0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

97 DUA YA SAFARI

DUA YA SAFARI

الله أكبر، الله أكبر، الله أكبر،{سُبْحانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ * وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ}  “اللهم إنا نسألُكَ في سفرنا هذا البرَّ والتقوى، ومن العمل ما ترضى، اللهم هون علينا سفرنا هذا واطو عنا بعده، اللهم أنت الصاحب في السفر، والخليفة في الأهل، اللهم إني أعوذ بك من وعْثاءِ السفر، وكآبة المنظر وسوء المنقلب في المال والأهل

[Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, Mwenyezi Mungu ni Mkubwa; ametakasika ambaye ametudhalilishia sisi hiki (chombo au huyu mnyama) na hatukuwa sisi kwacho ni wenye uwezo, na sisi kwa Mola wetu tatarejeshwa.  Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakuomba katika safari  yetu hii wema na ucha Mungu, na katika matendo unayoridhia, Ewe Mwenyezi Mungu, ifanye nyepesi safari yetu hii, na ufupishe umbali wake, Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ndie Mwenzangu katika safari na Mchungaji wa familia yangu.  Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako kutokana na ugumu wa safari na ubaya  wa mtizamo na uovu wa kubadilikiwa katika mali na familia.]

Wakati wa kurudi safari atayasema hayo yalioko juu na kisha atazidisha:

[آيبون، تائبون، عابدون، لربنا حامدون]

 رواه مسلم2/ 978

[Tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, na Mola wetu tunamsifu.]         [Imepokewa na Muslim.]

DUA YA SAFARI  

 

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.