باب صفة طول القميص والكم والإزار وطرف العمامة وتحريم إسبال شيء من ذلك على سبيل الخيلاء وكراهته من غير خيلاء
عن ابن عمر -رضى الله عنهما- أن النبي ﷺ قال: من جر ثوبه خيلاء لم ينظر الله إليه يوم القيامة، فقال أبو بكر: يا رسول الله، إن إزاري يسترخي إلا أن أتعاهده، فقال له رسول الله ﷺ: إنك لست ممن يفعله خيلاء. رواه البخاري
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
119. MLANGO WA SIFA YA UREFU WA KANZU, MKONO (WA KANZU), KIKOI NA NCHA YA KILEMBA NA UHARAMU WA KUBURUTA SEHEMU KATIKA MAVAZI HAYO KWA KUFANYA KIBRI, NA KARAHA YA KUFANYA HIVYO IKIWA SI KWA KIBRI
Imepokewa na ‘Abdullâh bin ‘Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: “Mwenye kuburuta nguo yake kwa kibri, Allâh Hatamtazama Siku ya Qiyama.” Abûbakar akasema: “Yâ Rasûlallâh, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kikoi changu kinateremka ila ninapokikaza.” Mtume ﷺ akamwambia: “Wewe si katika wanaofanya hivyo kwa kibri.” [ Imepokewa na Bukhârî.]