باب صفة طول القميص والكم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء
وعن أَبي سعيدٍ الخدْرِيِّ رضيَ اللَّهُ عنه قَالَ: قَالَ رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم “إزرَةُ المُسلِمِ إِلى نصْفِ السَّاقِ، وَلاَ حَرَجَ أَوْ لاَ جُنَاحَ فِيمَا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الكَعْبَيْنِ، فَمَا كانَ أَسْفَلَ منَ الكعْبَينِ فَهَوُ في النَّارِ، ومَنْ جَرَّ إِزارهُ بَطَراً لَمْ يَنْظرِ اللَّه إِلَيْهِ
رواهُ أَبُو داود بإِسنادٍ صحيحٍ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
119. MLANGO WA SIFA YA UREFU WA KANZU, MKONO (WA KANZU), KIKOI NA NCHA YA KILEMBA NA UHARAMU WA KUBURUTA SEHEMU KATIKA MAVAZI HAYO KWA KUFANYA KIBRI, NA KARAHA YA KUFANYA HIVYO IKIWA SI KWA KIBRI
Imepokewa na Abû Sa‘îd al-Khudry (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: “Mtume ﷺ amesema: “Kikoi cha Muislamu ni mpaka nusu ya muundi, wala hapana ubaya kufikia baina ya muundi na vifundo, kinachofikia chini ya vifundo ni motoni, na anayeburuta kikoi chake kwa kibri, Allâh Hatamtazama Siku ya Qiyama.” [ Imepokewa na Abû Dâwûd, isnadi yake ni Sahîh.]