mwa wakazi wa pande za Yathrib. Khabari za Utume wa Mtume Muhammad (ﷺ) zilimfikia kupitia kwa Suwaidi bin Swamiti na Iyasi bin Muadh. Hiyo ndiyo ikawa sababu kusilimu kwake.

Bukhari alipokea kutoka kwa Ibn Abbas (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa; ”Amesema Abu Dharr, mimi ni mtu miongoni mwa watu wa kabila la Ghafar, ilitufikia khabari kuwa huko Makka yupo mtu anadai kuwa yeye ni Mtume, nikamwambia ndugu yangu nenda kwa mtu huyo, na ukazungumze naye kisha uniletee khabari zake.” Alikwenda akakutana naye kisha akarudi. ”Nikamwuliza una khabari gani?.” Akanijibu, “Ninaapa kwa Iina la Mungu, nimemuona mtu anayeamrisha kheri na kukataza shari.” Nikamwambia, ”Hujanitosha kwa khabari hiyo. Nikachukua kiriba changu cha maji na fimbo yangu, kisha nikafunga safari kuelekea Makka. Simjui huyo anaedai Utume wala sikutaka kumwuliza mtu. Nilifika katika Kisima cha Zamzam nikanywa maji yake, kisha nikaelekea Akanipita Ali na akaniambia, ”Ninakuona kama u mtu mgeni?’ Nikamjibu, ‘Ndiyo.’ Akaniambia; ’Twende nyumbani.’ ’Nikaondoka pamoja naye, njiani hakuniuliza kuhusu jambo lolote, na wala sikumwuliza wala kumueleza jambo lolote.’ Nilipopambazukiwa nilikwenda ili nimwulizie, na hapakuwepo na mtu yeyote ambaye angeweza kunielezea chochote kuhusu hilo.’ Alisema alinipitia Ali akaniuliza; ’Hivi bado hujajua tu mahala pa kwenda?.’ Nikamjibu, ’Hapana.’ Akaniambia, ’Twende pamoja na mimi’; Akaniuliza, ‘Una jambo gani? Nini lililokuleta katika mji huu?.’ Nikamweleza, ‘Kama upo tayari kutunza siri yangu nitakueleza’; Naye akajibu, ‘Mimi nitafanya hivyo Nikamwambia, ‘Zimetufikia khabari kuwa ametokea mtu hapa anayedai kuwa’ yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, nilimtuma ndugu yangu akaseme naye, amerejea lakini ameshindwa kunitosheleza kwa khabari zake nikaona bora nikutane naye. Ninataka kukutana naye mwenyewe binafsi.’ Akaniambia; ’Ama kwa hakika umekwisha ongoka, huu uelekeo wangu naelekea kwake, ingia kila mahali nitakapoingia na nitakapomwona mtu ambaye nina wasiwasi naye juu yako, nitajifanya kusimama ukutani kana kwamba ninatengeneza viatu vyangu. Ukiona hivyo endelea tu.’ Akaenda nami mpaka tulipoingia kwa Mtume (ﷺ) nikamwambia, ’Nieleze kuhusu Uislamu, akanieleza na nikasilimu pale pale.’

Ndipo aliponiambia, “Ewe Abu Dharr, lifiche jambo hili na rejea mjini kwako, zitakapokufikia khabari za ushindi wetu, njoo.” Nikasema: ”Naapa kwa yule ambaye amekuleta kwa haki, nitalitangaza tamko hili mbele zao.” Nikarudi na niliwakuta Makuraishi wamo ndani yake, nikasema; ”Enyi Makuraishi, hakika mimi ninashuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (s.w.t.) na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) na Mja Wake.” Wakasema; ”Simameni, mshughulikieni huyu ambaye ametoka katika dini yetu.” Wakanijia na kunishambulia karibu waniue, Al-Abbasi akaniwahi na kunikinga. Kisha akawaelekea na kuwaambia; ”Hivi mnathubutu kweli kumwua mtu wa ukoo wa Ghifari? na hali ya kuwa mahali penu pa kufanyia biashara na njia yenu ya kupita ni kwao? Muacheni.” Nilipoamka asubuhi nilirejea na nikasema maneno mfano wa yale ambayo niliyasema jana, wakaambizana tena muendeeni huyo aliyeacha dini yetu, nikafanyiwa mfano wa yale ambayo nilifanyiwa jana, Al-Abbasi akaniwahi na kunikinga tena na  akasema maneno kama yale aliyoyasema jana.

4. Tufail bin Amru Al-Dawsy alikuwa ni mtu mtukufu, mshairi aliyekuwa na kipaji, kiongozi wa kabila la Da’ws. Kabila lake lilikuwa ni watu waliokuwa na Utawala au mfano wa utawala kafika maeneo ya pande za Yemen. Alifika Makka mnamo mwaka wa kumi na moja wa Utume. Watu wake wakampokea kabla ya kufika kwake Makka na wakampa maamkizi yenye heshima kubwa. Wakamwambia; “Ewe Tufail! kwa hakika umefika katika mji wetu, na mtu huyu aliye mbele yetu ametutia katika matatizo, amewagawa watu na kuvuruga mambo yetu, na kwa hakika maneno yake ni kama uchawi, anatenganisha mtu na baba yake, mtu na ndugu yake na mtu na mke wake. Kwa Hakika tunahofu juu yako na juu ya jamaa zako kukufikeni lile ambalo limekwisha kututokea sisi. Kwa hiyo tunakuomba usimsemeshe na wala usisikilize kabisa maneno yake.”

Tufail alisema; ”Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, waliniandama kwa maneno mpaka nikaamua kutosikiliza kutoka kwao kitu chochote na sikusema na yeyote mpaka wakati nilipokwenda Nikaziba masikio yangu kusikia maneno yake.” Alisema, ”Asubuhi nikaenda msikitinina ghafla nikamwona akiwa amesimama, anasali mbele ya Al- Ka’aba, nikasimama karibu yake na Mwenyezi Mungu Akataka nisikilize baadhi ya maneno yake. Kwa hakika nilisikia maneno mazuri sana, nikajisemesha ndani ya nafsi yangu; Anikose Mama yangu (niangamie). Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi ni mtu mwenye akili na ni mshairi, maneno hayajifichi yakiwa mazuri au mabaya, sasa ni kitu gani kitakachonizuia kusikiliza yale anayoyasema mtu huyu?. Yakiwa mazuri nitayakubali na yakiwa mabaya nitayaacha. Nikakaa mpaka alipoondoka kuelekea nyumbani kwake, nikamfuata mpaka alipoingia ndani mwake, na mimi nikaingia na kumweleza kisa cha kufika kwangu na jinsi watu walivyoniogopesha juu yake, na kuziba kwangu masikio, kisha kusikia kwangu baadhi ya maneno yake. Baada ya hapo nikamwambia, ’Nieleze jambo lako, akaueleza Uislamu kwangu na akanisomea Qur’an. Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu nilikuwa sijawahi kabisa kusikia maneno mazuri yaliyopangwa vema kabisa kuliko Qur’an, wala jambo lenye uadilifu mkubwa kuliko hilo. Nikasilimu na nikatoa shahada ya ukweli mbele yake.

Baada ya hapo nikamweleza kuwa mimi ni mtu ninayetiiwa miongoni mwa jamaa zangu na ninategemea kurejea kwao. Nikamuahidi kuwa nitawalingania watu wangu kwenye Uislamu kwa hiyo niombee Mwenyezi Mungu Anijaalie uwezo wa kulingania, akaniombea. Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akajaalia nuru usoni mwake mfano wa taa, na yeye akaomba; “Ewe Mola Wangu wa Haki ninaomba muujiza huu usiwe usoni mwangu, watu wasije kudai kuwa ni adhabu”, basi Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akaihamishia nuru ile kwenye fimbo yake.

Alipofika kwake akamlingania baba yake na mke wake kwenye Uislamu na wote wawili wakasilimu. Ama jamaa zake wengine wao wakawa wazito kuukubali Uislamu, lakini hata hivyo hakuacha kuwa nao akiwapa Da’wa mpaka alipohama baada ya vita vya Khandaq. (5)

Wakati wa kuhama kwake alihama na familia sabiini au thamanini za jamaa zake. Alifanya mambo mazuri kabisa katika Uislamu. Aliuawa shahidi katika vita vya Yamama.  (6)

5. Dhamadi al-Azdy; Huyu alikuwa anatokana na kabila la Azdi Shanua kutoka Yemen na alikuwa na ujuzi wa kutibu watu waliopatwa na pepo. Alifika Makka na kuwasikia wajinga wa Makka wakisema kuwa Muhammad ni mwendawazimu, akasema laiti kama mimi nitamuendea mtu huyu, bila shaka huenda Mwenyezi Mungu Akamponya kutokana na mikono yangu. Siku alipokutana naye akasema; “Ewe Muhammad kwa hakika mimi ninatibu watu kutokana na upepo mbaya, Je, uko tayari nikutibu? Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) akasema, ’Kwa hakika Sifa Njema Anazistahiki Mwenyezi Mungu (s.w.t) tunamsifu na tunamwomba msaada. Yule‘ ambaye Allah (s.w.t) Amemuongoza hakuna wa kumpoteza na yule ambaye Amepotezwa na Allah (s.w.t) hakuna wa kumuongoza na ninashuhudia kuwa hakuna Mala mwenye haki ya kuabudiwa ila Allah (s.w.t), hali ya kuwa Yuko Peke Yake hana mshirika na ninashuhudia kuwa Muhammad (s.a.w) ni Mja Wake, na Mjumbe Wake. “ Baada ya kusema maneno hayo akamwomba arejee tena maneno haya, akayarejea mara tatu. Dhamad akasema, ’Kwa hakika nimeyasikia maneno ya makuhani na maneno ya wachawi na maneno ya washairi, lakini sijawahi kusikia maneno mfano wa maneno haya, lete: mkono wako nikupe ahadi juu ya Uislamu’; akasilimu.


1) Ibid. Juzuu 1, Uk. 425-427. Rahmatun Lil ‘Alamin, Iuzuu 1, Uk. 74. 
2) Najib A-badi, Tarikhul Islam, Iuzuu 1, Uk. 125. 238
3) Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 427-428. Tarikhul Islam, Iuzuu 1, Uk. 126.
4( Suhihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 499-500, 544-545.
5) Pia inasemwa ilikuwa ni baada ya Hudaybiya, kwani alifika Madina na Mtume alikuwa Khaibar (Angalia, Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 385).
6) lbn Hisham, Juzuu 1, Uk. 382~385. Rahmatu Lil ’AIamin, Juzuu 1, Uk. 81
*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk 238-244

Begin typing your search above and press return to search.