0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

798. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Sifa Ya Urefu Wa Kanzu, Mkono (Wa Kanzu Kikoi Na Ncha Ya Kilemba Na Uharamu Wa Kuburuta Sehemu Katika Mavazi…

باب صفة طول القميص والكم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء


وعن قَيسِ بن بشرٍ التَّغْلبيِّ قَالَ: أَخْبَرنى أَبي وكان جَلِيساً لأَبِي الدَّرداءِ قَالَ: كَانَ بِدِمشقَ رَجُلٌ مِنْ أَصحاب النَّبيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقال لَهُ سهلُ بنُ الحنظَليَّةِ، وَكَانَ رجُلاً مُتَوحِّداً قَلَّمَا يُجالسُ النَّاسَ، إِنَّمَا هُوَ صلاةٌ، فَإِذا فرغَ فَإِنَّمَا هُوَ تَسْبِيحٌ وتكبيرٌ حَتَّى يأْتيَ أهْلَهُ، فَمَرَّ بِنَا ونَحنُ عِند أَبي الدَّردَاءِ، فَقَالَ لَهُ أَبو الدَّردَاءِ: كَلِمةً تَنْفَعُنَا وَلاَ تضُرُّكَ،. قَالَ: بَعثَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم سريَّةً فَقَدِمَتْ، فَجَاءَ رَجُلٌ مِنهم فَجَلسَ في المَجْلِس الَّذِي يَجلِسُ فِيهِ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم، فقَالَ لرجُلٍ إِلى جَنْبهِ: لَوْ رَأَيتنَا حِينَ التقَيْنَا نَحنُ والعدُو، فَحمَل فلانٌ فَطَعَنَ، فَقَالَ: خُذْهَا مِنِّى. وأَنَا الغُلامُ الغِفَارِيُّ، كَيْفَ تَرى في قوْلِهِ؟ قَالَ: مَا أَرَاهُ إِلا قَدْ بَطَلَ أَجرُهُ. فسَمِعَ بِذلكَ آخَرُ فَقَالَ: مَا أَرَى بِذَلَكَ بأْساً، فَتَنَازعا حَتى سَمِعَ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فقَالَ: “سُبْحان اللَّه؟ لاَ بَأْس أَن يُؤْجَرَ ويُحْمَد” فَرَأَيْتُ أَبا الدَّرْدَاءِ سُرَّ بِذلكَ، وجعلَ يَرْفَعُ رأْسَه إِلَيهِ وَيَقُولُ: أأَنْتَ سمِعْتَ ذَلكَ مِنْ رَسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم،؟ فيقول: نعَمْ، فما زال يعِيدُ عَلَيْهِ حَتَّى إِنّى لأَقولُ لَيَبرُكَنَّ عَلَى ركْبَتَيْهِ.
قَالَ: فَمَرَّ بِنَا يَوماً آخَرَ، فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْدَاءِ: كَلِمَةً تَنفَعُنَا وَلاَ تَضُرُّكَ، قَالَ: قَالَ لَنَا رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “المُنْفِقُ عَلى الخَيْلِ كالبَاسِطِ يَدَهُ بالصَّدَقة لاَ يَقْبِضُهَا”. ثُمَّ مرَّ بِنَا يَوْماً آخَرَ، فَقَالَ لَهُ أَبو الدَّرْدَاءِ: كَلِمَةً تَنْفَعُنَا وَلا تَضرُّكَ، قَالَ: قَالَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: “نعْمَ الرَّجُلُ خُرَيْمٌ الأَسَديُّ، لولا طُولُ جُمته وَإِسْبَالُ إِزَارِه” فبَلغَ ذَلِكَ خُرَيماً، فَعجَّلَ فَأَخَذَ شَفرَةً فَقَطَعَ بِهَا جُمتَهُ إِلى أُذنيْه، ورفعَ إِزَارَهُ إِلى أَنْصَاف سَاقَيْه. ثَمَّ مَرَّ بنَا يَوْماً آخَرَ فَقَالَ لَهُ أَبُو الدَّرْدَاءِ: كَلِمةً تَنْفَعُنَا ولاَ تَضُرُّكَ قَالَ: سَمعْتُ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: “إِنَّكُمْ قَادمُونَ عَلى إِخْوانِكُمْ. فَأَصْلِحُوا رِحَالَكمْ، وأَصْلحوا لبَاسَكُمْ حَتَّى تَكُونُوا كَأَنَّكُمْ شَامَة في النَّاسِ، فَإِنَّ اللَّه لاَ يُحبُّ الفُحْشَ وَلاَ التَّفَحُش”.    رواهُ أَبو داود بإِسنادٍ حسنٍ، إِلاَّ قَيْسَ بن بشر، فاخْتَلَفُوا في توثيقِهِ وتَضْعفيه، وقد روى له مسلم.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى




119. MLANGO WA SIFA YA UREFU WA KANZU, MKONO (WA KANZU), KIKOI NA NCHA YA KILEMBA NA UHARAMU WA KUBURUTA SEHEMU KATIKA MAVAZI HAYO KWA KUFANYA KIBRI, NA KARAHA YA KUFANYA HIVYO IKIWA SI KWA KIBRI


Imepokewa na Qais bin Bishri at-Taghliby amesimulia: “Baba yangu amenieleza – naye alikuwa akiketi na Abuddardâ (Radhi za Allah ziwe juu yake)-: “Dimishq (Syria) alikuwepo mtu katika Maswahaba wa Mtume , anayeitwa Sahli bin al-Handhwaliyyah, alikuwa ni mtu anayependa kuketi peke yake, ni mara chache mno kuketi na watu, alikuwa akishughulika na Swala, akimaliza kuswali huwa akileta Tasbihi na Takbir mpaka afike kwa familia yake. Akatupitia nasi tuko na Abuddardâ, Abuddardâ akamwambia: “Tuambie neno litakalotunufaisha wala halitakudhuru.” Akasema: “Mtume alituma kikosi (katika Jihadi), kikarudi. Akaja mtu miongoni mwao, akaketi katika majilisi anayoketi Mtume , akamwambia mtu alieketi kando yake: “Lau ungalituona tulipokutana na adui (ungalifurahi). Fulani alimshambulia adui na akamdunga (mkuki), akamwambia: “Chukua kutoka kwangu, mimi ni kijana wa ki-Alghifâry.” Waonaje katika maneno yake haya?” Akamjibu: “Nadhani kuwa ujira wake umebatilika.” Mtu mwingine akayasikia maneno hayo, akasema: “Sioni kama kuna ubaya katika hilo.” Wakaanza kushindana mpaka Mtume akasikia. Akasema: Subhânallâh! Hapana ubaya apewe ujira na asifiwe.” Nikamuona Abuddardâ amefurahishwa mno na jambo hilo, akawa akiinuwa kichwa chake kwa msemaji na akimwuliza: “Maneno hayo umeyasikia kutoka kwa Mtume ?” Naye akimjibu: “Ndio.” Basi akawa akimrudishia maswali mpaka nikasema kuwa asije akapiga goti juu ya magoti yake.

Yule Swahaba, akapita siku nyingine. Abuddardâ akamwambia: “Tuambie neno litakalotunufaisha wala halitakudhuru.” Akasema: “Mtume alituambia: “Mwenye kumlisha ngamia (wa Jihadi) ni kama mtu aliyeunyosha mkono wake kutoa sadaka wala haufumbi.”

Siku nyingine akatupitia. Abuddardâ akamwambia: “Tuambie neno litakalotunufaisha wala halitakudhuru.” Akasema: “Mtume   alisema: “Neema ya mtu ni Khuraim al-‘Asady! Lau kama si urefu wa nywele zake na kuburuta kikoi chake!” Khuraim akasikia habari hii, akaenda haraka akachukua kisu akakata nywele zake zikafikia masikioni mwake, na akapandisha kikoi chake hadi nusu ya miundi yake.

Kisha akatupitia siku nyingine. Abuddardâ akamwambia: “Tuambie neno litakalotunufaisha wala halitakudhuru.” Akasema: “Nilimsikia Mtume akisema: “Hakika nyinyi mtaenda kwa ndugu zenu, basi watengenezeni ngamia wenu na mavazi yenu mpaka muwe – katika watu – kama baka (mutambulikane kwa urahisi). Hakika Allâh Hapendi uchafu wala (mtu) kujijkalifisha kutenda uchafu.”   [ Imepokewa na Abû Dâwûd, isnadi yake ni Hasan.]


Begin typing your search above and press return to search.