AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Miaka Mitatu katika bonde la Abu Twalib Vikwazo vikazidishwa makali yake, wakazuiliwa kupata chakula na mahitaji mengine muhimu. Mushirikina hawakuacha chakula kilichoingia Makka isipokuwa walikinunua chote (ili wasikipate chakula kile walioamua kumlinda Muhammad) na mwishoni wakapata taabu kubwa sana (kwa kukosa chakula) na wakati huo chakula chao kikawa ni majani na ngozi. Sauti za wanawake na watoto zilikuwa zikisikika bondeni wakilalamika kwa sababu ya njaa.
Hakuna chakula kilichowafikia isipokuwa kwa njia ya siri. Katika bonde hilo hapakuwepo cha kununua isipokuwa katika miezi mitukufu na walikuwa wakinunua kutoka katika Misafara ya, kibiashara kutoka nje ya Makka. Watu wa Makka walikuwa wakiwazidishia bei za bidhaa maradufu wasiweze kununua.
Hakimu bin Hizam siku moja alikuwa anakwenda kuchukua ngano kumpelekea shangazi yake Bi Khadija (Radhi za Allah ziwe juu yake) akanutana na Abu Jahli. Akajaribu kumzuia Hakimu asipeleke Ngano kwa shangazi yake. Abu al-Bukhtar aliingilia kati na akamwezesha kuendelea na safari yake ya kumpelekea ngano Shaugazi yake.
Kwa sababu ya khofu aliyokuwa _nayo Abu Twalib juu ya Maisha ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alibuni utaratibu maalumu wa malazi yake, watu walipokwenda kulala yeye alimwambia Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ.) alale juu ya tandiko lake mpaka anaporidhika kuwa maadui walikuwa wakitaka kumvamia ili wamuue wameliona hilo. Pindi watu wanapokuwa wamelala alikuwa akimuamrisha mmoja wa watoto wake au ndugu zake watoto wa ammi yake kulala juu ya tandiko la Mtume Mwenyezi Mungu (ﷺ).
Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) na baadhi ya Waislamu walikuwa wakitoka katika masiku Matukufu na katika msimu wa makutano kwa ajili ya kukutana na watu na kuwalingania waukubali Uislamu.*